Bwana Bongo
Senior Member
- Dec 12, 2021
- 167
- 239
Mikopo ya Ushauri
Kila mtaa una wale watu wanaokopesha kila kitu—pesa, nguo, kiwanja, nyumba, gari.
Lakini aliibuka mtu mmoja yeye, alikopesha ushauri.
Ndiyo. ushauri. Alikuwa anaitwa Mshauri, lakini wengi walimwita tu Mjomba Kichwa.
Hakukuwa na kitu ambacho hakuwa na maoni nacho. Ukiwa na shida ya ndoa, elimu, biashara, siasa, ukienda kwake umerudi na suluhisho.
Si kwa sababu alikuwa bingwa sana, ila alijua kuzungumza kwa namna ya kukufanya ujisikie una jibu.
Siku moja, Bwana Bongo alikaa nae kijiweni. Akamwambia:
“Mjomba, unawakopesha watu ushauri, lakini mbona wengi bado wanaishi vile vile? Au unawakopesha ushauri wa muda tu?”
Mjomba akatabasamu, kisha akajibu:
“Tatizo si ushauri wanaopewa, ni namna wanavyoutumia. Nikikupa ushauri ikiwa hukufata ipasavyo" Kama gari isiyoendeshwa.
Na mwingine akipewa ushauri, anadhani ana uwezo wa kuwadanganya wengine badala ya kujisaidia mwenyewe.”
Bwana Bongo akacheka kisha akaongeza:
“Kumbe ushauri ni kitu cha kuendelezwa. Maana hata ukikopeshwa pesa kausha damu, usipojua utalipa vipi hela ya watu itakula kwako.”
Mjomba Kichwa akacheka sana. Kisha akasema:
“Tatizo la wengi si kukosa akili, ni kutokujua walipoiweka.”😅