CIA na Viongozi Wa Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CIA na Viongozi Wa Afrika

Discussion in 'International Forum' started by Kichuguu, Aug 31, 2008.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi kama kweli CIA huwa inafanya utafiti wa kutosha na kuwafahamu sawasawa viongozi wa kiafrika; mara nyingi huwa wanakosea. Kwa mfano walisema Mkapa alikuwa Kiongozi mzuri sana aliyekuwa akipendwa sanana na watu wake. Ukweli ni kuwa Mkapa aliondoka madarakani akiwa anachukiwa hata na watoto wadogo. In fact, wakati wa mwisho wa utawala wake, Mkapa alifanya jitihada sana za kushawishi watu wakubali kuwa ameleta maendelea sana Tanzania. Mara baada ya Kikwete kuingia madarakani, amekuwa akimwagiwa sifa nyingi sana kuwa ni kiongozi shupavu sana na mwenye nia kubwa ya kuwaondoa watu wake kutoka kwenye umaskini. Ukweli ni kuwa Kikwete hana mpando wowote wa kuwaondoa watu wake kwenye umaskini, ndiyo maana anela ufisadi kama vile haupo.


  Zaidi zadi, kilichonifanya nijiulize swali hili ni jinsi walivyokuwa wanam-characterize Nyerere eti ni mtu asiyekuwa shupavu kiuongozi kiasi kuwa anasukumwa na wafuasi wake tu; yeye mwenyewe hawezi kujiamulia. Je ni kweli kuwa Nyerere alikuwa "Weak" leader? Hebu angalia ripoti hii ya CIA ya mwaka 1965.
   

  Attached Files:

  • CIA2.pdf
   File size:
   538.5 KB
   Views:
   80
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  CIA,could never have liked nyerere,for the simple reason,he was not dancing to their tune,hawa wengine wanaonekana positive,cause hata hiyo tune haijaanza kulia, wao washaanza kucheza
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwalimu Kichuguu,

  Nyerere was a strong man who could stand tall and declare his mind and independent, that is why he was hated.

  Si unajua jinsi gani FBI walikuwa na dossier ya Martin Luther King na Malcolm X na kuwachafua majina huku hawa jamaa wakiwa ni wanamapinduzi wenye falsafa bora?

  Sasa hao hao CIA, walimuona Mobutu kuwa ni shujaa bora kuliko Nyerere, waulize leo nani alikuwa bora.

  Sasa hivi tuna kizazi cha viongozi wavivu na wazembe wa kufikiri. Viongozi wengi si imara na hawana uhuru wa kufikiri na kujenga misingi imara ya kujitegemea.

  Angalia jinsi Kikwete anavyokuja hija Marekani, karibu mara tatu kwa mwaka tangu awe Rais, ukiuliza maendeleo ya kweli unasikia ni makampuni ya kigeni ndiyo yanapata faida kila siku, lakini siye tunalia umasikini.

  We have a class of leaders who are looking forward to be puppets of Developed countriesl. I am not sure why, but we need to ask them tough questions and tell them to stop this BS of bilatteral relationship crap!
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  CIA ndumila kuwili.
  Hawawezi kutushawishi sisi Wa tz kukubaliana na maslahi yao hapa nchini.
  Wanaweza kusema kiongozi huyu ni mzuri wanavyotaka lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Kikwete kashindwa.
  Hata wasemeje. Kashindwa. Na ukweli Kikwete alikuwa anaingia kualizia ulaji wa nchi hii.
  Ole wetu na wanetu maana watu wataamka nchi ikiwa haina chochote.
  Wakati Tanzania sera ni kuiba kiasi uwezavyo ukiingia madarakani, Marekani sera zake ni kusifia wanakoiba au kupata support kwao ya kuweka military base.
   
 5. I

  Iga Senior Member

  #5
  Sep 1, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi tuna kizazi cha viongozi wavivu na wazembe wa kufikiri. Viongozi wengi si imara na hawana uhuru wa kufikiri na kujenga misingi imara ya kujitegemea.


  Angalia jinsi Kikwete anavyokuja hija Marekani, karibu mara tatu kwa mwaka tangu awe Rais, ukiuliza maendeleo ya kweli unasikia ni makampuni ya kigeni ndiyo yanapata faida kila siku, lakini siye tunalia umasikini.

  We have a class of leaders who are looking forward to be puppets of Developed countriesl. I am not sure why, but we need to ask them tough questions and tell them to stop this BS of bilatteral relationship crap!


  Na Rev. Kishoka
  __________________

  Rev. Kishoka,

  Yapo mengi ninayoweza kuzungumza kuhusiana na swali/maswali yako hapo juu. Lakini kwa leo naomba nizungumzie tu sababu zinazowafanya baadhi ya VIONGOZI wetu Afrika wenye HESHIMA zao kutaka kuwa vibarakala wa Marekani au nchi za Magharibi.

  Kabla sijaongolea yangu kwanza naomba kama utaweza kufanya kautafiti kadogo kuhusu ni nchi gani hasa inayomimina MISAADA kwa Tanzania? Mimi ninaamini nchi hiyo si Marekani. Lakini propaganda na public relations machinery ya watu wao inafanya ionekane kama vile hivi sasa Tanzania inapata misaada kebekebe toka huko kwa mayankii! Si kweli hili. Naomba lithibitishe na baadhi ya misada tunayopewa ni ile iliyoahidiwa na Democrats miaka 45 iliyopita!

  Haijawahi katika historia ya nchi yetu sisi kuwa marafiki wa karibu sana na viongozi wa Republicans. Maana viongozi hawa Baba wa Taifa aliwajua ndio hao hao wafanya biashara wa haramu ikiwemo silaha, madawa na wizi wa madini toka Sierra Leone hadi Kongo, Paraguay hadi Burma!

  Ninayotaka kuwajuza wenzangu leo ni kuwa viongozi wetu Afrika wanakubali kuwa watumwa wa viongozzi wa nje kwa sababu zifuatazo. Hizi ni zile nilizoweza kuzifikira haraka haraka baadaye zaweza kuzuka mpya:

  [Naomba Rev. Kishoka uwe shuhuda wa haya na watafiti wa Kitanzania na wote wenye uchungu na nchi hii wayafanyie kazi haya na majibu yao wayaweke bayana ili tujue kunguni na chawa wanaotuhangaisha usiku na mchana wako wapi?

  KUTOKUWA NA VISHENI
  KIONGOZI yeyote anayekuja madarakani bila kuwa na AJENDA au WITO wa kuisaidia nchi na watu wake kupiga hatua moja au mbili mbele hawezi akafanya lolote ila kwa kuongoza na nchi kubwa na vyombo vya wakubwa kama vile Benki Kuu, IMF na wengineo ambao sote tunajua kuwa USHAURI wao na DAWA zao mara kadhaa zimemuua badala ya kumsaidia mgonjwa.

  KUDHANIA UONGOZI NI KITU CHA MTU MMOJA
  UONGOZI ni dhamana. Dhaman anayopewa mtu mmoja lakini anayotarajiwa kwayo kugawa madaraka ili wengine wamsaidie kufanya yale wanayoweza kufanya bila yeye na yeye aachiwe yale tu ambayo ni yeye tu anayoweza kuyafanya. Katika nchi ambayo Waziri wa Michezo kakaa pembeni-michezoni inaporomoka yeye kimya, michezo inakufa yeye kimya, je, huoni kuwa hapa kwamba bwana huyu kapewa cheo bila kazi na juu ya yote mshahara wa bure. Hatima ya yote eti mkuu wa nchi ndiye anayekuja kuifanya kazi ya Waziri. Ama ukweli ni kuwa mkuu hataki mtu amsaidie kazi hiyo; au waziri husika hana uwezo na kazi hiyo. Kwa vyovyote vile iwavyo hapa ni kuwa nchi haina uongozi bora! Na uongozi wa namna hii utaishia kujiweka kwapani kwa viongozi wa nchi nhyingine ili anusuriwe, alindwe na ahakikishiwe kuwepo madarakani kwa kupewa pipi, tende na halua za kuwagawia watu bure ili wasilalame lalame sana....

  KUTOJIAMINI
  Mtu yeyote asiyejiamini hawezi kufanya jambo ila kwa ushauri wa mtu au watu wengine. Anaogopa lawama, anaogopa kushindwa. Lakini mwisho wa yote kama wanaokushauri ni bomu na wewe mwenyewe unakuwa bomu!

  KUTOWATHAMINI RAIA WA NCHI YAKO
  Nchi nyingi za Kiafrika zinamuona Mzungu au Mjapani au Mchina ni bora zaidi kuliko mtu mweusi. Yaani rais wa watu weusi anawaona watu wake ni takataka, hawana akili, hawana jipya na hakubali ushauri wao ila ushauri wa watu wenye ngozi za rangi nyingine. Na hili sio kwa sababu ngozi nyingine zina akili bali kwa kuwa 'wameendelea' kwa namna yao na wana fedha.

  Kiongozi wa maana Afrika atakuja pale tu ambapo mmoja wetu ataionesha dunia kuthamini zaidi ngozi nyeusi kuliko ngozi nyingine. Hii wenzetu Marekani wanaita ni kitu Positive Affirmation!

  Katika hili na sisi waswahili tuna mengi ya kujirekebisha. Nchi isiyokuwa na maadili au vigezo vya tabia zinazokubalika. Nchi inayolishwa tamaduni nyingine na kuzimeza nzima nzima haiwezi ikawa na maendeleo ya kweli na ya kudumu!

  Kwa bahati mbaya hiyo ndiyo Tanzania yetu. Hatuna maadili ya Mtanzania. Yaani kitu kinachotuonesha huyu bwana ni Mtanzania. Huyu bibi si Mtanzania. Na hili halihitaji wala makubwa ni makongamo tu ya kitaifa ili wananchi waamue tunataka tutambulike kama taifa la MAFISADI au WATU SAFI; WAZINIFU au WATU WANAOHESHIMU NDOA ZAO; WEZI au WAAMINIFU; WASAFI au WACHAFU: WENYE HURUMA au WATU MAKATILI; WACHA MUNGU au WAOVU na kadhalika.

  Ni lazima tukatae kisicho maadili ya Kitanzania kwenye vyombo vyetu vya habari. Lakini hili gumu hata kwa Tanganyika Broadcasting Corporation [TBC] je, tunapata picha gani toka chombo kinachotumia fedha za kodi yetu katika kulinda na kuendeleza utamaduni wetu? Hata TV ya Taifa inaabudu mpira wa Waingereza kuliko wa Wajerumani au Wabrzil na Waarjentina? Achilia mbali wa Afrika?

  Dhambi kubwa ya chombo chochote cha habari kwanza, ni kuua utamaduni wa taifa, ambayo ndio raha ya taifa na pili ni kuiingiza nchi kwenye matatizo yanayochangia kuvunja umoja na amani ya watu.

  UBIA WA KISIRI SIRI NA VIONGOZI WA NJE
  Zipo tuhuma kwamba viongozi wengi wa Kiafrika sasa wameanza kuingia ubia na viongozi wanaostaafu huko Magharibi. Mojawapo ni papa hapa Tanzania ambapo eneo zima la kutoka Mbamba Bay hadi bandari ya Mtwara limeshauzwa kisirisisri kwa ajili ya madini yanayopatikana sehemu hizo.

  KULIPA FADHILA
  Wakati mwingine nchi tajiri huwa zinawasaidia viongozi fulani kuingia madarakani. Kwa hiyo kuna kuwa na deni linalodaiwa mtu huyu linalogeuzwa deni la nchi. Lazima lilipwe. Kutegemeana na uwezo wa kisiasa wa mtu wale dhaifu wanaweza wakauza mpaka nchi nzima kwa watu wa nje katika kulipa fadhila za huko nyuma.

  SHULE KWA WATOTO
  Mamia ya watoto wa viongozi wa Kiafrika wanapelekwa Marekani na Ulaya kusoma. Ili kuhakikisha kuwa watoto na ndugu na jamaa zao wanaendelea kukubalika kwenda kusoma huko ni lazima mtu auze kiasi fulani cha nchi yake!

  SHOPPING KWA KINA NANIHINO
  Na kina mamaa, dadaa na shangazii na kina nanihino lazima wawe na mahala ambapo wanaweza kununua nguo zao za ndani, marashi yao, viatu vyao, nywele za bandia na vipodozi vingine.

  Hili pia kutegemeana na nguvu ya mwanamke laweza sababisha kiongozi wa Afrika kuiuza nchi bila kujua!

  KUSHINDWA KUJIFUNZA TOKANA NA HISTORIA
  Kweli kama alivyosema Rev. viongozi wetu wengi wavivu wa kuwaza na kuwazua, walegevu wa fikira na vipofu wa maono na visheni!
  Si hayo tu ni wavivu hata wa kuwaomba wasaidizi wao kuwasomea historia ya wale waliotutangulia.
  Kwanini Nyerere aliwaogopa Wamarekani kama ukoma? Jibu au majibu yapo. Nani kayatafuta. Hawa ni watu ambao siasa na utu wao ni bora kuliko siasa na utu wa watu wengine. Maslahi yao yanakuja mbele ya hata dunia nzima. Na hakuna la kuwazuria pale wanapokutaka ukawakubali kisha ukawakataa. Unakumbuka hadithi za masolja wanaokataliwa na washikaji wao wanapochukua silaha kwenda lindoni kumbe anarudi kwa aliyemnyakulia kimwana na kumlipua yeye na mwanamke wake? Solja hujilipua, Mayankii sivyo hawajilipui! Jifunze toka Marekani ya kati na kusini, Vietnam, Masharikik ya kati na mjue hatua ya nne ni Afrika na Tanzania.

  Amani na umojawa Watanzania hautabomolewa na Watanzania wenyewe bali Wamarekani ambaye Baamkubwa anawafungulia milango yote kwa hivi sasa.

  Tusijidanganye kwamba ni Bush au Obama au McCain anayetawala Marekani sio hivyo. Anayetawala Marekani sio rahisi jamani bali ni wafanyabiashara wakubwa wenye migodi ya madini kama Barracks, Mabenki na biashara zingine....

  UWEZO MDOGO wa MENEJIMENTI NA UTAWALA
  Wengi waliosomea sosholojia na sayansi ya siasa hawafui dafu inapokuja kwenye maswala ya menejimenti na utawala. Na kwa sababu hii ili kuficha udhaifu wao hawawataki wenye uwezo kimeneja na kitawala bali huzungukwa na wanasosholojia na ngwini wengi tu kama wao walivyo. Matokeo yake nchi inayumba, inapotea stepu na kisha kwa msaada wa rafiki wa kweli na urongo mamboyanakuwa si mambo!

  KUTOKUWA NA WATU WANAOFAA CHINI YAKO

  Hii ina maana kwamba kiongozi anayezungukwa na watendaji dhaifu hana atakalolifanya ila kuwarudia tena wageni kuomba ushauri na utaalamu ambao kama angezungukwa na watu wanaofaa kwa kazi hizo basi pasingelikuwa na lazima ya kuliingiza tena taifa kwenye gharama nyingine.

  UWEZO DUNI WA KUPITIA TAARIFA NA KUMBUKUMBU ILI KUFANYA MAAMUZI SAHIHI

  Kwa sababu ya uvivu na ulegevu wao viongozi wengi wa Kiafrika hawana muda wa kupitia taarifa kwa ukamilifu na kufanya maamuzi sahihi. Matokeo yake ni kuingiza nchi kwenye tatizo hili toka tatizo lile. Wsilkilize Resident Presidents -BBC na utapata picha kamaili ya kiongozi wa Kiafrika na jinsi asivyohifadhi yaliyo muhimu lakini mwepesi wa kuhifadhi upuuzi.

  KUCHANGANYA MASUALA YA UCHUMI NA SIASA
  UNAPOKUWA na nchi ambayo siku zote siasa hujui inaishia wapi na uchumi unaishia wapi basi matokeo yake ni kwamba hata yaliyo rahisi yanakuwa magumu. Matokeo yake unawatafuta watu weupe kuja kuwashauri watu kuhusu ujinga wanaoufanya na ujinga huo wanaujua lakini mzungu hajui na hatakaa aujue!

  MFUMO MBOVU WA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI
  Hivi tunajua kwa mfano waziri wa vijana, utamaduni na mcihezo anatakiwa kufanya nini ili kuendeleza utamaduni wetu; ili kuendeleza wanamichezo na michezo; au kuwapatia vijana wasio na ajira kazi; au kuwapa mbinu za kujiajiri?
  Naamini sio rahisi kama anajua hili. Wengi nadhani wanaamini kazi yao ni kuja na shangingi l enye airconditioner; kukaa kwenye ofisi yenye airconditioner; kusoma magazeti na sikuhizi kusikiliza FM na kutazama redio na ikifika saa kumi hajui watu wa chini wamefanya nini. Yeye mwenyewe hatathminiwi na yeye atatathmini vipi? Mkuki kwa nguruwe, bwanae....

  Nchi hii tunadanganyanya tu....

  Kwa hiyo utawakaribisha Wamarekani wakuletee OPRAS sio au? Bilioni kadhaa zinatumika ili mzungu amfundishe Mtanzania jinsi ya kujitathmini ili ajue anafanya au hafanyi kazi kikweli kweli?

  KUSHINDWA KUGAWA MADARAKA ILI WIZARA NA MIKOA IJIENDESHE

  HIVI Tanzania ingelikuwa papa hapa tulipo kweli kama Wizara zingekuwa na uhuru wa mwisho kuamua juu ya mambo yaoe. Na pengine wizara nyingine zingelikuwa kwenye kanda zinazotahili kuwepo kuliko hapa Dar au Dodoma?

  NA mikoa nayo ikiwa huru kujiendesha kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutafuta wawekezaji kama ilivyo hapa India, je, hakuna mikoa itakayoweza kulipa msihahara ya Watanzania wote?
  Mbona kuna mikoa mingine mikubwa kuliko Rwanda na Burundi? Iweje hatuoni ukweli huu wa madaraka ya kiuchumi mkoani kwa wanamkoa?
  KUZUNGUKWA NA MASHABIKI BADALA YA WATU WENYE FIKIRA NA UWEZO WA KUBADILI MAMBO
  MATOKEO ya kuzungukwa na watu wa ndio mzee, ndio mzee na wanaotetea hoja za mkubwa bila kuzipangua na kuzipanga upya ili kupata chenga na mchele sio jambo jema.
  Matokeo yake kwa mara nyingine ni hao sycophant kuanza ooh, hawakupendi mzee, hawakutakii mema mzee, kumbe tatizo au wasiomtakia mema mkuu ni hao hao wanaomzunguka! Hivi dunia ya leo utazungukwa na maofisa wasiosoma hata kitabu kimoja kwa mwaka, makatibu wakuu ambao darasa lao ni Daily News na Habari leo -basi!
  Baba wa Taifa hakuwa na doctorate bwanaee lakini vitabu viwili -vitatu kwake ilikuwa mchezo?

  Teknolojia ipo leo pia ya vitabu vinavyojisoma vyenyewe -wewe washa DVD yako kitabu kinajisoma chenyewe na wewe kazi yako kusikiliza tu. Tufunguke macho viongozi!

  OBSESSION NA AJENDA MOJA AU MBILI ZISIZO NA UMUHIMU MKUBWA
  KUNA nchi zime speshalaizi kwenye kudanganya nchi masikini kwamba viajenda vidogo vidogo ndio masuala muhimu kweli ya kitaifa. Viongozi wakuu badala ya wahusika wanaishia kupoteza muda wao kwenye kufanya yale ambayo hayakustahili kufanywa nao.

  Hivi ajenda yetu ni kondomu na ukimwi na upimaji wake kweli? Au hii ni kazi ya Wizara husika? Hivi ajenda yetu ni kuwa na shule kweli au Hazina na Wizara zinatakiwa kufanya kazi hii usiku na mchana? Ajenda ya kiongozi ni kuona kila wizara na kila mtu anatoa na hakwamishwi kutoa mchango wake katika maendeleo ya nchi yake na sio vinginevyo. Ikiona kiongozi anaanza kufanya kazi za Wizara fulani basi ndugu hapo hamna kiongozi!

  UWEZO DUNI WA KUTUMIA ICT KURAHISISHA KAZI

  Teknolojia ya habari na mawasiliano inaweza kusaidia sana katika kazi za uongozi wa nchi.

  Lakini zaidi ya website ya taifa, je, kuna wizara au idara gani zenye website ambazo waziri, katibu mkuu na watendaji wao wanaweza kuzitumia katika kupanga, kuratibu, kudhibiti na kuongoza utendaji wa kazi katika wizara zao? Jibu nadra kukuta kitu kama hiki Tanzania.

  Kanch ka Jamaica chenye watu milioni 3 tu lakini wanatushinda akili. Wanamichezo wao wote ikiwemo wanariadha wako kwenye mtandao na kwa kutumia tovuti wanaweza kuwasiliana na viongozi ikiwa ni pamoja na waziri wa michezo na Waziri Mkuu bila wasiwasi..... na maamuzi muhimu yakafanyiak katika sekunde chache.

  Tunawaambia mawaziri wetu nyie kaeni huko kwenye viyoyozi, mkija shuka chini mtakuta utandawazi umetunyoa wote huku mitaani na badala ya kupokelewa kwa mapenzi mnajua mtakachokiona?
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Naomba niongeze, japo nitatoka katika mada kidogo. Sehemu kubwa ya yale maendeleo ambayo yamafanyika wakati wa Mkapa ni mikopo ya muda mrefu kutoka taasisi za fedha za kimataifa, fedha ambazo tuliona kama "fadhila" toka kwa "wafadhili" maana hata Benki ya Dunia huwa tunaiita "mfadhili"... fedha hizo tutaanza kuzilipa wakati ambao Mkapa, Kikwete watakuwa hawapo na pengine itakuwapo serikali ya Rais wa chama kingine ambaye ataonekana ameshindwa kazi kwani mzigo wa madeni utakuwa ni mkubwa mno. Nakumbuka barabara nyingi, miradi mingi (mingine hewa) ilikuwa "inafadhiliwa" na benki ya dunia na waandishi wetu wanaendelea kuimba, "INAFADHILIWA" na beni ya dunia au ADB..... Kwa wanaojua zaidi na data watusaidie tujiandae sisi ama wajukuu zetu kulipa madeni hayo ya fedha ambazo nyingine zimenunua rada na ndege ya Rais GS50
   
Loading...