Chuo kikuu Mbeya chaunda kifaa kukabili ajali za majini

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,620
4,265
Chuo kikuu cha Mbeya University of Science And Technology (MUST) ambacho Zamani ilikuwa Mbeya technical college (MTC), badaye Mbeya Institute of Science and Technology (MIST) na sasa kimepewa hadhi ya UNIVERSITY. Kimeunda kifaa maalum cha kukabiliana na ajali za majini. Kifaa hiki kinatoa taarifa za kiasi cha mzigo, hali ya mawimbi n.K kutoka ktk eneo la meli husika kwenda kwa manahodha na mamlaka za udhibiji (SUMATRA) N.K.
mmoja wa wagunduzi hao ameiomba serikali kukubali kifaa hicho ili kianze kazi mapema.

Source: STAR TV, habari ya saa 10.00 am.
 
Hongereni vijana na wanasayansi wetu.Acheni na kelele za siasa zinazo zungumzwa saidieni taifa lenu kwa hali na mali.Nyie ni wanasayansi na sio wanasiasa.Hakikisheni mnakipa jina kwa harufi zenu za mwaqnzo za majina yenu wotemlioshiriki kwa ugunduzi huo.
Wenu katika ujenzi wa taifa
LWLNLW
 
Ni lini wamekippa hadhi ya university hiki chuo? Mbona nafasi za kazi tutorial sijazisikia?au washawekana ndugu kwenye vitengo?
 
Ni lini wamekippa hadhi ya university hiki chuo? Mbona nafasi za kazi tutorial sijazisikia?au washawekana ndugu kwenye vitengo?

Unataka kila kitu utakisikia katika nchi hii?

Vitu vingine hata rais havisikii, wewe elewa tu kuwa kimepandishwa hadhi na kuwa chuo kikuu!
 
Dhu kumbe nscho kimeshakuwa universty..taasisi ya technolojia mbeya...inabidi tuwe makini tusije tukawa na uttr wa unversty zsizo na vwango tusipeane kufuraishana
 
Hongereni vijana na wanasayansi wetu.Acheni na kelele za siasa zinazo zungumzwa saidieni taifa lenu kwa hali na mali.Nyie ni wanasayansi na sio wanasiasa.Hakikisheni mnakipa jina kwa harufi zenu za mwaqnzo za majina yenu wotemlioshiriki kwa ugunduzi huo.
Wenu katika ujenzi wa taifa
LWLNLW

acha kupotosha weweee!!! siasa mbovu za ccm ndio zimesababisha vijana kama hawa wawe nadra kupatikana. kama kungekuwa na siasa nzuri Tanzania nakuhakikishia gunduzi kama hizi zingekuwa nyingi mno. hebu fikiria, walimu wa sayansi wa kubangaiza na bado hawathaminiwi, wanafunzi vyuoni wanapata pesa za kujikimu kwa maandamano, ni saa ngapi watakaa wa-concentrate kubuni vitu wakati tumbo halina kitu? vifaa, maabara mashuleni hakuna, bajeti zimejaa posho za vikao unategemea nini???? kuna chuo cha serikali kinafundisha Computer Engineering lakini mwaka wa tatu mwanafunzi hajawahi hata kufungua computer!!, mbona baadhi yetu sie watanzania tunapenda kuchukulia mambo juu juu tu halafu kirahisi??? sasa subiri uone kama serikali itawapa hata motisha hawa vijana, labda kama wanasiasa wetu hawa wasioamini katika uwezo wa watanzania wenzao watavutiwa na huo ugunduzi. au subiri miaka 2 halafu uulize huu ugunduzi umutunufaishaje kama watanzania, jibu lake naamini utashika kichwa ukae chini.
 
Chuo kina bahati mbaya kimebuni kifaa muda ambao serikali Dhaifu haithamini na kujali ugunduzi wa watalaamu wazalendo
 
mnhh maybe mimi sijui geography mbeya kuna eneo la maji mengi mpaka kudevelop kifaa hicho?

Na unaposema hali ya mawimbi mfano natoka dar naenda zanzibar mawimbi yapo znz kifaa kinapimwa dar itasaidia?

Mtoa mada hebu fafanua zaidi kama unajua
 
Safi sana kumbe na si tunaweza eee!

Tunaweza tatizo ni siasa chafu ndo zinakatisa tamaa na hivyo kudumaza vipaji na ugundua
we subiri usikie wanasiasa watakavyoaanza kutoa porojo kwenye hilo hadi inatawa-discourage kuanzia mgunduzi hadi wanaotegemea watumiaji!
 
Chuo kikuu cha Mbeya University of Science And Technology (MUST) ambacho Zamani ilikuwa Mbeya technical college (MTC), badaye Mbeya Institute of Science and Technology (MIST) na sasa kimepewa hadhi ya UNIVERSITY. Kimeunda kifaa maalum cha kukabiliana na ajali za majini. Kifaa hiki kinatoa taarifa za kiasi cha mzigo, hali ya mawimbi n.K kutoka ktk eneo la meli husika kwenda kwa manahodha na mamlaka za udhibiji (SUMATRA) N.K.
mmoja wa wagunduzi hao ameiomba serikali kukubali kifaa hicho ili kianze kazi mapema.

Source: STAR TV, habari ya saa 10.00 am.

Hakuna kitu kipya hapo, sasa kinazuiaje ajali? kwa maana ajali ya meli haisababishwi na mawimbi wala kiasi cha mzigo pekee. Mi nadhani hayo ni mambo ya mamlaka ya hali ya hewa isitoshe vyombo kama hivi vipo melini tayari isipokuwa meli nyingi za kisasa
 
Ni lini wamekippa hadhi ya university hiki chuo? Mbona nafasi za kazi tutorial sijazisikia?au washawekana ndugu kwenye vitengo?

umeonaeee hiki ni mbeya institute of science and technology MIST
 
mnhh maybe mimi sijui geography mbeya kuna eneo la maji mengi mpaka kudevelop kifaa hicho?Na unaposema hali ya mawimbi mfano natoka dar naenda zanzibar mawimbi yapo znz kifaa kinapimwa dar itasaidia?Mtoa mada hebu fafanua zaidi kama unajua
Jiografia ya darasa la saba: Ziwa Nyasa (aka Malawi) linapakana na mikoa gani upande wa Tanzania? Au ndo mawazo ya kuwadis watanzania wenzetu yametujaa kichwani?
 
Hakuna kitu kipya hapo, sasa kinazuiaje ajali? kwa maana ajali ya meli haisababishwi na mawimbi wala kiasi cha mzigo pekee. Mi nadhani hayo ni mambo ya mamlaka ya hali ya hewa isitoshe vyombo kama hivi vipo melini tayari isipokuwa meli nyingi za kisasa

Jambo jema ni kufuatilia jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi na sio ku-dispair kaz walizofanya wenzenu. Ni muhimu kuwapa moyo wale wanaojituma kubuni vitu mbalimbali maana mtoto hawez kukimbia bila kutambaa. Kuna notion kwamba Tz hakuna wataalamu wa sayansi, la hasha, wapo-isipokuwa tatizo ni kwamba serikali hatoi kipaumbele kwenye shughuli za utafit wa kisayansi kama inavyofanyika nchi zilizoendelea.

On the other hand, hakukuwa na haja ya kukipandisha hadhi hiki chuo wala vyuo vya DIT na Arusha tech. Bado tunawahitaji sana technicians na kwa kulingana ma mtaala wao, walikuwa wanafanya vizuri sana kuliko hata hawa wa vyuo vikuu. Graduates wa tech ni watendaji wakati hawa wa vyuo vikuu ni watu wanaosubiri kazi za ofisin.
 
Yaani Tz huwa nachoka watu wanaotengeneza magobole kule mbozi na maeneo mengine nchini hukamatwa
Alafu twatumia millions of money kuagiza silaha while tungewaendeleza hawa angalau nasi tungekuwa na AK 48
 
Back
Top Bottom