Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania)

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,037
20,333
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (kwa Kiingereza: Open University of Tanzania) ni chuo kikuu kinachotoa kozi za cheti, stashahada na shahada kupita masomo ya mbali (Distance Learning). Makao makuu yako Dar es Salaam, Tanzania. Chuo Kikuu Huria kina takribani wanafunzi 70,000 kutoka ngazi mbalimbali za kitaaluma.

Historia
Kilianzishwa mwaka 1992 kwa kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992. Sheria hiyo ilipata nguvu ya utendaji rasmi tarehe 1 Machi 1993 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 55 ya gazeti lake rasmi.

Mwaka 1994, Januari 19 Makamu Mkuu wa kwanza wa Chuo alishika madaraka na mwezi huohuo walisajiliwa wanafunzi wa awamu ya kwanza.

Mwaka 2007 kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilianza kutumia sheria na taratibu zake za ndani ya chuo toleo la mwaka (2007) katika shughuli zake za kiutawala.

Taaluma
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa stashahada, diploma na shahada mbalimbali kupitia elimu ya kimtandao au elimu ya masafa ya juu kwa njia ya tehama au nyenzo nyingine mbalimbali za kiteknolojia. Shughuli za chuo zinafanyika na kutoa huduma katika viwango vya utendaji na usimamiaji wa baraza la vyuo vikuu Tanzania (TCU). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa programu takribani 125.

Vituo
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina vituo kwenye mikoa zaidi ya 30 nchini Tanzania; hii ni kujumlisha na vituo vya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (Unguja na Pemba), Kenya vituo viwili (Chuo cha Egerton na Njoro), Rwanda (eneo la Kibungo), Uganda na Namibia (Chuo cha Triumph).

Vituo vingine vya mashirikiano ya ndani ni ACDE-TCC (African Council for Distance Education- Technical Collaboration Committee), CECED (Centre for Economics and Community Economic Development), SADC ODL CoS TE (SADC Centre of Specialization in Teacher Education).

Chuo Kikuu Huria kina vituo vya kusomea takribani 69 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vitivo
Ina:

•Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
•Kitivo cha Elimu
•Kitivo cha Sheria
•Kitivo cha Uongozi wa Biashara
•Kitivo cha Sayansi, Teknolojia na Masomo ya Mazingira
•Taasisi ya kuyaendeleza masomo
•Taasisi ya Teknolojia ya Elimu
•Kurugenzi ya Huduma za Mikoa
•Kurugenzi ya Utafiti na Masomo ya baada ya Shahada
 
Ingawa kulikuwa na sheria ya kuanzisha chuo kikuu huria cha Tanzania, hakikuanza (take off) kwa nia njema. Mwaka 1989 wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar wakiongozwa na Injinia Deusdedit Kakoko (aliyekuwa bosi wa bandari) waligomea mambo kadhaa yaliyokuwa imposed chuoni na serikali kutokana na masharti ya IMF na kusababisha rais mwinyi wakati huo atamke kuwa wanafunzi walimtukana "matusi ya nguoni."

Wakati ule VC wa UDSM Profesa Mmari alikuwa anasapoti madai ya wanafunzi; hali hiyo ilisababisha Mwinyi afunge chuo kile kwa mwaka mzima, na kufanya reshuffle ya uongozi na kumfanya profesa Luhanga apande haraka hadi kuwa VC, na "kumtupa" Profesa Mmari huko OUT ambako hapakuwa na infrastructure yoyote bali jina na sheria tu.

Kinyume na matumainio ya waliomtupa kule wakidhani angekuwa frustrated, Profesa Mmari alibadilisha kabisa dhana ya Open University kwa kujenga infrastructure imara unayoijua leo kama OUT.
 
Prof Mmari ni kichwa. Recently nadhani amewahi kuwa VC wa Tumaini University Dar es salaam college
 
Ingawa kulikuwa na sheria ya kuanzisha chuo kikuu huria cha Tanzania, hakikuanza (take off) kwa nia njema. Mwaka 1989 wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar wakiongozwa na Injinia Deusdedit Kakoko (aliyekuwa bosi wa bandari) waligomea mambo kadhaa yaliyokuwa imposed chuoni na serikali kutokana na masharti ya IMF na kusababisha rais mwinyi wakati huo atamke kuwa wanafunzi walimtukana "matusi ya nguoni."

Wakati ule VC wa UDSM Profesa Mmari alikuwa anasapoti madai ya wanafunzi; hali hiyo ilisababisha Mwinyi afunge chuo kile kwa mwaka mzima, na kufanya reshuffle ya uongozi na kumfanya profesa Luhanga apande haraka hadi kuwa VC, na "kumtupa" Profesa Mmari huko OUT ambako hapakuwa na infrastructure yoyote bali jina na sheria tu.

Kinyume na matumainio ya waliomtupa kule wakidhani angekuwa frustrated, Profesa Mmari alibadilisha kabisa dhana ya Open University kwa kujenga infrastructure imara unayoijua leo kama OUT.
Aisee .... asante mwalimu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom