Chuo gani wanafundisha hii course hapa Tanzania?

Chuo gani wanafundisha hii course hapa Tanzania?

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
834
Reaction score
1,213
Mimi nilikua sijui kwamba kuna watu wanaweza kujiunga na masomo kwa ajili ya kusomea fitna na chuki ili kuwafitinisha watu anajiunga kabisa tena elimu ya juu na chuo kikuu

Yani anasomea masomo maalumu kwa ajili ya fitna na anafanya mitihani na anahitimu na shahada anapewa

Kisha anaingia kazini kuanza kazi yake katika nyanja tofauti tofauti na anafanikiwa

Kuanzia siasa biashara ajira mapenzi mali ndoa familia nk.

Kwavile kasomea fitna na akapata shahada basi anafanikiwa katika kuwafitinisha watu na kuchukiana

Nyinyi mtajikuta tu ghafla mmegawanyika wengine huku na wengine kule na kila mmoja ataongea anayoyajua yeye

Na ukitaka uamini haya maneno yangu wewe angalia kwa uchache juu ya hayo niliyoyataja

Angalia kwenye siasa mapenzi ndoa mali ajira biashara familia na popote pale kwenye mafanikio

Atafanya jitihada zake zote ili aharibu na mwengine akiona anachelewe kuiingiza fitna yake basi atakua yupo tayari kuongeza na ushirikina pia

Kisha baada ya kufanikiwa kuwafitisha watu hao na kugombana na chuki kuingia baina yao hapo yeye hukaa pembeni na kuhuzunika na mwengine ndio huyo huyo akawa ni mshauri mkubwa

Atatoa rai na njia ili watu wamsifie kumbe anawazunguka na kuwakwamisha na yeye ndio huridhika watu wakiharibikiwa

Fitna mbaya na huwenda akawa yupo pembeni yako anajiandaa tu kukuharibia

Umakini unahitajika vyenginevyo hakuna kupona maana mtengeneza dawa ya kuponyesha viumba ndie huyo huyo anaetengeneza sumu ya kuwaulia viumbe

Ishi kwa akili na watu wengine mnaweza mkagombana au kupigana vita wakati mpo kwenye tawi moja.
 
Umasikini unasababisha wivu. Wivu ukikomaa unasababisha chuki. Chuki ikikolea vizuri ndio roho mbaya inaingia halafu sasa matunda ya roho mbaya ni kutaka kila mtu awe masikini kama wewe au hata zaidi yako. Hapo ndio fitina na ushirikina vinaingia kazini kuhakikisha hilo lengo linafikiwa.
 
Mimi nilikua sijui kwamba kuna watu wanaweza kujiunga na masomo kwa ajili ya kusomea fitna na chuki ili kuwafitinisha watu anajiunga kabisa tena elimu ya juu na chuo kikuu

Yani anasomea masomo maalumu kwa ajili ya fitna na anafanya mitihani na anahitimu na shahada anapewa
Kipo Dar Mtaa wa Lumumba ila sijui jengo gani, wajuzi watalitaja
 
Umasikini unasababisha wivu. Wivu ukikomaa unasababisha chuki. Chuki ikikolea vizuri ndio roho mbaya inaingia halafu sasa matunda ya roho mbaya ni kutaka kila mtu awe masikini kama wewe au hata zaidi yako. Hapo ndio fitina na ushirikina vinaingia kazini kuhakikisha hilo lengo linafikiwa.
umeifafanua kozi vilivyo👏
 
Back
Top Bottom