Kimepelekwa Arusha; kwa sababu Watawala ni Wachaga. Huu ndiyo ukabila wa viongozi wetu. Kwa nini wasifanye Draft ktk Mikoa yote? Kila kitu kinakwenda North ya TZ. Huu ni ubaguzi unaosababishwa na Watawala wetu.
MpendaTz,
..ukiuangalia uamuzi huu kama Mtanzania ofcourse utaenda kujenga Kigoma,Sumbawanga,Rufiji, Nachingwea etc.
..zaidi utakapofanya uamuzi wa kujenga taasisi hiyo ktk maeneo hayo hapo juu utalazimika kujenga na shule za msingi na sekondari zenye hadhi, pamoja na hospitali yenye hadhi. zaidi itabidi uongeze na ujenge na soko kwa ajili ya mahitaji mbalimbali. pia unaweza kulazimika kujenga kiwanja kidogo cha ndege.
..off course hiyo inaweza kuuinua mkoa wa Kigoma. naelewa kuna miji ktk nchi mbalimbali za magharibi imeibuka na kustawi kutokana na kuwa karibu na vyuo vikuu.
..kwa mtizamo wangu ,tatizo ni kwamba uamuzi wa eneo la kujengwa chuo hicho unafanywa na watu wa nje washirika wa Mzee Mandela. sasa je wafadhili hao wako tayari kufanya yote hayo niliyoyabainisha hapo juu? au serikali ina nia ya at least kutoa mchango kufanikisha hilo?
..pia ukumbuke kwamba baada ya ujenzi inabidi uajiri Wakufunzi wa chuo hicho. sasa hapo si kwamba utakuwa unauza jina la chuo tu, mshahara, na research opportunities, bali the whole package kwa mfano wapi watoto wa wakufunzi watakwenda shule, hospitali etc etc.
..kuna maeneo Tanzania yana sifa ya kuwa na nyoka wakali wenye sumu tena hayana hata zahanati za uhakika. sasa unategemea kweli a young and up coming researcher atapenda kuishi huko na familia yake?
NB:
..pia kuna faida gani ya kujenga hicho chuo sehemu kama Kigoma wakati hatuna hata mawazo ya kuimarisha shule za msingi na sekondari?
tehe tehe tehe JF bana......watu wana mawazo mbadala kichizi.......kuna maeneo Tanzania yana sifa ya kuwa na nyoka wakali wenye sumu tena hayana hata zahanati za uhakika. sasa unategemea kweli a young and up coming researcher atapenda kuishi huko na familia yake?
Masanja said:Jokaa Kuu I feel your argument. Lakini tunasahau kitu kimoja, hata US au western Europe miji mingi iliendelea kwa style hii. Ukitaka sehemu iendelee weka opportunities. Kuna watu tumesoma "porini" simply because tulikuwa tunatafuta elimu. Simple.
On the outset lets put record straight. Sisi kama taifa ndo tuna uamuzi wa mwisho Chuo kijengwe wapi. Hakuna cha mfadhili wala nani..ni uamuzi wetu. JK hawezi kusema chuo kijengwe Kigoma..sijui sponsor aseme kwamba Kigoma ni mbali. Mbali na wapi? Kigoma is part of our Republic bwana! Lets think big wajameni! You dont need a PhD to know this! Sema tatizo letu viongozi wetu siyo makini in what they do. they have Parochial interests... Hivi wakuu, mnadhani Kigoma itatoka vipi? juzi tumeona Dodoma wanaweka Chuo kikuu..mbona wengi wanaenda huko? Swala siyo umbali..swala ni opportunities. Period. Ndo maana utakuta Mzungu wa Nevada au Australia anafanya kazi na wakimbizi UN Kasulu au Ngara! Unaweza linganisha Nevada na Ngara au KASULU? No way..swala ni opportunity. Nakuhakikishia leo ukiweka University Kigoma full funded na hao Mandela foundation (kama ndo wanatoa pesa) nakwambia Serikali itachachamaa....hata mafisadi watapeleka watoto wao huko wakaipate elimu...bara bara zitajengwa..hata ndege za akina KQ zitaruka kwenda huko! Swala ni opportunities. Sasa kama hatujazitengeneza..zitakujaje?
As you say a young researcher hawezi kwenda Kigoma..kama hakuna opportunities. Ila kama zipo..kwa nini asiende? Tatizo sisi watanzania especially VIONGOZI wetu ni wavivu wa kufikiria mbele.
Nikupe mfano mmoja, mimi ni kati ya watanzania waliokuwa dissapointed kuona East African Community Headqrtr inajengwa pale Arusha Mjini. Serikali ingekuwa na (sijui niseme akili?) ..makao makuu ya EAC yangejengwa nje ya Arusha kabisa! Tunashindwa kuelewa impact ya mashirika kama haya miaka 20 ijayo. Serikali ingetoa kama hectares 100......kwanza yaani EAC ingepanuka and in the process..inaongeza ajira za watanzania (atleast local staff). Leo unaibananisha pale Arusha mjini..unategemea nini? Hivi sisi tulirogwa na nani?
Kifupi..Mikoa kama Kigoma, Pemba, Lindi nk (peripheral regions)..zitatoka endapo utapeleka opportunities huko! Leo kuna Ruaha University..watu si wanakwenda kusoma huko? kabla ya hapo nani ungewambia aende Ruaha?
Wakuu naomba niwambie tena. Chuo kama hiki kingejengwa Kigoma au Pemba! Kama Mjerumani alitujengea reli miaka hiyo mpaka Kigoma..kwa nini leo sisi tuone Kigoma ni mbali? 100 years baada ya yeye Mjerumani kuondoka? Ukiweka opportunities hizi huko mikoani hata unadumisha umoja wanchi..watu wanaona unawajali..
In all jokaa Kuu your argument has merit lakini..think from the other side of the coin...utagundua kwamba..waafrika akili yetu ni fupi mno. hatujui namna ya kupanga mambo yetu. Hivi kweli unaamini mfadhili anaweza kukuamlisha ujenge chuo wapi kwenye nchi yako? sasa huo uhuru ulipata uhuru gani? duh!
..nani atakwenda Pemba?
..Wapemba wenyewe kina Salim Salim na Maalimu Sefu wamejibanza mjini.
..wacha kijengwe Arusha ni mji wa kimataifa huo.
Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!
Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?
..lakini huoni kwamba hiki chuo kinajengwa Arusha kwasababu miundombinu imeshatangulia pale?
..
Huenda pia kiwanda cha almasi kilijengwa Iringa kwa sababu miundombinu ilishatangulia pale !!..binafsi sikubaliani na utaratibu wa Mwalimu Nyerere kuweka mbele siasa ktk maamuzi ya kiuchumi. utaratibu huo ndiyo uliopelekea kiwanda cha kukata almasi kikajengwa Iringa wakati almasi inapatikana Mwadui.
..
Chuma said:Haya ndio aliyoafanya MRAMBA....wawekezaji Mkuranga...kawapeleka Moshi kuchangia shule.
KAMATI YABAINI UPOTEVU WA MABILIONI MKURANGA said:KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali, imebaini kuwapo kwa upotevu wa mabilioni ya fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, kutokana na kutokuwepo kwa ufuatiliaji wa karibu wa miradi ya maendeleo.
Imebainika kuwa, shughuli za utekelezaji na usimamizi wameachiwa makandarasi pamoja na wadhamini, jambo ambalo limesababisha hasara ya mabilioni katika miradi mbalimbali ya halmashauri hiyo.
Aidha, kamati hiyo imesikitishwa na kutomalizika kwa ujenzi na jengo la hospitali ya wilaya, licha ya Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mama Anna Mkapa, kuchangia mifuko 400 ya saruji ambayo imeharibika huku jengo hilo likiwa hatarini kuwaangukia wagonjwa.
Inadaiwa kuwa, msaada wa Mama Mkapa umekuja kutokana na urafiki wa karibu na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Khanifa Karamagi, hivyo mradi huo wa ujenzi ulikuwa unasimamiwa na mkuu huyo wa wilaya bila kumshirikisha mtu mwingine katika halmashauri ya wilaya hiyo.
Hayo yamebainika baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya siku moja, ili kukagua miradi iliyopo katika halmashauri hiyo na kujionea matumizi ya fedha za serikali zinavyotumika.
Kati ya zaidi ya mifuko hiyo 400 ya saruji iliyotolewa, hakuna hata mmoja uliotumika kwenye ujenzi huo na hata mifuko iliyokutwa kwenye ghala la halmashauri hiyo, mingine ilikosa taarifa kamili.
Na kwa nini kijengwe Pemba na si Kilimatinde? kila kitu Pemba , Pemba mbona wa Pemba mnapenda kulalamika kama wanawake siku zote? Pemba itajengwa na nyinyi wenyewe,
Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!
Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?
Kama alivyosema GT..hiki Chuo ingebidi kijengwe hata Kigoma! Hivi nyinyi mnafikiri kule siyo Tanzania? au watu wanafurahi tuu wakipewa eneo la kutoza ushuru..responsibility inaishia hapo?
Yaani kuna mikoa imetengwa bongo mpaka inasikitisha..