Kuhusu watoto wa wamiliki wa shule private kusomea ualimu sjawahi kuona yaan boss amsomeshe mtt wake kuwa ticha wakati huko unaweza kuajiri headmaster kwa salary ya laki 5...
Kwa faida yako tuu kwa sasa walimu wametosha hasa wa arts kwa karibia miaka 10 hakutakuwa na uhitaji wa mwalim wa arts... maybe in minor cases
Labda nikueleze kitu
Shule nyingi waliosomea ualimu na walimu Tanzania hawajui kugeuza ualimu wao kuwa biashara
Mfano mzuri ni Uganda. Uganda walimu wazuri wa masomo tofauti huungana pamoja na kufungua shule ya Private
Wao wenyewe wanakuwa wamiliki na walimu.Uganda shule nyingi za private zinamilikiwa na walimu sio watu wa mitaani
Mfumo huo Hapa kwetu unakuta shule inamilikiwa na darasa la saba kaajiri walimu
Sisi elimu ya kujiajiri hata hatujui maana yake.Mfano wahindi na waarabu kama ana biashara inategemea kama ni ya usafirishaji anapeleka watoto kwenda kusoma digrii kama za Transport management, Business administration, Mechanical Engineering nk related subjects.
Kama ana hospital anapeleka watoto kusoma course related na hospital kama medicine,pharmacy nk
Kama mkulima anapeka watoto.kusoma digrii za kilimo nk
Sisi ndio maana biashara za kiswahili hufa mwenyewe akifa.Mtu ana malori na mabadi anampeleka mtoto kusomea udaktari kisa ohh akimaliza apate ajira serikalini anasahau ana biashara yake inahitaji mtu wa ku take over
Ona kampuni kama ASAS mzee alikufa siku nyingi kampuni inakwenda vizuri watoto wame take over
Azam pia mzee wa watu darasa la pili aliishia ila watoto kawapigisha shule hasa za biadhara Azam inapaa
Mo Dewji baba yake alimsomesha mno mambo ya biashara ona kampuni inavyoenda
Matajiri waswahili hawajui hilo
Wanawaza cheap labor tu badala ya kuingiza kwenye kampuni mtoto wako mwenyewe aliyesoma vitu vipya aendeshe hiyo kampuni kisasa na aweza jituma mno sababu ni mmojawapo wa wamiliki wa kampuni
Waswahili hawatoi hisa kwa watoto