MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 8,436
- 11,439
Hawa UDOM si ndio walimpelekea form JK mwaka 2010 kwa mbwembwe zote!!
Nina mashaka na GPA watakazopata Wanafunzi hao.Wanaonekana wachumia tumbo waliopitiliza.
Si ajabu walitoa maneno hayo kwa matarajio ya kupiga mzinga. Yaani wahuni wajikusanye huko tu na njaa zao kali kali wajifanye wawakilishi wa wanafunzi wote? Ni nani aliwatuma? Hawana tofauti na wale walioenda kula mishikaki kule Monduli walipotoka huko wakawa waropokaji wakubwa
Vibaka wamekusanyanana na kupeana sapoti. Eti watasaidia kuchangisha hela?ha ha ha ha! ------
dont generalize bro. we hujui kama kuna wachumia tumbo wachache wanaharibu taswira ya chuo, hao wamelishwa maneno, unakuwa kama vile huwajui ccm that is a propaganda mtu mwenye akili sasa hivi anajipanga kufanya UE sio kwenda kula kuku za LOWASA
Hawa UDOM si ndio walimpelekea form JK mwaka 2010 kwa mbwembwe zote!!
Wanafunzi zaidi ya 600 wanaosoma Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) ambao walimaliza elimu yao ya Sekondari katika shule za Kata nchini, wamemuomba Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Wawakilishi wa wanafunzi hao wapatao 40,juzi jioni walimtembelea kiongozi huyo nyumbani kwake maeneo ya Area C mjini hapa na kula naye chakula cha usiku, huku wakimueleza kuwa wapo tayari kumpigia debe, kumchangia fedha za kuchukua fomu pamoja na kuwashawishi vijana wenzao kwamba Lowassa ndiye kiongozi anayefaa kwa sasa.Hafla hiyo pia illihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanafunzi hao.
Chanzo: Mwananchi
Maskini chuki inakupelekea mpaka unawavua uanafunzi,basi malizia jumuiya ya wazazi Udom ili ufurahishe nafsi.Sema uvccm chuo kikuu cha Dodoma sio wanafunzi wa udom.