Chuo kipya cha NELSON MANDELA

MpendaTz,

..ukiuangalia uamuzi huu kama Mtanzania ofcourse utaenda kujenga Kigoma,Sumbawanga,Rufiji, Nachingwea etc.

..zaidi utakapofanya uamuzi wa kujenga taasisi hiyo ktk maeneo hayo hapo juu utalazimika kujenga na shule za msingi na sekondari zenye hadhi, pamoja na hospitali yenye hadhi. zaidi itabidi uongeze na ujenge na soko kwa ajili ya mahitaji mbalimbali. pia unaweza kulazimika kujenga kiwanja kidogo cha ndege.

..off course hiyo inaweza kuuinua mkoa wa Kigoma. naelewa kuna miji ktk nchi mbalimbali za magharibi imeibuka na kustawi kutokana na kuwa karibu na vyuo vikuu.

..kwa mtizamo wangu ,tatizo ni kwamba uamuzi wa eneo la kujengwa chuo hicho unafanywa na watu wa nje washirika wa Mzee Mandela. sasa je wafadhili hao wako tayari kufanya yote hayo niliyoyabainisha hapo juu? au serikali ina nia ya at least kutoa mchango kufanikisha hilo?

..pia ukumbuke kwamba baada ya ujenzi inabidi uajiri Wakufunzi wa chuo hicho. sasa hapo si kwamba utakuwa unauza jina la chuo tu, mshahara, na research opportunities, bali the whole package kwa mfano wapi watoto wa wakufunzi watakwenda shule, hospitali etc etc.

..kuna maeneo Tanzania yana sifa ya kuwa na nyoka wakali wenye sumu tena hayana hata zahanati za uhakika. sasa unategemea kweli a young and up coming researcher atapenda kuishi huko na familia yake?

NB:

..pia kuna faida gani ya kujenga hicho chuo sehemu kama Kigoma wakati hatuna hata mawazo ya kuimarisha shule za msingi na sekondari?
 
Kimepelekwa Arusha; kwa sababu Watawala ni Wachaga. Huu ndiyo ukabila wa viongozi wetu. Kwa nini wasifanye Draft ktk Mikoa yote? Kila kitu kinakwenda North ya TZ. Huu ni ubaguzi unaosababishwa na Watawala wetu.

Mbolea kabisa....!!
 
Mimi ningependelea kijengwe Mwanza ila hata Arusha ni sawa tu ili mradi kinajengwa Tanzania na wazalendo wataweza kumudu gharama za kusoma hapo.
 
MpendaTz,

..ukiuangalia uamuzi huu kama Mtanzania ofcourse utaenda kujenga Kigoma,Sumbawanga,Rufiji, Nachingwea etc.

..zaidi utakapofanya uamuzi wa kujenga taasisi hiyo ktk maeneo hayo hapo juu utalazimika kujenga na shule za msingi na sekondari zenye hadhi, pamoja na hospitali yenye hadhi. zaidi itabidi uongeze na ujenge na soko kwa ajili ya mahitaji mbalimbali. pia unaweza kulazimika kujenga kiwanja kidogo cha ndege.

..off course hiyo inaweza kuuinua mkoa wa Kigoma. naelewa kuna miji ktk nchi mbalimbali za magharibi imeibuka na kustawi kutokana na kuwa karibu na vyuo vikuu.

..kwa mtizamo wangu ,tatizo ni kwamba uamuzi wa eneo la kujengwa chuo hicho unafanywa na watu wa nje washirika wa Mzee Mandela. sasa je wafadhili hao wako tayari kufanya yote hayo niliyoyabainisha hapo juu? au serikali ina nia ya at least kutoa mchango kufanikisha hilo?

..pia ukumbuke kwamba baada ya ujenzi inabidi uajiri Wakufunzi wa chuo hicho. sasa hapo si kwamba utakuwa unauza jina la chuo tu, mshahara, na research opportunities, bali the whole package kwa mfano wapi watoto wa wakufunzi watakwenda shule, hospitali etc etc.

..kuna maeneo Tanzania yana sifa ya kuwa na nyoka wakali wenye sumu tena hayana hata zahanati za uhakika. sasa unategemea kweli a young and up coming researcher atapenda kuishi huko na familia yake?

NB:

..pia kuna faida gani ya kujenga hicho chuo sehemu kama Kigoma wakati hatuna hata mawazo ya kuimarisha shule za msingi na sekondari?

Hizo ndizo challlenges za maendeleo ambazo viongozi shupavu huzifanyia kazi. Ni kweli tena naunga mkono sana wazo kuwa ni lazima na sisi tuahidi kuwa katika kipindi cha miaka mitatu mitano ijayo tutakuwa tumechangia nini katika kuweka miundombinu inayostahili. Na kuahidi kuwa itakuwa kamili katika kipindi cha miaka kumi hivi. Tukishajipanga sawasawa utaona tunapata na washabiki hata majirani wenye nia ya kuendeleza Heshima ya Mzee wa Kiafrika Mandela.
JKuu katika vitu muhmu katika nchi kugawa vizuri hakuna kama elimu, hii ndiyo maana unaona leo hii tunashindwa kuing'oa ccm madarakani. Kwa sababu wanatumia udhaifu wa sehemu nyingi kuwalaghai wananchi na kununua kura zao, kuwadanganya watafanyiwa hiki na kile wanakubali. Angalia fedha zilizoitwa za kugawia watu kuwawezesha leo zinagawiwa mijini tu! Mabenki yameshindwa wanaambiwa wazirudishe.
Kuna Nchi ziliwekeza kwa wananchi wao kielimu kama Korea Kusini miaka ishirini na tano tu iliyopita tulikuwa karibu sawa leo hii wanauchumi ulio imara sana. Vingine vyote vifuate ushauri kiuchumi lakini ili nchi iendelee elimu inatakiwa isambazwe sawia!
 
..kuna maeneo Tanzania yana sifa ya kuwa na nyoka wakali wenye sumu tena hayana hata zahanati za uhakika. sasa unategemea kweli a young and up coming researcher atapenda kuishi huko na familia yake?
tehe tehe tehe JF bana......watu wana mawazo mbadala kichizi.....
 
Jokaa Kuu I feel your argument. Lakini tunasahau kitu kimoja, hata US au western Europe miji mingi iliendelea kwa style hii. Ukitaka sehemu iendelee weka opportunities. Kuna watu tumesoma "porini" simply because tulikuwa tunatafuta elimu. Simple.

On the outset lets put record straight. Sisi kama taifa ndo tuna uamuzi wa mwisho Chuo kijengwe wapi. Hakuna cha mfadhili wala nani..ni uamuzi wetu. JK hawezi kusema chuo kijengwe Kigoma..sijui sponsor aseme kwamba Kigoma ni mbali. Mbali na wapi? Kigoma is part of our Republic bwana! Lets think big wajameni! You dont need a PhD to know this! Sema tatizo letu viongozi wetu siyo makini in what they do. they have Parochial interests... Hivi wakuu, mnadhani Kigoma itatoka vipi? juzi tumeona Dodoma wanaweka Chuo kikuu..mbona wengi wanaenda huko? Swala siyo umbali..swala ni opportunities. Period. Ndo maana utakuta Mzungu wa Nevada au Australia anafanya kazi na wakimbizi UN Kasulu au Ngara! Unaweza linganisha Nevada na Ngara au KASULU? No way..swala ni opportunity. Nakuhakikishia leo ukiweka University Kigoma full funded na hao Mandela foundation (kama ndo wanatoa pesa) nakwambia Serikali itachachamaa....hata mafisadi watapeleka watoto wao huko wakaipate elimu...bara bara zitajengwa..hata ndege za akina KQ zitaruka kwenda huko! Swala ni opportunities. Sasa kama hatujazitengeneza..zitakujaje?

As you say a young researcher hawezi kwenda Kigoma..kama hakuna opportunities. Ila kama zipo..kwa nini asiende? Tatizo sisi watanzania especially VIONGOZI wetu ni wavivu wa kufikiria mbele.

Nikupe mfano mmoja, mimi ni kati ya watanzania waliokuwa dissapointed kuona East African Community Headqrtr inajengwa pale Arusha Mjini. Serikali ingekuwa na (sijui niseme akili?) ..makao makuu ya EAC yangejengwa nje ya Arusha kabisa! Tunashindwa kuelewa impact ya mashirika kama haya miaka 20 ijayo. Serikali ingetoa kama hectares 100......kwanza yaani EAC ingepanuka and in the process..inaongeza ajira za watanzania (atleast local staff). Leo unaibananisha pale Arusha mjini..unategemea nini? Hivi sisi tulirogwa na nani?

Kifupi..Mikoa kama Kigoma, Pemba, Lindi nk (peripheral regions)..zitatoka endapo utapeleka opportunities huko! Leo kuna Ruaha University..watu si wanakwenda kusoma huko? kabla ya hapo nani ungewambia aende Ruaha?

Wakuu naomba niwambie tena. Chuo kama hiki kingejengwa Kigoma au Pemba! Kama Mjerumani alitujengea reli miaka hiyo mpaka Kigoma..kwa nini leo sisi tuone Kigoma ni mbali? 100 years baada ya yeye Mjerumani kuondoka? Ukiweka opportunities hizi huko mikoani hata unadumisha umoja wanchi..watu wanaona unawajali..

In all jokaa Kuu your argument has merit lakini..think from the other side of the coin...utagundua kwamba..waafrika akili yetu ni fupi mno. hatujui namna ya kupanga mambo yetu. Hivi kweli unaamini mfadhili anaweza kukuamlisha ujenge chuo wapi kwenye nchi yako? sasa huo uhuru ulipata uhuru gani? duh!
 
Mimi naona ARUSHA ni sehemu nzuri ya vyuo. Hata Agha Khan watajenga chuo Arusha. Arusha wanabahati ya kuwa na mashamba makubwa ambayo yako karibu na barabara. Hii inafanya iwe rahisi kujenga Vyuo na hotel kubwa. Hata kwa viwanda Arusha bado ni sehemu nzuri lakini hawana bandari na ndiyo maana wanaenda Tanga. Wanzanzibar hawataki wabara wawekeze Zanzibar na wanataka tuwe na vitambulisho na ubaguzi unachangia sana kuvutia vitu kama hivi. Arusha ni ya kila mtu anayetaka kuwekeza.
 
Masanja said:
Jokaa Kuu I feel your argument. Lakini tunasahau kitu kimoja, hata US au western Europe miji mingi iliendelea kwa style hii. Ukitaka sehemu iendelee weka opportunities. Kuna watu tumesoma "porini" simply because tulikuwa tunatafuta elimu. Simple.

On the outset lets put record straight. Sisi kama taifa ndo tuna uamuzi wa mwisho Chuo kijengwe wapi. Hakuna cha mfadhili wala nani..ni uamuzi wetu. JK hawezi kusema chuo kijengwe Kigoma..sijui sponsor aseme kwamba Kigoma ni mbali. Mbali na wapi? Kigoma is part of our Republic bwana! Lets think big wajameni! You dont need a PhD to know this! Sema tatizo letu viongozi wetu siyo makini in what they do. they have Parochial interests... Hivi wakuu, mnadhani Kigoma itatoka vipi? juzi tumeona Dodoma wanaweka Chuo kikuu..mbona wengi wanaenda huko? Swala siyo umbali..swala ni opportunities. Period. Ndo maana utakuta Mzungu wa Nevada au Australia anafanya kazi na wakimbizi UN Kasulu au Ngara! Unaweza linganisha Nevada na Ngara au KASULU? No way..swala ni opportunity. Nakuhakikishia leo ukiweka University Kigoma full funded na hao Mandela foundation (kama ndo wanatoa pesa) nakwambia Serikali itachachamaa....hata mafisadi watapeleka watoto wao huko wakaipate elimu...bara bara zitajengwa..hata ndege za akina KQ zitaruka kwenda huko! Swala ni opportunities. Sasa kama hatujazitengeneza..zitakujaje?

As you say a young researcher hawezi kwenda Kigoma..kama hakuna opportunities. Ila kama zipo..kwa nini asiende? Tatizo sisi watanzania especially VIONGOZI wetu ni wavivu wa kufikiria mbele.

Nikupe mfano mmoja, mimi ni kati ya watanzania waliokuwa dissapointed kuona East African Community Headqrtr inajengwa pale Arusha Mjini. Serikali ingekuwa na (sijui niseme akili?) ..makao makuu ya EAC yangejengwa nje ya Arusha kabisa! Tunashindwa kuelewa impact ya mashirika kama haya miaka 20 ijayo. Serikali ingetoa kama hectares 100......kwanza yaani EAC ingepanuka and in the process..inaongeza ajira za watanzania (atleast local staff). Leo unaibananisha pale Arusha mjini..unategemea nini? Hivi sisi tulirogwa na nani?

Kifupi..Mikoa kama Kigoma, Pemba, Lindi nk (peripheral regions)..zitatoka endapo utapeleka opportunities huko! Leo kuna Ruaha University..watu si wanakwenda kusoma huko? kabla ya hapo nani ungewambia aende Ruaha?

Wakuu naomba niwambie tena. Chuo kama hiki kingejengwa Kigoma au Pemba! Kama Mjerumani alitujengea reli miaka hiyo mpaka Kigoma..kwa nini leo sisi tuone Kigoma ni mbali? 100 years baada ya yeye Mjerumani kuondoka? Ukiweka opportunities hizi huko mikoani hata unadumisha umoja wanchi..watu wanaona unawajali..

In all jokaa Kuu your argument has merit lakini..think from the other side of the coin...utagundua kwamba..waafrika akili yetu ni fupi mno. hatujui namna ya kupanga mambo yetu. Hivi kweli unaamini mfadhili anaweza kukuamlisha ujenge chuo wapi kwenye nchi yako? sasa huo uhuru ulipata uhuru gani? duh!

Masanja,

..hebu chukulia Mandela Foundation wanakuja Tanzania, halafu meya wa Arusha, na meya wa Kigoma, wanapewa nafasi kufanya presentation ya mradi wa chuo kikuu uende mji upi.

..you know what is going to happen.

..nimeisoma posting yako nakubaliana na wewe kwamba itapendeza zaidi kama chuo hiki au taasisi nyingine kama hizo zitapelekwa ktk yale maeneo "yamesahauliwa."

..sasa tukiupanua zaidi mjadala huu, je tutakuwa tunafungua Kigoma/Lindi/Songea kwa Watanzania wengine, au wana Kigoma/Lindi/Songea.. nao watapata nafasi ya kufaidika na ujio wa taasisi kama hiyo?

..ninauliza swali hilo kwasababu mimi pia nimesoma "porini", lakini tatizo ni kwamba hakukuwa na mwanafunzi hata mmoja mzaliwa wa maeneo[read wilaya,mkoa] ya karibu na shule yangu.

..pamoja na kuwa na imbalance ktk allocation ya institutions kama vyuo, hospitali, etc pia kuna disparity kubwa sana ktk quality ya elimu baina ya maeneo mbalimbali ya Tanzania. hilo kwangu nadhani ni tatizo kubwa na a time ticking bomb.
 
..nani atakwenda Pemba?

..Wapemba wenyewe kina Salim Salim na Maalimu Sefu wamejibanza mjini.

..wacha kijengwe Arusha ni mji wa kimataifa huo.

Walio na shida ya kusoma watakwenda huko Pemba kama kitakuwa kimejengwa huko. Lakini sioni reason ya kuunganisha uwepo wa Pemba na makimbilio au makazi ya Salim na Seif Hamad.

Kuna watu wanahitaji elimu na hii itasaidia kuleta maendeleo kokote watakapokuwa wameamua kujenga, aidha Pemba, Kigoma. Newala n.k
 
Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!

Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?

Mbona hili ni jambo la siku nyingi sana; uamuzi wa kukijenga Arusha ulipita tangu mwaka 2007 kama sikosei.
 
..lakini huoni kwamba hiki chuo kinajengwa Arusha kwasababu miundombinu imeshatangulia pale?
..
..binafsi sikubaliani na utaratibu wa Mwalimu Nyerere kuweka mbele siasa ktk maamuzi ya kiuchumi. utaratibu huo ndiyo uliopelekea kiwanda cha kukata almasi kikajengwa Iringa wakati almasi inapatikana Mwadui.
..
Huenda pia kiwanda cha almasi kilijengwa Iringa kwa sababu miundombinu ilishatangulia pale !!
 
Kama uamuzi ungefanyika kisiasa basi kingejengwa Morogoro. Kama ungefanyika Kiswahili basi kingejengwa Pemba, Sumbawanga au Kigoma. Nadhani uamuzi ulifanyika kitaaluma ndio maana ikaonekana kijengwe Arusha.

Kama aliivyodokeza mmoja, ni kampasi zinajengwa katika kanda mbalimbali za Afrika. Ya Arusha kitakuwa kwa ajili ya Mashariki mwa Afrika. Sasa kama hivyo ndivyo, kinachoangaliwa ni mahali panapofaa kwa watu wa eneo lote, na sio kuangalia siasa za Kiswahili za nchi moja tu.

Arusha panafikika kwa basi na mashangingi binafsi toka sehemu yoyote ya Afrika Mashariki. Pemba na Kigoma ni pa shida, kiusafiri. Wale wanaoogopa usafiri wa mashua watafikaje Pemba?

Na akiugua mwanafunzi wa kimataifa Kigoma utampeleka kwa waganga wa kienyeji au utafanyaje? Maana hakuna hospitali ya kweli pale! Pemba hivyo hivyo. Arusha kuna hospitali nzuri za misheni, na hospitali za serikali zipo vile vile. Kusema ujenge chuo Kigoma ili nao wajengewe hospitali ni kuwatakia mabaya hao wanafunzi. Zinatangulia huduma, sio wanafunzi.

Kigoma na Pemba wanaweza kujenga elimu, lakini itabidi kuanza chini. Ni lazima kuanza kwa kuwa na shule nzuri za msingi na za sekondari. Na kwa hilo mnakosea kuisubiri mno serikali. Nawaomba wananchi wa Kigoma washirikiane na viongozi wao wa kidini wajenge shule moja ya bweni ya wasichana inayofanana na St. Joseph ya Mbeya, Mariam ya Bagamoyo au St. Gorett ya Moshi.
 
Chuo kujengwa Arusha sioni tatizo maana walioamua sio Watanzania peke yao bali ni watu wa nje. Kwa watu wa nje nadhani walikuwa wana-consider nchi nyingi na hatimaye kuchagua Arusha. Arusha ni mji unaojulikana sana duniani, hata Rais wa zamani wa Marekani alipaita 'Geneva of Africa'. Pia ni mji unao ongoza kwa utalii hapa nchini. Vilevile imekuwa kituo cha Mahakama ya Kimataifa. Arusha pia ina sifa ya kuwa na hali ya hewa nzuri yaani 'cool' inayovutia watu wengi. Pia inafikika kirahisi kwa ndege kwa kuwepo uwanja wa KIA karibu na pia kiwanja cha ndege (kidogo) pale pale Arusha. Naunga mkono Arusha kuwa host wa chuo hicho. Vyuo vingine vipya vinaweza kufikiriwa maeneo/miji mingine lakini lazima tuelewe uchaguzi wa mahala pa kuweka chuo huangalia vigezo kadhaa ili kuhakikisha uendeshaji wa chuo utakuwa 'sustainable'.
 
Mie sioni sababu ya Msingi ya kujengwa Arusha. na watetezi wa Arusha historia yafahamika hapa JF..."siwezi shangaa..."

Haya ndio aliyoafanya MRAMBA....wawekezaji Mkuranga...kawapeleka Moshi kuchangia shule...so walochukua maamuzi haya ni wale wale...!!!

Ukiangalia namna Maprofesa/wafanyakazi wa Mzumbe walivyojenga maeneo karibu na Mzumbe utakiri uwepo wa Chuo Kikuuu sehemu na Athari zake miaka ya Mbele...Chuo ni moja ya chachu ambayo ingeweza kuleta vyote vya maendeleo. Kuchanganyika na watu ndio kunakoleta Maendeleo eneo husika...!!!

Kama Chuo "Kinge" au "Kita" jengwa Kigoma...basi Maendeleo mengi yangewezaibuka....

Hivi Kigoma na Arusha ipi ambayo inaweza fikika na nchi za Kanda ya Ziwa?..Sehemu zote ambazo infrastructure mbovu zina viwanja vya Ndege hata kama sio vya Kimataifa lkn local planes zinafika...!!!

Kusema eti Wa-Kigoma waanze kutokea chini ni kufilisika kimawazo...!!!

Msisingizie eti Walimu....mara ohh Maresearcher....watakataa kwenda Huko..nani kakwambia?.....hao Wazungu tunao"waamini" still wapo interior ya Tanzania ambapo hakuna Umeme wala Maji..wala usafiri wa Uhakika...atlast wengine wanajikuta wanaolewa/kuzaa na wabongo...

Hao watu wa NJE hawawezi kuamua kwa niaba yetu ni Ubwege tu wa Viongozi wetu...
 
Chuma said:
Haya ndio aliyoafanya MRAMBA....wawekezaji Mkuranga...kawapeleka Moshi kuchangia shule.

Chuma,

..hivi ni nani alikwambia mwekezaji kwenye mradi Mkuranga hawezi kuchangia shule Rombo? sheria gani ya Jamhuri imevunjwa hapo?

..yule Mbunge wenu Mkuranga alikuwa amesinzia kazini. alikuwa akitumiwa na Yusuf Manji kumshambulia Reginald Mengi bungeni, badala ya kushughulikia kero za wananchi wa Mkuranga.

..sasa tukuulize: Yusuf Manji amechangia kiasi gani huko Mkuranga?
 
KAMATI YABAINI UPOTEVU WA MABILIONI MKURANGA said:
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali, imebaini kuwapo kwa upotevu wa mabilioni ya fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, kutokana na kutokuwepo kwa ufuatiliaji wa karibu wa miradi ya maendeleo.
Imebainika kuwa, shughuli za utekelezaji na usimamizi wameachiwa makandarasi pamoja na wadhamini, jambo ambalo limesababisha hasara ya mabilioni katika miradi mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Aidha, kamati hiyo imesikitishwa na kutomalizika kwa ujenzi na jengo la hospitali ya wilaya, licha ya Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mama Anna Mkapa, kuchangia mifuko 400 ya saruji ambayo imeharibika huku jengo hilo likiwa hatarini kuwaangukia wagonjwa.
Inadaiwa kuwa, msaada wa Mama Mkapa umekuja kutokana na urafiki wa karibu na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Khanifa Karamagi, hivyo mradi huo wa ujenzi ulikuwa unasimamiwa na mkuu huyo wa wilaya bila kumshirikisha mtu mwingine katika halmashauri ya wilaya hiyo.
Hayo yamebainika baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya siku moja, ili kukagua miradi iliyopo katika halmashauri hiyo na kujionea matumizi ya fedha za serikali zinavyotumika.
Kati ya zaidi ya mifuko hiyo 400 ya saruji iliyotolewa, hakuna hata mmoja uliotumika kwenye ujenzi huo na hata mifuko iliyokutwa kwenye ghala la halmashauri hiyo, mingine ilikosa taarifa kamili.

Chuma,

..wakati unamlaumu Mramba kwa kuwapokonya mwekezaji, Mkuranga mmeshindwa kutumia msaada wa Mama Anna Mkapa.
 
Na kwa nini kijengwe Pemba na si Kilimatinde? kila kitu Pemba , Pemba mbona wa Pemba mnapenda kulalamika kama wanawake siku zote? Pemba itajengwa na nyinyi wenyewe,

Reference to women is not forbiden,but it should not be in this regard! Umesoma kweli wewe? huna hata chembe ya gender knowledge kiasi hicho? Jadili mada don't cross the line.
 
Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!

Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?

Hahaha, unaweza kufikiri kirahisi hivi hasa kama unaweka siasa ndani yake!

1. Zanzibar hakuna ardhi. Si unajua hata Watanganyika hawaruhusiwi kuja kumiliki ardhi huku kwetu zenji!

2. lakini pia, Zanzibar ni ya Wazanzibar ila Tanzania ni ya Watanzania

3. Kigoma hakuna barabara wala uwanja wa ndege. Si unajua serikali inafanya kazi zake kwa vipaumbele? kipaumbele cha usafiri kwa mkoa wa kigoma hakijafikiwa (hata mwenyekiti wa ccm-mkoa alisema hili!).
 
Hivi mwafahamu wanatutawala ni WAKUU na sio Viongozi....Wanaweza jenga hata Dar pembeni ya Mlimani.
 
Kama alivyosema GT..hiki Chuo ingebidi kijengwe hata Kigoma! Hivi nyinyi mnafikiri kule siyo Tanzania? au watu wanafurahi tuu wakipewa eneo la kutoza ushuru..responsibility inaishia hapo?

Yaani kuna mikoa imetengwa bongo mpaka inasikitisha..

One of the major functions of the cities is Education. Many big colleges are located in the cities. Together with agglomeration of economies if a university is located in a city it meets the needs of both students and staff very well: prominent professors will go there, good students will flock into it from both within and outside the country etc. Leave away politics if you really want to put up a good university. Why don't you ask for the decision makers to put up the university in Mtwara/Lindi/Songea? It does not mean that these places are ignored,rather development process is gradual. Develop the infrastructure first then put up colleges/universities otherwise we are just wasting time locating a university at a place where the infrastructure is so poor! Are we serious when we say we should build this university in Dodoma with the present infrastructure? I suggest this university to be built in DSM and it will be superb: many lecturers will flow in to teach,students' enrolment will surpass all other universities in the country. Put it in Dar and not Arusha to bring real competition to the UDSM.
 
Back
Top Bottom