Chuo cha Kiislamu cha Al Mustafa Mbezi Beach Chateketea kwa moto

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Chuo cha Kiislamu cha Al Mustafa kilichopo maeneo ya Mbezi Beach Makonde, Jijini Dar es Salaam kinateketea kwa moto. Chanzo cha Moto huo bado hakijajulikana.



=====

UPDATE:

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amesema moto uliounguza Chuo cha AI Mustafa Mbezi Beach Dar es salaam usiku huu umesababisha Mwanafunzi mmoja kujeruhiwa lakini hakuna ripoti ya kifo licha ya madhara ya vifaa kuungua ikiwemo komputa mpya 30, magodoro, passport na vyeti.

"Moto umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa, zoezi linaloendelea sasa ni kuwahamisha Wanafunzi wote 120 wa Chuo hiki kutoka Mbezi Beach na kuwapeleka Temeke ambako kuna eneo ambalo limeandaliwa kwa ajili ya Wanafunzi hao kulala kwa leo huku taratibu nyingine zikiendelea kufanywa"

"Tutafanya uchunguzi kujua kilichotokea lakini kwa sasa usalama umedhibitiwa maeneo haya, Wanafunzi kwa sasa wanapelekwa Chang'ombe na tayari gari la kwanza limeondoka na Wanafunzi 50, kuanzia kesho tutakaa na Uongozi wa Chuo kuona juhudi za kufanya ukaratabati ili shughuli za Chuo ziweze kuendelea"

Chanzo: Millard Ayo
 
Back
Top Bottom