Chumvi imeadimika mitaani

Stayfar

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
1,092
Reaction score
2,297
Haijapata kutokea,hata ilipokuwa kipindi cha uongozi wa Hayati Baba wa Taifa,hatukuwa kupitia hali hii Chumvi kukosekana.Ajabu sana awamu hii, Chumvi imekuwa bidhaa adimu madukani.

Ilianza Dola, Umeme, ikaja Sukari, Sasa ni zamu ya Chumvi. Madini tunayochimba hapahapa nchini. Kuanzia Kigoma, Dodoma Dar hadi Mtwara huko kote kunachimbwa Chumvi. Sasa iweje iadimike nchini! Kuna shida gani?
 
Upo mkoa gani? Maeneo ya pwani sidhani kama kuna shida ya MUNYU.....Daslamu chumvi pakti 3(500g) ni Tsh 1000
 
uko mkoa gani mkuu
tukuletee chumvi
hapa tarime ni nyingi kwa 500 tu
 
Chumvi ipi mleta mada unayoongelea?! Ni hii hii chumvi ya Uvinza ama nyengine?! [emoji848]
 
Kwani sukar ilivo adimika ilikua inatengenezwa nje ya nchi?
Viwanda vya sukar vipo vingi tuu
TPC moshi3
Mtibwa
Kilombero
Kagera
Manyara
Bagamoyo
Rukwa sugar
Mbeya sugar
Kwa nn ushangae chumbi kuadimika??


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…