Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania)

Nimefanya bachelor yangu Open
Nasema wapo vizuri sanaaa
Kinachoibeba ni idara ya research, wamedigitize na zinakua cited worldwide
Hongera mkuu kwakuwa shuhuda wa chuo hicho.
Bila shaka wengine watapata kitu kupitia wewe.
 
Rafiki yangu amedahiliwa ktk foundation course ila ishu za uchumi zimemkalia vibaya kidogo, hivyo anahitaji kufahamu inawezekana akafanya malipo mwakani na kuanza kusoma?
 
Rafiki yangu amedahiliwa ktk foundation course ila ishu za uchumi zimemkalia vibaya kidogo, hivyo anahitaji kufahamu inawezekana akafanya malipo mwakani na kuanza kusoma?
Anaweza kuahirisha/kusimamisha mwaka au mhula akiwa vizuri atarejea
 
Hivi wameanza masomo kwa mwaka huu hao jamaa?
Na vipi mtu anaweza kumaliza masomo ya Bachelor ndani ya miaka miwili kwa course ya miaka mitatu?
 
I am not an educationist/academician but kuna tofauti kubwa sana kati ya OUT na distance learning za vyuo vingine duniani, OUT hakina tofauti sana na vyuo ambavyo vinamtaka mwanafunzi na mwalimu wake kua karibu, ukisoma materials ya CIC cha Uingereza na OUT cha bongo, kuna possibility ya huyu wa CIC kumaliza mapema sana kuliko wa OUT, sijui tatizo ni nini kwa kweli!?
 
Nahisi huku complications nyingi sana
 
Nahisi huku complications nyingi sana
Niliogopa sana kusema hivo lakini huo ndio ukweli; kuna watu wanasoma Uhasibu ili wawe na leseni kwa njia ya distance learning, kwa hapa kwetu ni hizo CPA (T), watu wanasoma za board za Uingere ACCA na zile za India with Distance learning, jambo hilo ni gumu sana kwa bongo; yaani sisi tuna complicate kila kitu na still bado sio kwamba sisi ni bora saana kuliko wengine, tuna tatizo sehemu
 
Tz wametanguliza masilahi mbele sana
 
Nisalimieni Madam Grace Mbwete wa idara ya ICT, kama Lecturer wote wangekuaga kama huyu madam.. elimu ya tz ingefika mbali sana.
 
Nisalimieni Madam Grace Mbwete wa idara ya ICT, kama Lecturer wote wangekuaga kama huyu madam.. elimu ya tz ingefika mbali sana.
Salamu zitamufikia je alikuwa OUT wapi?
 
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (kwa Kiingereza: Open University of Tanzania) ni chuo kikuu kinachotoa kozi za cheti, stashahada na shahada kupita masomo ya mbali (Distance Learning). Makao makuu yako Dar es Salaam, Tanzania. Chuo Kikuu Huria kina takribani wanafunzi 70,000 kutoka ngazi mbalimbali za kitaaluma.

Historia
Kilianzishwa mwaka 1992 kwa kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992. Sheria hiyo ilipata nguvu ya utendaji rasmi tarehe 1 Machi 1993 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 55 ya gazeti lake rasmi.

Mwaka 1994, Januari 19 Makamu Mkuu wa kwanza wa Chuo alishika madaraka na mwezi huohuo walisajiliwa wanafunzi wa awamu ya kwanza.

Mwaka 2007 kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilianza kutumia sheria na taratibu zake za ndani ya chuo toleo la mwaka (2007) katika shughuli zake za kiutawala.

Taaluma
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa stashahada, diploma na shahada mbalimbali kupitia elimu ya kimtandao au elimu ya masafa ya juu kwa njia ya tehama au nyenzo nyingine mbalimbali za kiteknolojia. Shughuli za chuo zinafanyika na kutoa huduma katika viwango vya utendaji na usimamiaji wa baraza la vyuo vikuu Tanzania (TCU). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa programu takribani 125.

Vituo
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina vituo kwenye mikoa zaidi ya 30 nchini Tanzania; hii ni kujumlisha na vituo vya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (Unguja na Pemba), Kenya vituo viwili (Chuo cha Egerton na Njoro), Rwanda (eneo la Kibungo), Uganda na Namibia (Chuo cha Triumph).

Vituo vingine vya mashirikiano ya ndani ni ACDE-TCC (African Council for Distance Education- Technical Collaboration Committee), CECED (Centre for Economics and Community Economic Development), SADC ODL CoS TE (SADC Centre of Specialization in Teacher Education).

Chuo Kikuu Huria kina vituo vya kusomea takribani 69 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vitivo
Ina:

•Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
•Kitivo cha Elimu
•Kitivo cha Sheria
•Kitivo cha Uongozi wa Biashara
•Kitivo cha Sayansi, Teknolojia na Masomo ya Mazingira
•Taasisi ya kuyaendeleza masomo
•Taasisi ya Teknolojia ya Elimu
•Kurugenzi ya Huduma za Mikoa
•Kurugenzi ya Utafiti na Masomo ya baada ya Shahada
Nimeipenda tushindwe wenyewe tu

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom