Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,046
- 3,078
Jibu rahisi ni kwamba balance of payment haijakaa vizuri,tunachopeleka nje kina thamani ndogo kuliko tunachoingiza nchini kutoka nje,hivyo tunatoa dola (foreign currency) nyingi kuliko tunavyopokea,fikiria ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya treni ya SGR unafanyika kwa fedha za kigeni,jibu lingine ni kupanda kwa bei za mafuta kumechangia,maana kama ulikuwa ukitumia dola milioni moja kuagiza lita X za mafuta baada ya kupanda utahitaji dola zaidi kuagiza kiasi kile kile,na jibu lingine Kama kutakuwa na usimamizi mzuri, kilimo pekee kinaweza kuleta mapinduzi katika biashara na kubadili thamani ya kubadili fedha.
Kama mazao yote yataongezwa thamani kabla hayajauzwa nje, nchi itapata fedha nyingi… unaweza ukaona hata madini tunayasafirisha yakiwa hayajaongezwa thamani, jambo ambalo si zuri kwa mustakabali wetu kiuchumi kama nchi,Kwa maoni yangu, sababu kwa nini export na import zina-corelate na thamani ya shilingi ni kwa sababu mara nyingi uchumi ukikua na kukomaa tunakuwa na bidhaa nyingi zenye ubora sana na kuna uwezekano zaidi wa watu wa nje kuzihitaji, na hivyo demand yake ya nje itaongezeka kwa kuwa tumekuza uchumi wetu kwa kutumia exports (exports led growth).
Ili sarafu (currency) yoyote ifanye kazi lazima kuwe na uaminifu (trust),lazima watumiaji waamini kwamba currency hiyo thamnani yake ni imara (stable),wasipoamini hivyo watapunguza matumizi yake au kuacha kabisa,na thamani yake itazidi kuporomoka,trust ni muhimu kwa currency yoyote,hata kama umei-peg kwa gold,lazima mtu aamini kwamba thamani ya gold haitashuka kamwe,Ili kitu chochote kitumike kwa ajili ya kubadilishana thamani,nilazima kitu hicho kiwe na guarantee of value,yaani ili mimi nikupe dhahabu wewe unipe yale makaratasi ya dollar,
Uhakika wa uthamani ni muhimu,ni lazima kuwe na guarantee some where kwamba nikipeleka hayo makaratasi nitapata thamani inayokaribiana na thamani ya dhahabu zangu,makaratasi hayo tumekubaliana yaitwe dollar,Without this guarantee no one would use the currency as the medium of exchange,tunaitumia dhahabu kama currency,sababu haina explicit guarantee ya value, lakini mtu atakuwa tayari kubadilisha bidhaa yake na dhahabu (Gold)kama anaamini kwamba baadaye atarudisha thamani yake kwa kuibadilisha hiyo gold na kitu kingine chenye thamani sawa na hiyo,kuna wakati chumvi ilitumika kama currency, kwa sababu wakati huo watu walikuwa wanaamini kwamba akibadilisha kitu na chumvi atarudisha thamani yake hapo baadaye.
Uwingi wa rasilimali tuliyojaaliwa Watanzania,hauwezi kudhani kiwango cha matumizi ya Dola nchini kikafikia kiasi cha kuwa na madhara kwenye uchumi wetu,sasa ukiona benki kuu imesema hifadhi ya dola imepungua(dola ndio tumekubaliana iwe kipimio) inamaanisha demand(hitaji) la dola ni kubwa kuliko supply(upatikanaji),hivyo expenditure ya forex (matumizi ya dola)ni makubwa,kumaanisha tunatumia (spend) kwa dola (forex) kuliko dola (forex) tunazoingiza,hii maana yake tuna import zaidi kwa kutumia dola (forex) kuliko export ya forex income zetu,hivi karibuni tumekuwa na miamala mingi(Telegraphic Transfers) kwa ajili ya kuagiza mizigo China na uturuki,
-Swali,
Kama Watalii na mikopo ya masharti nafuu vinaongezeka kwa nini fedha za kigeni zipungue?
Hakuna ndege itabeba pesa kuleta Tanzania,zaidi ya mzungu kuja na briefcase mkononi na kukabidhi hundi (cheque) ya benki yao uko ulaya na pesa hizo zitahamishwa kama shilingi pale hitaji linapotokea, kama madolari ya mikopo yangebebwa na meli na kuingizwa katika mzunguko wetu wa fedha,basi zingeweza kusababisha upatikanaji wa dola katika soko letu la fedha,hivyo kuongezeka thamani shilingi yetu,fedha za mikopo ziingiapo kwenye mzunguko,zinasaidia kupunguza uhaba wa dola na kusababisha dola kuuzwa kwa bei nafuu na kuchangia kupandisha thamani ya Shilingi,leo dola moja ya Marekani inanunuliwa kwa shilingi 2,370 pengine January dola moja inaweza kununuliwa kwa shilingi 2,400
Uchumi wetu ukikomaa,uzalishaji ukaongezeka hata kama ni kwa ajili ya mahitaji ya ndani tu, ajira zikaongezeka, etc, hata kama exports hazitapanda kihivyo kuna uwezekano wa thamani ya shilingi kupanda,Hayati Rais Magufuli walau alithubutu kupigia kelele viwanda viwanda viwanda,agenda ya viwanda kwa sasa nayo imekufa na dira ya nchi hatuelewi ni ipi,naamini tuna tatizo sehemu ujamaa ulituathiri kama taifa,angalia hata mtanzania anavyotembea barabarani kwanza anasalimia kila mtu na wakati huo anatembea kwa kuburuza miguu yaani hayupo faster kabisa,not smart at all,tupo kiujanja ujanja tu kama sungura,
Nimalizie kwa kusema sisi ndio shilingi kwa maneno mengine dollarisation has created weak demand for Tsh.sijui tunafeli wapi,kushuka kwa uchumi na pesa kukosa thamani itapelekea people shunning away from Tshs,inamaana Tsh is becoming cheaper na ndio matokeo yanayoonekana,itapelekea inflation na effect ya inflation in the end consumer wanaloose appetite ya local currency.If the worse comes to the worse,itakuja watu wanaanza kubadilishana vitu kuepuka kutumia madafu,Je, utapendekeza tuweke sheria kwamba watu hawaruhusiwi kubadilishana vitu?mliopewa dhamana ya uchumi wetu, kindly solve the core problems,tusisubiri madhara ya inflation,Case study Zimbabwe.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.