CIA walimuua Bob Marley?

Bora umesema huyu mvuta bangi alikua na nini haswa kiasi cha kufuatiliwa na CIA , watuw ajinga sana kwa kuamini kila lisemwalo kwnye internet .

Jamaica ilikuwa ni nchi yenye upinzani mkali wa kisiasa.Vyama viwili vikubwa vya kisiasa nchini humo wakati huo vilikuwa ni Jamaica Labour Part(JPL) kilichoongozwa na Edward Seaga na chama cha Peoples’National Part kilichoongozwa na Michael Manley.Ghasia za kisiasa zilitokea mara kwa mara. Michael Manley na chama chake cha Peoples’National Part wakiwa madarakani chama chao kilikuwa kinaeneza ujamaa na wa kisaidiwa na Fidel Castro wa Cuba, wakiwa na lengo kueneza ujamaa visiwa vyote vya Caribean Hii haikuwa habari njema kwa adui mkuu wa ujamaa Marekani, kwa kulitumia shirika lake la ujasusi, CIA Marekani ikapanga kumdhibiti Michael Manley kwa njia mbili; kumwandalia mpinzani watakae msapoti kwa kila kitu. Akaandaliwa Edward Seaga kupitia chama Jamaica Labour Party, Wakamwezesha kwa kila kitu wakati ukikaribia uchaguzi mkuu uliokuwa ukifuata 1976. Pili; kumchonganisha Michael Manley na wananchi, wakatengeneza mazingira ya vurugu, Jamaica ikashuhudia mauaji makubwa mitaani, vurungu mateso na kila aina ya ubabe, Nchi ikawa inaelekea kutotawalika. Ili mkakati huo ufanikiwe zaidi ni lazima wananchi wawe upande wa mpinzani mkuu kibaraka wa Marekani Edward Seaga hivyo CIA wakapanga kumtumia Bob Marley kwa namna yoyote, Bob alikuwa ni habari nyingine kwa wa jamaica kwao alikuwa ni super star mkubwa kabisa. CIA waliamini kuhusika kwa Bob kwenye harakati zao kungesaidia kuwavuta watu kuwa upande wao. Kwanza wakataka kumuua ili kuwaminisha wananchi serikali iliyo madarakani imeshindwa kuwalinda raia wake, hivyo wamkatae Michael Manley na wamchague Edward Seaga kwenye uchaguzi ujao. Wakamvamia Bob nyumbani kwake na kumpiga risasi, lakini kwauwezo wa Mungu alinusurika kifo. yeye mwenyewe alishtukia ule ulikuwa mchezo mchafu wa CIA alipotoka hospitali, akawatungia wimbo wa AMBUSH IN THE NIGHT

Ambush in the night all guns aiming at me, Ambush in the night They opened fire on me now, Ambush in the night, Protected by his majesty


Walinivamia usiku wa manane bunduki zote zilielekwezwa kwangu, wakanifyatulia risasi nikalindwa na aliye mkuu Mungu Mara nyingi Bob hakuwa akiwataja majina anaowalenga kwenye mashairi yake ila alitumia mafumbo rahisi ambayo watu wakawaida waliweza kuyafumbua na kuelewa alicho maanisha. Hata kwenye AMBUSH IN THE NIGHT, Bob hakutaja majina ya aliowatuhumu kujaribu kumuua bali alielezea sifa zao. See them fighting for power,
But they know not the hour,
so they bribing with their guns, spare-parts and money, trying to belittle our integrity now .
they say what we know
is just what they teach us;
And we’re so ignorant
Cause every time they can reach u
through political straterg.​


Waone wanavyopigania madaraka,
Hawajui saa yenyewe watakayoyapata hayo madaraka
Hivyo wanatoa hongo na bunduki zao vipuri na pesa,
Wakijaribu kutushushia heshima yetu ,
Wanasema kile tunacho kijua ni kile tu walichotufundisha,
Na kwamba eti sisi ni wajinga kwa sababu wakati wowote
Wanaweza kutufikia kwa mikakati yao ya kisiasa.



Sifa hizi ni za Marekani na Wakala wake mkuu CIA , Wao ndiyo waliokuwa wakihonga silaha kwa magenge ya wahuni kufanya vurugu. Wao ndiyo waliokuwa wakitoa pesa kufadhili harakati za kuidondosha serikali ya kidemokrasia ya Michael Manley .



Baada ya kushindwa kumuua Bob Marley CIA wakamshawishi awe upande wao ili kuwavuta wananchi , walijua wakifanikiwa kupata uungwaji mkono na Bob watakuwa wamepata uungwaji mkono na wajamaica kwa sababu wajamaica walimsikiliza na kumwamini sana Bob, Bob akakubali kwa sharti la kuwapatanisha kwanza Michael Manley na Edward Seaga Bob aliamini wanasiasa hao wakipatana mtaani kutakuwa hakuna vurugu tena .

Baada ya wanasiasa hao kupatanishwa Bob akatunga nyimbo ya RAT RACE nyimbo ambayo iliwalenga wabaya wake CIA. DON’T INVOLVE RASTA IN YOUR SAY SAY RASTA DON’T WORK FOR NO CIA. Bob Marley alikuwa habari nyingine aliimba vitu vingi ambavyo vinatoke na vitazidi kutokea.
 
Nzuri hii na umenikumbusha jinsi Bob Marley alivyowashikisha mikono hawa jamaa Manley na mwenzake kwenye One Love Peace Concert
 
Kimsingi Rasta yeyote mala nyingi hua na mawazo angavu na yenye nguvu.Rasta hutumia muda mwingi kutafakali kwa mapana juu ya haki na upendo.so Bob Marley alikua hivyo na baada ya kutafakali kwake aliibukia kwenye kutunga nyimbo zenye ujumbe unaorudisha mahusiano na upendo kwa watu wote,mzungu nae siku zote hapendi kuona watu weusi wanakua wamoja wenye nguvu.sasa mzungu anapokutana na ujumbe kama wa Bob Marley hukasirika na kujaa gadhabu inayompelekea hata kuua.kiufupi hicho chaweza kua ni kweli aliuawawa na watu wabaya kwa kusema ukweli

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
kwa style hii nahisi hata babu yangu aliuawa na CIA .... ngoja nikaulizie kule kijijini maana naye ilikuwa pale kijijini ana wafuasi wengi na akawa anawapiga neno hasa kuwa wajikwamue...mwisho akaja akafa kwa kuuawa na CIA bila shaka.
 
Kama CIA, huwa hawashindwi kuuana wao kwa wao kwa hiyo hawashindwi kumua mtu kama Bob Marley.

Nasikia hata yule nani sijui wa Taifa wanahusishwa hao CIA na MI6.
 
Aisee
 
sishangai kwani CIA walimuua hata Rais wao JF Kennedy

Daaah...hii inasikitisha sana mkuu

jimmy Hendrix,James Brown waliuwawa ns hao hao

alikuwa na impact gani hadi wazee wa kazi a.k.a wazee wa mission CIA wamuue?????? au bange zake tu zilimzidia.

Hawa jama ni hatari

Wafuatao ni wahanga wa mauaji yaliyofanywa na CIA
Bob Marley
JF Kennedy
Ernesto che Guevara
Patrice Lumumba
Hugo Chavez

Ongezea unaowajua wengine...

Jamaa sio wa mchezo, waliwatungua hadi Tupac na Notorious BIG
 
Mbona Kennedy hakujiunga na hao jamaa na alikula punch.......

Yeye anawakataa wakamtia tanuruni
Kennedy kilichomuua ni mazingira ya uvamizi wa Bay of the Bigs 1961. Inasemekana kukataa kutoa amri ya kupigwa mabomu Cuba ili kusambaratisha walinzi wa pwani wa Cuba, kulisababisha wavamizi kushindwa na majeshi ya Fidel na aibu kuwafikia vinara wa Kijeshi nchini Marekani. Hoja nyingine ni Vietnam. Hakusamehewa, fuatilia simulizi mbalimbali hasa mkanda wa HolyWood wa JFK uliotolewa 1991.
Kevin Costner: Oliver Stone's JFK: JFK assassination investigation ...
www.jfk-online.com/jfkcostner.html
 
Basi CIA wakati mwingine huwa wanakosa kazi za kufanya.
Walianzaje kuhangakaika kumuua yule mvuta bangi?

Sent using Jamii Forums mobile app
For you bob alikua mvuta bangi kuna waliomuona alikua play boy kuna waliomuona ana alama za sias pale alipozulu zimbabwe kuna waliomuona mwokoz na mwanageuz kupitia nyimbo zake ukijakuangalia cia huua mbegu kabla hazijaleta madhara katika jamii na hili walilifanya hata kwa wale akina 2pac nA mwenzake notorious big nadhan kuna uz humu upo kwa wale members wa jf toka kitambo wanaweza kujua nazungumzia nini kuhusu vifo vya hawa wana hiphop wawili american inteligence wapo vizr hata ukija fuatililia kifo cha malcom x kilikua n lazima kwao ingawa wakisingiziwa kikundi kimoja cha kiislam kuwa kimemuua lakin cia walihusika watu weng mashuhuri duniani wanapotea au walikiwa wanapotea (hufa) pale tu wanapoanza kwenda kinyune na matkwa ya america na tamaduni zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…