Chuo cha SAUT kinara ufaulu Shule ya Sheria

Chuo cha SAUT kinara ufaulu Shule ya Sheria

Chuo gani Jurisprudence wanawafundisha mwaka wa kwanza , hivi mtoto katika zake sekondari ndio unaanza kumkandika jurisprudence? Ataelewa sheria gani? Halafu Wana furushi la masomo ambayo sio ya kisheria comparative religions, mara Kifaransa. Mtu anamaliza na cheti kuonekana kafautu Kifaransa lakini ukimuuliza "comment allez vous" hawezi kukujibu
Juriprudence lazima isomwe mwaka wa Kwanza ili mwanafunzi aelewe falsafa za sheria atakazo soma baadae. Naunga mkono kwa hilo wanalofanya SAUT
 
Juriprudence lazima isomwe mwaka wa Kwanza ili mwanafunzi aelewe falsafa za sheria atakazo soma baadae. Naunga mkono kwa hilo wanalofanya SAUT
Unaleta madhara? Mwaka wa kwanza aelewe huo uchawi wa PROFESA MKOYOGO ( R.I.P)?
 
Mleta mada (mwandishi) hayuko makini katika uchambuzi wake.
Alipaswa kutuambia hiyo idadi ya wahitimu waliofaulu Law school kutoja SAUT ni kati ya wahitimu wangapi kutoka SAUT ambao walijiunga Law school.
(Note: SAUT ndio chuo kinachodahili wanafunzi wengi zaidi wa shahada ya sheria, na ndio kinachotoa wahitimu wengi zaidi wa sheria, ndio kinachoongoza kuandikisha wanafunzi wengi zaidi kuanza mafunzo pale Law school, itakuwa maajabu kama wengi watakaofaulu Law school hawatatokea SAUT)

Kwa mfano, embu tuwaze tu, labda
Wahitimu wa SAUT waliojiunga Law school walikuwa 500, kati yao waliofaulu ni 10 (hiyo ni sawa na 2%)

Wahitimu wa vyuo vingine (UDSM, Mzumbe, Tumaini nk) waliojiunga Law school walikuwa 321, kati yao waliofaulu ni 14 (sawa na 4.4%).

Ni vipi utaiona SAUT ni bora zaidi ya wengine?
Ukiachana na maswala ya Russia na Ukraine, kwenye mambo mengine upp vizuri.
 
Chuo cha Mtakatifu Augustino cha Mwanza Campus Ya Malimbe Imeendelea Kushika Kasi katika Nafasi za Ufaulu Shule ya Sheria Kwa wahitimu Wanamaliza

Hayo Yanajiri Baada Ya idadi Kubwa Ya Wanafunzi Wanao fanya Vizuri Kutokea Chuo Cha SAUT

Mwaka jana wanafunzi 633 walifanya mtihani wa kuhitimu stashahada ya juu ya sheria kwa vitendo (PGD in Legal Practice). Kati yao ni wanafunzi 26 tu waliofaulu kwenye mkao wa kwanza (first sitting). Kati ya hao 26 wanafunzi 11 (sawa na 42%) ni wahitimu wa chuo kikuu cha St.Augustine, Mwanza (SAUT). 15 waliosalia walitoka vyuo vingine.

Mwaka huu (waliohitimu mwezi January) ni wanafunzi 821. Waliofaulu (first sitting) ni 23 tu. Kati ya hao 23, wanafunzi 10 sawa na 46% wametoka SAUT. 14 waliosalia wametoka vyuo vingine kama UDSM, Mzumbe, Tumaini, Open University, Makumira, SMMCO, St.John, MOCU etc.

Kwa miaka miwili mfululizo karibu nusu ya wanafunzi wanaofaulu Law School ni wahitimu wa SAUT.

SOURCES Via Malisa Gj

View attachment 2608611
Tatizo huyo Malisa naye kila kitu anajifanya anajua...kwa akili ndogo tu ya kawaida mbona hajatuambia katika hao waliofaulu kutoka saut ni Kati ya wahitimu wangapi kutoka chuo hicho? What if kama Kuna chuo wamehitimu wanafunzi watatu afu wakafaulu wawili haoni kama Hawa watakuwa wamefanya vizuri zaidi katika ufaulu? Assume saut wamefaulu 10 Kati ya 100 na chuo x wamefaulu 2 kati ya 3 wapi hapo tutasema wamefaulu vizuri? Arudie kufanya uchambuzi wake apunguze kukurupuka
 
Kama ni hivyo kuwa UDSM wanaweka pass mark za juu basi ningetegemea hao wachache wanaokwenda Law school ndio. wangefanya vizuri na kuwa katika Kundi la wafaulu!! Unfortunately, sio hivyo!
Wanaoenda law school kutoka udsm ni wangapi? Unajua idadi yao? What if wakawa wameenda 10 na kufaulu 7 hapo utasemaje? Leteni data kamili ili tuone Kama uchambuzi wenu una mashiko
 
Back
Top Bottom