my whole thing ni kwamba, sisi kama taifa masikini inabidi tujenge vyuo kiuchumi. Na unajengaje chuo kiuchumi? Unaangalia where is the most immediate demand in oreder to preserve sustainability.
Wewe unasema si kweli kwamba sehemu inayofaa kujengwa Chuo Kikuu iwe na sekondari nyingi, una disregard hierarchy ya decentralization.Kwamba unataka kujenga Chuo Kikuu, kwa mfano, mfano tu,Kibondo huko, kwenye shule za sekondari 4 na kati ya hizo zenye A Level mbili, wakati demand iko Kilimanjaro, Mbeya na Dar kwenye maelfu ya shule za sekondari, hatima yake itabidi watu wa Kilimanjaro, Dar na Mbeya watoke makwao huko kuingia katika ma treni, mabasi na mitumbwi kuja Kibondo kusoma.
Hizi infrastructure zetu zinavyotengenezwa inabidi tuwe makini sana kwa sababu kuna ma hidden costs kibao humu.Wenzetu wanapigia hesabucost ya traffic jams kwenye uchumi, kwamba Wamarekani kwa mwaka mmoja wanatumia so much billion manhour kwenye traffic jams, na hiyo inakuwa sawa na dollar billion ngapi katika uzalishaji.Sisi tunaona muda hauna thamani wakati ni moja kati ya vitu ambavyo huwezi kuvirudisha.
Kwa hiyo ninachosema ni kwamba, kabla hatujajenga Chuo Kikuu Pemba na Kigoma (by the way kujenga na decentralization ni lazima na haki ya wananchi wa huko) nataka kuona kwambakuna local demand kwanza, nataka kuona kuna shule za sekondari zenye A-Level za kutosha zitakazoweza kutoa wananfunzi wa kwenda kwenye hivi vyuo, sitaki kuona mwanafunzi anatoka Ruvuma analazimika kwenda kusoma Pemba au Kigoma eti kwa sababu tu ndiko chuo kiliko.Hizi ni characteristics za command economy inayofanya mambo kibabebabe tu bila kujali forces za market.Ikiwa mtu ataamua kwenda kusoma sehemu nyingine ya Tanzania -pengine kwa utashi wa kutaka kuijua nchi yake vizuri not unlike Chelsea Clinton alivyoamua kwenda Stanford kusoma undergraduate degree wakati wazazi wake wako DC na kwa baba yake ni Arkansas- that is fine, as long as huu ni utashi wa mtu binafsi tu mwenye uwezo huo na si kwa sababu hamna shule za karibu.
My point has to do with the whole point of gradual decentralization.Fine, tutajenga vyuo Pemba na Kigoma tukijaaliwa, lakini tujenge sensible demand basi, tujenge sekondari basi.Sio tunajenga our version of a bridge to nowhere.