Chura kiumbe wa karne

Chura kiumbe wa karne

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,332
Reaction score
10,913
Ugonile Wakuu!!

Kalagabao Joka ndani ya nyumba kila mtu anahaha. Ukweli ni kuwa Joka ndiye kiumbe anayeogopeka na watu wengi kuliko kiumbe yeyote duniani. Licha ya kuwa kiumbe huyu hana miguu lakini mwonekano wake ni wakustaajabisha na kuogopesha mno.

Habari ya Joka niachieni mimi. Niende kwenye mada husika. Duniani imepitia mapinduzi mengi sana. Kuna mapinduzi ya kilimo(Agrarian revolution), mapinduzi ya viwanda(industrial revolution na mapinduzi makubwa ya kiteknolojia yaliyotokea mwishoni mwa karne ya ishirini.

Hivi karibuni kabisa ulimwengu unapitia katika mapinduzi yakipekee. Mapinduzi ambayo hayajawahi kutokea tokea dunia ianze. Mapinduzi ya kiumbe Chura. Chura ni mnyama bora wa karne hii yenye watu wenye akili, utashi, maarifa na elimu za kila namna. Ule usemi wa kelele za chura hazimnyimi tembo kunywa maji Chura kaupoteza. Mpaka sasa ninapozungumza Tembo hathubutu kabisa kutia mkonga wake majini si tu asikiapo kelele za chura bali hata akihisi chura yupo eneo hilo. Basi Tembo na ukubwa wake lazima akunje mkonga wake na kuunyanyua juu na kupasa sauti kali za hisia.

Mapinduzi ya Chura mpaka sasa haieleweki ni medani gani imetumika mpaka watu wamshangae chura na kumsujudia. Chura amepata ushawishi mkubwa si tu majini huko alipokuwa akipiga kampeni zake ambazo wengi waliziita kampeni za maji taka. Lakini Ushawishi wake sasa umeingia si mitaani tu bali hata majumbani mwa watu.

Chura kwa sasa ndiye kiumbe apewaye heshima kuliko kiumbe mwingine. Mataifa yote wanamsujudia, wanamhimidi na kumshangilia. Wanastaajabu madoido na vingorimbo vyake. mapozi na mikogo yake wengi wamejikuta wakimfurahia.

Chura apitapo mtaani vijana, vizee na vitoto vyote vinainama kwa adabu iliyotukuka. Baadaye humuangalia kwa nyumba chura adundapo na kurukaruka kwa shangwe. Vijana huvunja shingo zao wapende wasipende chura apitapo. Nasikia kuwa ukimtazama chura unapata tiba ya moja kwa moja ya kihisia bila malipo.

Chura huko mitandaoni amechafua hali ya hewa. Kila mtandao wanampigia chapuo. Wanamuziki nao wanamtukuza kila iitwapo leo. Wengi husisimuliwa kwa michezo yake ya dansi pindi atembeapo. Heshima aliyonayo chura japo si chakula imezidi kushinda kitimoto. Chura ni kinara wa kuvunja ndoa za watu hasa pale ukishindana nae. Chura kwa sasa ndiye mtawala wa dunia katika karne hii. Tena nasikia utawala wake unaweza kudumu kwa karne nyingi zaidi.

Chura wewe ni nani hata ututese vijana. Wewe ni nani unayefilisi vizee na pensheni zao. Unayeharibu akili za viongozi wakubwa wa nchi na kukupa mali ya wavuja jasho. Chura mbona unawatesa kina baba waliopo ndoani kila siku kugombana na wake zao pindi ukipita barabarani.

Chura acha kututesea dada zetu kutwa kupiga picha wakiinga mwendo wako wa dansi mia mia. Wakivaa viguo vifupi na vimbano vya kushikilia tuta zao mbili ili zidunde kwa staili yako ile pendwa.

Ni nani asiyekupenda chura katika dunia hii. Ni nani asiyetaka kukushika hata sekunde tuu aone ulaini wako utokapo kuoga majini. Ni nani asiyeshtuka upitapo. Kila mmoja hujikuta akilia huku machozi yakitiririka kwa ndani kama underground flow.

Chura imefika hatua sasa uingie kwenye nembo ya taifa. Au tukuweke kwenye moja ya sarafu yetu. Kwa jinsi unavyotupa raha sijaona wakukupinga hapa duniani.

Chura endelea kututawala mpaka tuingie pande za kuzimu.

Chura mtawala mpya katika karne hii.

Wasalamu!!
 
Ilibidi watu wapotoke Sana kwenye suala la uzinzi Ili ule mwisho uje huku malkia wa uzinzi akiendelea kupoteza watu KUPITIA mitandao kwa speed ya ajabu.hakuna namna yanayokatazwa ndo yanayopendwa.waswahili kwao AFRICA bambataa.. UZURI WA NYUMBA NI CHOO
 
Afu ikumbukwe katika Bible study nimejifunza spiritual keys nyingi ambapo chura huwa anamaanisha SUMU..
 
Ilibidi watu wapotoke Sana kwenye suala la uzinzi Ili ule mwisho uje huku malkia wa uzinzi akiendelea kupoteza watu KUPITIA mitandao kwa speed ya ajabu.hakuna namna yanayokatazwa ndo yanayopendwa.waswahili kwao AFRICA bambataa.. UZURI WA NYUMBA NI CHOO

Dunia ili iishe lazima chura atawale dunia. Rejea sodoma na gomora
 
Ajabu ya mimi nikiona kitu kinapapatikiwa sana nakidharau, the same kwa dame mwenye chura


Mkuu chura ndiye mtawala wa dunia. Hata umdharau ndivyo hivyo mkuu. Ukimdharau wewe hata mkeo anampenda
 
Habari hii bila picha ni mboga bila chumvi
LiFrog
images.jpeg
 
Mmmh. Chura tu huyo ndio umejua kumpangilia kiasi hicho duuuh.

Mie nakazia tu hapo kwenye kamstari ka tatu kutoka chini "huyo chura aendelee kuwatawala tu mpaka muingie pande za kuzimu" Teh teh teh


Nasikia huko kuzimu ndio anamamlaka kubwa zaidi
 
chura.jpg

Chura akicheza mchezo wa dansi miamia kwa tabasamu murwaa
 
Eti eeee?

Haya basi zidini kumpa sifa huyo chura.


Hatumpi sifa bali ndio uhalisia Mkuu.
Kama humkubali basi mmeo anamkubali, na kama yeye hamkubali basi watoto wako wanamuimbia na mapambio kabisa. Chura kapata wapi kibali hiki lakini jamani
 
Back
Top Bottom