Watu hawakuelewi sababu wanajitia ujuaji mwingi na hakuna hata mmoja aliyeweza kujibu swali lako.
Ninachofahamu mimi ni kwamba askari wetu anapomaliza cadet course kwa wale ambao wameingia spacial programme hupelekwa TMA kwa ajili ya kozi za uofisa na baada ya hapo huwa commissioned kulingana na viwango vya elimu zao na kozi walizosomea kwa maana kuna ambao kwa elimu yao watapewa Asst. Lt, Lieutenant, wengine Captain kwa watu kama marubani na madaktari.
Kuhusu wengine kupelekwa nje na kupewa nyota hukohuko kwa sasa sina uhakika nachofahamu zamani kulingana na baadhi ya utaalamu hatukuwa nao walikuwepo maofisa wengi waliopandishwa vyeo hukohuko kama waliopelekwa Cuba, Israel na Urusi na Jamhuri za kisovieti.
In short askari wapo wanaenda kozi za kila aina huko nje ila akimaliza kozi akirudi home ndio atasubiri wakati wa commission zikitolewa basi file lake kama safi na anadeserve commission ndio hupewa cheo.
I hope nimekujibu kulingana na swali lako