Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,664
- 59,735
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA DAR ES SALAAM (DUCE) CHASEMA CCM NDIO CHAGUO LAO KWA SASA.
Tarehe 23 desemba 2018 Ndg Said Said Nguya Afisa wa CCM Makao makuu ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Tawi la Chuo Kikuu Kishiriki Cha Dar es salaam (DUCE) uliyofanyika katika ukumbi wa Iddi Nyundo Wilayani Temeke kama Mgeni Mzungumzaji.
Katika mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Tawi Ndg Paul Kawawa umehudhuriwa na wanafunzi takribani 320, ambapo Ndg Said Said Nguya ametumia fursa hiyo kuwaeleza wanafunzi mambo makubwa ya maendeleo yanayofanywa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Ndg John Pombe Joseph Magufuli, hivyo amewataka vijana nchi nzima wawe walinzi kwa yeyote anayetaka kumvunja moyo ama kumkatisha tamaa kiongozi wetu.
Wakati huo uo kumefanyika zoezi la ugawaji wa kadi kwa wanachma wapya wa CCM takribani 220, na kwa kauli moja wameahidi kuwa wanachama waaminifu kwa CCM siku zote.
Wamesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu na Mwenyekiti wa CCM Ndg Magufuli hasa katika utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu, Ununuzi wa Ndege, Ujenzi wa Reli ya kisasa, ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Stieglers gorge n.k ambapo yote haya yanalenga kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa Mkoa wa Tanga Ndg Fredrick Chagoha, Mjumbe wa Halmashauri kuu Wilaya ya Mkuranga Ndg Bofu, na viongozi wengine ambao wote kwa wakati tofauti wamewaasa Wanafunzi mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Nidhamu, bidii ya kazi pamoja na kujitolea katika kufikia malengo.
Imetolea na Katibu Hamasa
TAWI LA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA DAR ES SALAAM ( DUCE).