KERO Chuo cha Ustawi wa Jamii wananyanyasa wanafunzi waliopungukiwa ada

KERO Chuo cha Ustawi wa Jamii wananyanyasa wanafunzi waliopungukiwa ada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi mwanafunzi wa degree institute of social Work campus ya dar es salaam.

Nimeathirika kisaikolojia baada ya kuzuiwa kufanya mtihani wa continuous assessment (CA) kwasababu sijalipa ada kwenye installment ya 3. Kumbuka ni mitihani ya CA sio hata mtihani wa mwisho wa semester.

Sasa, mimi nataka kuuliza kwani kile chuo si cha Serikali jamani? Kwanini wameweka utaratibu huu unaowaumiza wanafunzi ambao hasa hatuna uwezo? Kwa sababu vyuo vingine wanafunzi wanasoma na mitihan ya CA wanafanya bila kuzuiwa na mtihani wa end of semester wanafanya bila kuzuiwa ila matokeo yake ya mwisho ndo huoneshwi hadi ulipe ada na huo ndo utaratibu unaojulikana. Na sio kwamba sijalipa kabisa, nimelipa awam ya 1, 2 ya 3 nimekwama kidogo.

Hii imenifanyaa nijisikie vibaya na nimeathirika kisaikolojia kwa sababu mm ni over-thinker pia nashindwa kuzingatia masomo vizuri kwani nawaza ada nitatoa wapi.
 
Mkuu baadhi ya wakuu wa taasisi za umma hujimilikisha hizo taasisi na hizo ada wala huwa haziendi popote zaidi ya kugawana posho huku kodi zetu zikiwalipa mishahara. Kimbembe chuo hichohicho kinakutaka ujitafutie field
 
Back
Top Bottom