Chuo kipya cha NELSON MANDELA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo kipya cha NELSON MANDELA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Aug 23, 2009.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!

  Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?
   
 2. Kakati

  Kakati Senior Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Chuo gani?
  Kinajengwa na nani?
  Kwa fedha ya nani?
  Kwa ajili ya masomo gani na nani watasoma?
  Anayeamua kijengwe wapi ni nani?
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,755
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  ..nani atakwenda Pemba?

  ..Wapemba wenyewe kina Salim Salim na Maalimu Sefu wamejibanza mjini.

  ..wacha kijengwe Arusha ni mji wa kimataifa huo.
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ni moja kati ya vyo vya Engineering vi3 vitakavyojengwa Africa.
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  duh! mbona mapema namna hiyo?

  5


  4

  3

  2

  1
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,755
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  ..ndiyo!!

  ..si wana mafuta hao.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  duuh!


  1...
   
 8. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  GT, asante kwa taarifa.

  Nisaidie, sijaelewa, kwa nini kisijengwe ARUSHA for that matter?
   
 9. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Na kwa nini kijengwe Pemba na si Kilimatinde? kila kitu Pemba , Pemba mbona wa Pemba mnapenda kulalamika kama wanawake siku zote? Pemba itajengwa na nyinyi wenyewe,
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kwa kuwa mnabishania hata mahali pa kujengwa, mi naona afadhali kisijengwe kabisa tanzania, kihamimishiwe msumbiji
   
 11. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mpitanjia,,

  \sasa wewe Msumbwa mbona unatoa kali ya mwaka
   
 12. H

  Haki JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimepelekwa Arusha; kwa sababu Watawala ni Wachaga. Huu ndiyo ukabila wa viongozi wetu. Kwa nini wasifanye Draft ktk Mikoa yote? Kila kitu kinakwenda North ya TZ. Huu ni ubaguzi unaosababishwa na Watawala wetu.
   
 13. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280  Kama alivyosema GT..hiki Chuo ingebidi kijengwe hata Kigoma! Hivi nyinyi mnafikiri kule siyo Tanzania? au watu wanafurahi tuu wakipewa eneo la kutoza ushuru..responsibility inaishia hapo?

  Yaani kuna mikoa imetengwa bongo mpaka inasikitisha..
   
 14. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160

  Ingelifaa sana kingejengwa Kigoma. Tena along the beatiful Lake Tanganyika. Nilikuwa Bulombora JKT, that is naturally a beautiful place!!!
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,755
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  ..jamani hiki ni chuo kikuu cha Afrika cha kimataifa.

  ..kingekuwa kinajengwa na serikali ya Tanzania basi tungekuwa na uwezo wa kuulizana kwanini hakijengwi Kigoma,Sumbawanga,Rufiji,Mafia etc.

  ..binafsi nadhani kilichozingatiwa hapo ni kuangalia eneo lenye miundombinu ya ku-support chuo kikuu. Arusha tayari miundombinu ya namna hiyo ipo mfano uwanja ndege, mawasiliano ya uhakika, mji wenye hadhi etc etc.

  ..sehemu kama Kigoma hata Watanzania wenyewe tunapakimbia. kuna maeneo kama Rufiji ambayo mtumishi wa serikali akihamishiwa anaamua kuacha kazi kabisa.

  ..sasa hawa wasomi/wahadhiri wa kimataifa ambao watafanya kazi kwenye chuo cha Mandela tuna uhakika kweli watavumilia kukaa eneo kama Kigoma, au Rufiji, au Mafia, au Sumbawanga, au Pemba?

  ..mngependekeza chuo kijengwa Mwanza kidogo ningewaelewa.

  Masanja,

  ..nakubaliana na wewe kwamba kuna maeneo serikali imeyatelekeza.

  ..cha kusikitisha zaidi hata wananchi wa maeneo hayo nao kama wameunga tela la serikali ktk kuyatelekeza maeneo walikuzaliwa na kukulia.

  ..iliwahi kuletwa hoja hapa ikizungumzia utendaji wa Zitto Kabwe jimboni kwake.

  ..wana jamii forums wengi waliizima hoja hiyo wakisema Zitto halazimiki kuweka juhudi zozote zile kuchochea maendeleo ya Kigoma.

  ..sasa kama Zitto hana uchungu wowote na Kigoma mnategemea JK, Pinda, Masanja,jokaKuu etc ndiyo wawe na uchungu na Kigoma?

  ..hebu fikiria mkoa wa Kagera pamoja na kuonekana "nshomile sana" waliitana na kuchangishana 1.5 bilion kwa ajili ya elimu.

  ..umesikia wabunge toka Kigoma waki-organise mkutano wowote ule kuchangisha kwa ajili ya maendeleo ya Kigoma? na mikutano ya namna hiyo siyo lazima uite wana Kigoma peke yake.
   
 16. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kukijenga chuo kule ndiyo ingelikuwa kichocheo cha serikali kuweka infrastructure stahili taratibu kwani ndivyo mikoa yote mikubwa ilivyoanza. Nyerere ndivyo alivyokuwa anashauri mara kwa mara, nakumbuka Mbeya cement ilikuwa kidogo isijengwe kule, kama sikosei ilikuwa phase two ya Tanga Cement
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,755
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  MpendaTz,

  ..i see your point.

  ..lakini huoni kwamba hiki chuo kinajengwa Arusha kwasababu miundombinu imeshatangulia pale?

  ..binafsi naamini tayari vipo vichocheo vingi tu vya kupeleka miundombinu Kigoma. kichocheo namba moja ni zao la michikichi, kichochoe kingine ni ziwa Tanganyika na mazao yake, hifadhi ya Sokwe ya Gombe, pamoja na soko/biashara na Jamhuri ya Congo.

  ..kama Watanzania wenyewe hatutaiinua na kuijenga Kigoma,Sumbawanga,Rufiji,Mafia,Kilwa, tusitegemee watu wa nje kama Mandela kuja kutufanyia kazi hiyo.

  ..binafsi sikubaliani na utaratibu wa Mwalimu Nyerere kuweka mbele siasa ktk maamuzi ya kiuchumi. utaratibu huo ndiyo uliopelekea kiwanda cha kukata almasi kikajengwa Iringa wakati almasi inapatikana Mwadui.

  ..
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Ni pale ilipokuwa Arusha Tech? Maana hata mbeya tech kimekuwa chuo kikuu. Na nia ni kuendeleza pale walipokuwa.Kwangu mimini habari njema
   
 19. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  JokaK,
  Pia nakubaliana sana kuwa ni wajibu wetu kwa kweli kuhakikisha tunaijenga nchi yetu wenyewe na tunajiandaa ili hata akitokea wa kuongeza tone la maendeleo awe amevutiwa na juhudi zetu.

  lakini kama kile chuo kinajengwa kwa ajili ya Waafrika wote na dunia na kwa heshima ya Mzee Mandela basi ingebidi kiwe cha kiaina siyo tu kufuata miundo mbinu. Kusema kweli kama Nyerere asingefanya mambo pia kisiasa nchi yetu ingekuwa imegawanyika vibaya. Kiuchumi tulirudi nyuma lakini bila hivyo leo tungekuwa kama jirani zetu. Wewe angalia tu joto la udini na ukabila lililokumba Bunge miaka ya karibuni utaona kuwa nchi hata siku moja haiwezi kushinda katika kila jambo. Lakini kuna kitu kama ukomavu wa kisiasa ambao unatusaidia Tz. Yale mauaji ya jirani zetu yalikuwa very ugly, maana matajiri pale mji mkuu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, masikini ndiyo waliokuwa wanauana wenyewe kwa wenyewe.
   
 20. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hivi uamuzi wa Chuo kujengwa Ar. aliutoa nani??

  Joka kuu ni kweli miundombinu in the nothern circut ni mizuri ndo maana kuna vyuo vingi vya serikali kama Polisi, Wanyama Pori, TMA n.k

  Mimi nilidhani kihstoria kwa vile Wakimbizi wengi wa SA waliishi Morogoro basi Chuo kikuu cha Mandela kingejegwa Morogoro kwa vile hata miundombinu ni safi!

  Over Pemba au Tunduru..sasa kama hata watu wanaotoka huko hawataki kundeleza huko..je serikali ndo itaendleza huko??

  Huwa na campus Pemba may be..kama UDSM walivyo na kampasi ya mambo ya Uvuvi kule Unguja! Sema taabu ya Pemba ni umeme sasa utajenga Chuo cha teknologia sehemu ambapo hakuna umeme??
   
Loading...