Shida na raha
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 3,773
- 3,474
Habari za majukumu wakuu wenzangu.
Ni historia ndefu ila nitajaribu kuipunguza kidogo.
Ilikua mwaka jana maeneo ya ferry Kigamboni baba mdogo alikua ameshauza samaki wake na kumalizia kufunga mahesabu, ghafla walimfata watu wawili ambao walimzuga na kujifanya wana vitu vya thamani wanataka kumuuzia.
Na yeye kwakua tayari alikua ameshazugwa, ilibidi atoe milion mbili na kuwakabizi.
Hatimae kajikuta hana kitu hata kimoja bidhaa na hata pesa mkononi hakujua zimeenda wapi.
Alichanganyikiwa na kuwa chizi kabisa, hakuwa anaelewa kinachoenda wala kurudi.
Alijikuta amelala ufukweni wala hakujua ni nani alimlaza pale.
Alijijua baada kuona anaitwa na mkwe wake kumbe hakuwa mkwe bali ni mashetani ndo yalimuamsha na kuelekea nyumbani kwake. Ilimbidi amweleze mkwe wake ambae ni mganga...
Mkwe wake akaingia mzigoni kutaka kumsaidia, hakukua na masharti magumu kazi ilienda vizuri.
Mkwe wake alimwambia nitakuonesha waliokuibia pesa zako ila tusiuwe,,, bamdogo alikubali kwa kua nae pia hakuna tayari kufanya mauwaji.
Ila alimuhakikishia kwamba... Kila aliehusika na wizi ule basi atamfilisi na kweli iliwezekana.
Alianza kumtajia watu kama watano, na wote bamdogo alikua anawajua, hao watu ni wapemba ambao walifanya mchezo huo.
Siku ziliendelea watu watatu walianza kuwa machizi, yule bosi wao alianza kuunza nyumba na gari, nyumba ambayo ilikua na thamani kama million 25 aliuza kwa milioni 6 watu hawakuamini walijua hana radhi.
Nyumba yenyewe ipo Daraja bovu Zanzibar.
Gari ya milioni 18 aliuza kwa m 8,,, gari ilikua Pemba.
Walivyopata habari wapi wamekosea walianza kulaumiana kwanini wameenda kumtampeli mtu yule wakati wanajua fika kwamba mkwe wake hataki masihara kwenye masuala ya kipuuzi.
Wazee wa wale waliofanywa machizi walikwenda kuomba msamaha ili watoto wao wapone.
Hao kwakweli ni matapeli sana, bamdogo alinisimulia na kunisihi nisije nikawaambia chochote maana wanajua hakuna watu wengine wanaojua kwa maovu wanayoyafanya.
Mwisho nawasihi wanajamii wenzangu, usimuamini mtu yeyote kukuita na kumsikiliza ikiwa hauna imani nae (kumfam). Watu wamebasilika sana.