Chuo cha SAUT kinara ufaulu Shule ya Sheria

Chuo cha SAUT kinara ufaulu Shule ya Sheria

Mwambie ndugu yako asome hizi kanuni za Rufaa maana hawezi kuzipata kwenye tovuti ya law school au hata stationery za around law school.

Hizi hata ukeshe kuomba upewe nakala, huwezi kupewa.
Yeye karidhika na matokeo yake japo sio mazuri ila anaona ni haki yake.
 
Mleta mada (mwandishi) hayuko makini katika uchambuzi wake.
Alipaswa kutuambia hiyo idadi ya wahitimu waliofaulu Law school kutoja SAUT ni kati ya wahitimu wangapi kutoka SAUT ambao walijiunga Law school.
(Note: SAUT ndio chuo kinachodahili wanafunzi wengi zaidi wa shahada ya sheria, na ndio kinachotoa wahitimu wengi zaidi wa sheria, ndio kinachoongoza kuandikisha wanafunzi wengi zaidi kuanza mafunzo pale Law school, itakuwa maajabu kama wengi watakaofaulu Law school hawatatokea SAUT)

Kwa mfano, embu tuwaze tu, labda
Wahitimu wa SAUT waliojiunga Law school walikuwa 500, kati yao waliofaulu ni 10 (hiyo ni sawa na 2%)

Wahitimu wa vyuo vingine (UDSM, Mzumbe, Tumaini nk) waliojiunga Law school walikuwa 321, kati yao waliofaulu ni 14 (sawa na 4.4%).

Ni vipi utaiona SAUT ni bora zaidi ya wengine?
mathematical facts, uzi ufungwe
 
Chuo cha Mtakatifu Augustino cha Mwanza Campus Ya Malimbe Imeendelea Kushika Kasi katika Nafasi za Ufaulu Shule ya Sheria Kwa wahitimu Wanamaliza

Hayo Yanajiri Baada Ya idadi Kubwa Ya Wanafunzi Wanao fanya Vizuri Kutokea Chuo Cha SAUT

Mwaka jana wanafunzi 633 walifanya mtihani wa kuhitimu stashahada ya juu ya sheria kwa vitendo (PGD in Legal Practice). Kati yao ni wanafunzi 26 tu waliofaulu kwenye mkao wa kwanza (first sitting). Kati ya hao 26 wanafunzi 11 (sawa na 42%) ni wahitimu wa chuo kikuu cha St.Augustine, Mwanza (SAUT). 15 waliosalia walitoka vyuo vingine.

Mwaka huu (waliohitimu mwezi January) ni wanafunzi 821. Waliofaulu (first sitting) ni 23 tu. Kati ya hao 23, wanafunzi 10 sawa na 46% wametoka SAUT. 14 waliosalia wametoka vyuo vingine kama UDSM, Mzumbe, Tumaini, Open University, Makumira, SMMCO, St.John, MOCU etc.

Kwa miaka miwili mfululizo karibu nusu ya wanafunzi wanaofaulu Law School ni wahitimu wa SAUT.

SOURCES Via Malisa Gj

View attachment 2608611
kati ya hao waliofaulu, wanafunzi kutoka SAUT walikuwa wangapi jumla yao?
 
Hamna namna unaweza kulinganisha SAUT na UDSM kwenye kada ya sheria mkuu. Nimewahi kutana na wanafunzi wengi wa SAUT mwaka wa 4 hata plaint hajui kuandika, Ukimpa ajibu WSD ndo utacheka, ukitaka vituko mpe kazi aandae Charge, hata ku identify offence hajui.

Sijawahi kukutana na Hali kama hiyo Kwa wanafunzi wa UDSM na Mzumbe.

Hizo story za chuo flani kutoa watu wengi Huwa ni stori za vijiweni na wakufunzi Km mtaalamu Shonga au Don chuwa wakiziskia Huwa wanacheka sana Kwa dharau maana uhalisia ni tofauti.

Sijasoma UDSM lakini Kwa sheria UDSM na MZUMBE bado ni best Kwa nchi yetu Angalia hata wanafunzi wanaochukua, ni wachache na wanaufaulu mzuri hivyo rahisi kufundishika tofauti na SAUT ambao ni zoa zoa mpaka D 2 anaenda kusoma Ll.b

Ll.b3 wa mwaka huu SAUT wapo Karib 1000plus unadhani mazingira ya kujifunza yatakuwa rahisi kulinganisha na chuo kama UDSM wanachukua watu 100 ni wote ni Division one?
Sasa kwann hao wa Udsm wanafeli kuliko Saut!? Mmekariri Udsm ndio the best!?
 
Naona mnahalalisha ufelishaji wa wanafunzi unaofanywa na law school of Tanzania, makanjanja ni LST brazaj
Hiyo ni mipango mdogo wangu. Usidhanie inafanyika kwa bahati mbaya. Watu wanapigwa pini wasiingie kwa wingi kwenye chakula wasijewakaribu zaga
 
Kuna jambo hujaelewa nadhani. Mtoa post hajasema SAUT ni bora kuliko UDSM na MZUMBE, la hasha.
Amesema kwa matokeo ya Law School kwa miaka hii miwili mfululizo, SAUT wamefaulisha zaid ya vyuo vingine.

Unajua kuna tofauti kati ya kufaulisha zaid na kuwa bora

Chukulia mfano, kati ya hao 23 waliofaulu, tuseme 5 wametoka UDSM, 5 MZUMBE, 10 SAUT, na hao 3 vyuo vingine

Alafu hao 5 wa UDSM, wakawa na GPA 4-45
Hao 5 wa MZUMBE wakawa na PGA 4-43
Hao 10 wa SAUT wakawa na 3.8-4

Sasa hapo unafikiri chuo gani kitahesabiwa kuwa bora???

NB: Nimetumia GPA japo sijui km mfumo wa kipimo chao ni GPA au la
Umeelezea vizuri sana
 
Mleta mada (mwandishi) hayuko makini katika uchambuzi wake.
Alipaswa kutuambia hiyo idadi ya wahitimu waliofaulu Law school kutoja SAUT ni kati ya wahitimu wangapi kutoka SAUT ambao walijiunga Law school.
(Note: SAUT ndio chuo kinachodahili wanafunzi wengi zaidi wa shahada ya sheria, na ndio kinachotoa wahitimu wengi zaidi wa sheria, ndio kinachoongoza kuandikisha wanafunzi wengi zaidi kuanza mafunzo pale Law school, itakuwa maajabu kama wengi watakaofaulu Law school hawatatokea SAUT)

Kwa mfano, embu tuwaze tu, labda
Wahitimu wa SAUT waliojiunga Law school walikuwa 500, kati yao waliofaulu ni 10 (hiyo ni sawa na 2%)

Wahitimu wa vyuo vingine (UDSM, Mzumbe, Tumaini nk) waliojiunga Law school walikuwa 321, kati yao waliofaulu ni 14 (sawa na 4.4%).

Ni vipi utaiona SAUT ni bora zaidi ya wengine?
Umejibu vyema sana mtoa uzi na malisa wameangalia wingi na sio factor nyingine
 
Yeye karidhika na matokeo yake japo sio mazuri ila anaona ni haki yake.
Sijamwambia akate rufaa, ila nimependa asome na kujua watu wanapolalamika kuhusu law school hawalalamiki kihewa hewa tu bali wanaona ukandamizi upo mfumoni kabisa.

Haiwezekani kukata rufaa nako kujadiliwe na wasahishaji waone kama wakubali kusahisha tena au wakatae. Zingatia, mtihani unaosahishwa ni uleule aliofanya mwanafunzi, kuna ugumu gani kumsahishia tena ilhali amelipa ada?? Haombi afaulishwe bali anaomba mtihani usahishwe upya aone alipokosea
 
Shule watu wanaenda kujifunza ili wafaulu, sio kufeli.

Hakuna anayetaka kufaulishwa, watu wanataka kusahishiwa mitihani kwa haki.

Hebu tuambie, taarifa kuwa law school wamefaulu wanafunzi 21 tu umeipata wapi?
Tatizo watu wanajiunga Law school wakiwa na pass za Chini ukilinganisha na umuhimu wa course yenyewe.
Kozi ya ARTS ya kuandaa mwanasheria wa kuisemea Nchi kuruhusu GPA ya 3 nafikiri haijatendewa haki.
Wangeruhusu watu wenye GPA angalau ya 4 na kuendelea hizo kelele zingepungua......
 
SAUT ukiachana ujinga walionao kwenye suala zima la administration ya chuo huwa wanafundisha vizuri sana na mwanafunzi anatoka na ujuzi kuanzia vitendo na hata theory.
Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !
 
Chuo cha Mtakatifu Augustino cha Mwanza Campus Ya Malimbe Imeendelea Kushika Kasi katika Nafasi za Ufaulu Shule ya Sheria Kwa wahitimu Wanamaliza

Hayo Yanajiri Baada Ya idadi Kubwa Ya Wanafunzi Wanao fanya Vizuri Kutokea Chuo Cha SAUT

Mwaka jana wanafunzi 633 walifanya mtihani wa kuhitimu stashahada ya juu ya sheria kwa vitendo (PGD in Legal Practice). Kati yao ni wanafunzi 26 tu waliofaulu kwenye mkao wa kwanza (first sitting). Kati ya hao 26 wanafunzi 11 (sawa na 42%) ni wahitimu wa chuo kikuu cha St.Augustine, Mwanza (SAUT). 15 waliosalia walitoka vyuo vingine.

Mwaka huu (waliohitimu mwezi January) ni wanafunzi 821. Waliofaulu (first sitting) ni 23 tu. Kati ya hao 23, wanafunzi 10 sawa na 46% wametoka SAUT. 14 waliosalia wametoka vyuo vingine kama UDSM, Mzumbe, Tumaini, Open University, Makumira, SMMCO, St.John, MOCU etc.

Kwa miaka miwili mfululizo karibu nusu ya wanafunzi wanaofaulu Law School ni wahitimu wa SAUT.

SOURCES Via Malisa Gj

View attachment 2608611
Usichokijua SAUT law school ni Wengi Sana, unaweza kukuta katika hao 800, 200 wametoka SAUT hao 600 ndiyo wametoka Udsm, Mzumbe,tudaco, MoCU nk
 
Ndio maana yake! UDSM ilikuwa zamani enzi za wakina Prof. James, Botchwey, Kanywanyi, Nsekela etc.
Udsm Huwa sio wengi sana Kwa sabb hata admission Yao Huwa ni ndogo sana kutokana na kuweka passmark za juu sana kuliko SAUT, unaweza kukuta udsm walikuwa 40 law school yote, Wakati SAUT 200
 
Hakika huwezi Kufundishwa na Mapadre wa Kikatoliki ukawa Mpumbavu na usiwe Genius. Asanteni Wakatoliki na SAUT Mwanza kwani kwa Madini mliyonipa 2006 hadi 2009 yamenipa Jeuri Kubwa kokote ninapokuwa kutokana na Kuniongezea Akili nyingi na zilizotukuka Kichwani mwangu.
Akili Gani ulizonazo? Mbona bado akili huna,
 
Back
Top Bottom