Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wadau, nimesoma kwenye magazeti kuwa kuna mchezo mchafu unaendelea Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) - wanafunzi wanabadilirishiwa matokeo yao. Nimeshangaa sana! Hali kama hii inaondoa imani na baadaye hakuna atakayekuwa na imani na matokeo ya wanafunzi kwa vile itakuwa vigumu sana kujua kama ni ya kweli au yamebadilishwa.

Itaweza kusababisha wanachuo wanaohitimu OUT, wakitaka kujiunga na vyuo vingine itabidi wafanye mitihani tena ili kubaini kama wana sifa zinazostahili au la. Hii siyo hatari?
 
Uwezekano huo upo, niliwahi kusikia kuna mtu mmoja pale utawala, Kitivo cha Sheria, alikuwa anapokea hongo na anambadilishia mtoa hongo matokeo. Yule jamaa nasikia alikuja kuondolewa pale utawala, kitivo cha Sheria. Inawezekana na vitivo vingine mchezo huo umekuwepo vile vile! Hii elimu ya TZ imeoza kila mahali kuanzia Shule za Msingi hadi vyuo kwa wizi wa mitihani, ufundishaji mbovu, kufoji vyeti, nk. Sasa sijui matengenezo yaanzie wapi ndugu yangu!
 
hapafai pesa ina determined kufaulu kwako kuna jamaa zangu wanasoma pale assigment sijui nini wanamshkisha tu mwl kiasi cha mboga mambo yanakuwa yamekwisha
 
Frankly speaking ....elimu ya juu hapa nchini imejaa ubabaishaji,rushwa na fitina....!
tumewahi sikia maneno kama vile..."digrii yako ipo mikononi mwangu"........."digrii za chupi".....na mengineyo mengi.
yote haya yamegubika elimu ya juu! Ikafikia wakati memba mmoja humu ndani akatoa uchambuzi wa jinsi vyuo vilivyo.......waliosoma katika vyuo hivyo walimshutumu vikali lakini ndo hali halisi iliyomo vyuoni.....!
MFANO......CHUO CHA MWALIMU NYERERE LEKCHARA ANATOA ASAIMENT ANAENDA MAKTABA ANAFICHA VITABU VYOTE......NA MWISHO WA KUKUSANYA NI KESHO JUMATATU........! unatarajia nini?(iiyear-politics)
 
Mtu aliyepata digrii kwa rushwa akiingia kwenye utumishi wa umma (labda kwa rushwa pia), ni mtu hatari sana!
 
Back
Top Bottom