Chuki na husda dhidi ya wanaDiaspora

Kuna hili kubwa jinga linani.............
 
Mwenye hoja isha sema ni Chuki hivyo mnaokataa sio chuki ila ni....Nyie tuambieni haswa ni sababu gani mnaweka pingamizi uraia wa nchi mbili. Tunapenda sana kufahamu


Ni ukweli mtupu huwezi tumikia mabwana wawili kwa usawa!
Uwepo wa Uraia wa Nchi tofauti x2 ni kitendo kinachopdhalilisha asili ya Binadamu. Huwezi kuwa Mtanzania na wakati huu ukawa Mkenya.


Wale wote wenye nia ya kuishi popote duniani wajitahidi kuelekeza nguvu yao kwenye Sera ya Dunia Moja(Serikali Moja duniani kote) NWO.




Na kwa Maoni yangu; Ili kulinda Utaifa .Nawaomba wajumbe kuimarisha ibara hii kwa kuongeza;

Uraia wa Kuzaliwa.
57.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa
Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni
au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya Muungano na kwamba mtoto huyo hajapata kuandikishwa kuwa Raia halali wa Nchi alikozaliwa.
 


Watanzania aka Wabongo tu waoga sana wa mabadiliko na fikira zetu ni mgando. Ndio maana pamoja na CCM kuendelea kutufanya kwa mabwege itaendelea kutawala. Kwa sababu tunaogopa kuleta chama kingine . Ndio maana pamoja na muungano kutokuwa na faida yo yote, tutaendelea kuutetea. Dunia ya utandawazi ni tofauti na hiyo dunia unayoizungumzia. Tunaogopa kukubali uraia wa nchi mbili, wakati huo huo tunapiga domo ya kukumbatia utandawazi. Mnafikiri WaNigeri, au WaKenya, au WaGanda wanakosa nini waliporuhusu uraia wa nchi mbili. Hawa jamaa ni wajasiriamali na kama huamini pekua data za uchumi wao. Sisi tutakalia kuongonzwa namitazamo ya watawala wetu wenye fikira mgando na za kijima. "mtu huwezi kula huku na kule" JK
 

Watanzania wezangu mnaopinga dual
Naomba mtutumie akili na kuzishirikisha hizi akili. Hili si tusi, bali naomba mzishirikishe akili kwa tija yenu, yetu na kizazi chetu na kwa taifa kwa ujumla.
Kwasababu kupinga citizenship kwa Tanzania, hii inamnyima dual mzawa wa Tanzania tu na si mtu mwingine asiye mzawa. Hii inampa haki zaidi Mkenya kwa uzawa kuliko mTanzania kwa uzawa, kutokana na kwamba sheria hii tuliyonayo ya kijima bado inaruhusu kupewa mkenya uraia ama raia yeyote wa nje kuwa raia Tanzania kwa kuukana uraia wake wa awali. Nitakupa mfano kwanini hii sheria ni ya kinyanyembe kwa waTanzania wazawa tu.

Kwa sheria iliyopo
Mfano mie ni mkenya nakuja bongo naoa naomba citizenship(passport) napewa na Tanzania wanachukua passport yangu ya kenya. Poa, natumia passport ya Tanzania naingia kwetu Kenya, nikifika Kenya naomba passport nyingine ya Kenya na kwa sababu Kenya wanaruhusu kuwa na passport mbili hawaninyang'anyi ya Tanzania wananiachia. Narudi Tanzania nikiwa na passport mbili (Dual citizenship) na nunua ardhi ya Tanzania kubwaaaaaaa. Mmeona hapo???????

Hii sheria mnayotetea ya kijima na kinyanyembe , hailindi masilahi yoteyote ya Tanzania kwa njia zozote zile na kwa namna yoyote ile hata ya kubuni. Badala yake ina nyanyasa tu waTanzania wakuzaliwa na kupendelea wazawa wa nchi zingine, sijui sheria ya namna hii italinda vipi masilahi ya nchi???

Hii sheria ya kijima na kinyanyembe, wenda ilifanya kazi karne ile kwa sababu nchi nyingi wakati wa karne ile walikuwa hawaruhusu dual citizenship, hivyo ilikuwa ukichukua citizenship ya nchi husika na passport yako wanachukua na wanaituma nchi kwako hivyo ilikuwa kweli strictly unajulikana umekana uraia, lakini sasa sio hivyo. Kwa sababu mie mkenya niliechukua uraia wa Tanzania na kurudi kenya kuomba passport mpya Tanzania hawatajua kama nimeomba passport mpya ktk nchi yangu ya kuzaliwa, kwa sababu kenya haitaichukua passport yangu ya Tanzania na kuituma Tanzania ama kuwasiliana na Tanzania kabla ya kupewa passport nyingine ya Kenya.

Wanaotetea hii sheria ya kijima na kinyanyembe hawana hoja hata moja zaidi ya wivu wa kuwafunga watanzania wenzao wakati huohuo wakiwapa DUAL raia wa kigeni. Amkeni
 

Uraia wa nchi mbili Tanzania tayari upo kilichokuwa hakipo ni umiliki wa pass za kusafiria mbili. Kama huamini waulize wazanzibari kwa nini wana ID card za uzanzibari na sasa wanapewa ID card za utanzania?
 


:A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 
Sikubaliani nawe kwa mambo yote mawili!
Hatuwezi kutathmini michango yao kwa kulinganisha na wengine ambao nchi zao zinafanya jitihada za makusudi za kuhakikisha flow ya mapato ya raia wao. Pia michanga inayoonyeshwa huwa inajumuisha na raia wanaokwenda kufanya kazi nje na kutuma mapato yao kwao. Uzoefu tulionao sisi tunaoishi nje ni kuwa Watanzania hawako tayari kufanya kazi nje isipokuwa wale wanaokimbia na wale walio na taaluma zinazolipwa fedha nyingi. Aidha serikali za wenzetu zinachukuwa jitihada maalum za kuwalinda raia wao kimasilahi wakiwa nje ya nchi.
Sababu zote hizo zinafanya hili jambo la kupima faida ya diaspora kwa kuangalia kipato wakiletacho, isiwe kigezo kizuri.
Kuhusu hoja ya wao kujieleza mbona huwa wanafanya hivyo sana tu na viongozi wanajuwa hilo kwani wao ndio wanaokutana nao. Lakini sasa angalia ni sisi wananchi wa kawaida tunaojali kinachoitwa kutanua kwa diaspora ambao tumekuja na dhana ya kukataa uraia wa nchi mbili. Waulize kwani kuna athari gani Watanzania hawa wakirejeshewa Utanzania wao hakuna sababu za msingi.
 
Ninyi ndo watu mnaitwa ma-straight jackets, never to think outside the box.

Aliyekukataza kuwekeza kwenu ukiwa nje nani?
Na hata kama una vijisenti huko nje nani kakukataza kuzituma kwenu au kwa jamii yenu.

Tatizo la wengi wenu ni la kisaikolojia, mnataka kutambuliwa as if you are different!
Mkirudi kututembelea Piteni mitaani bongo na muone jamaa wanavyofanya biashara za uhakika na kutengeneza fueza ndefu.
 

kwa membe unamwonea kwa kweli,amejitahidi sana kulisemea hili na hata alipokuja china muda wote alikuwa akisisitiza swala la uraia pacha.
Kwa upande wangu namwona mh membe amefanya yake na kilichobaki ni wajumbe wa katiba kulipitisha ama la.
 
Mkuu wangu hivi huwa unafuatilia habari za Tanzania? Manake kama ungekuwa unafuatilia sidhani kama ungemwingiza Membe kwenye hicho unachoita chuki. Membe ndie waziri ambae anapigania sana suala la dual citizenship unless kama cjakuelewa! Membe mara zote amekuwa akisema wazi wazi kwamba si haki hata kidogo kwa mtu kupokonywa uraia wake kwavile tu amechukuwa uraia wa nchi nyingine wakati wengi wao wanafanya hivyo kwa ajili ya maslahi ambayo wanaweza kuyapata kwa kuwa raia wa hiyo nchi. Hata wakati wa maoni kwa Jaji Warioba, moja ya maoni ya Membe na Wizara yake ni hilo la dual citizenship.
 

Lyimo, hili siyo swala la mtu mmoja bali ni la kitaifa ndiyo maana ni sehemu ya katiba yetu. Kama million 45 walioko ndani hawaoni faida, sidhani kama kuna faida ya hii kitu TZ. Kwa kusema kwamba eti kundi fulani liloby ina maana kuwa hiyo sheria ipo kwa ajili ya hao wachache. Maswala kama haya lazima yaamuliwe kwa maslahi ya nchi. Hii issue mpaka kufikia sasa haikuibuliwa na wana Diaspora imeanzia huko huko serikalini. Sasa sioni ni kwa sababu gani wazo lao wenyewe halafu watu watoke nje waje kuloby badala ya wao wenyewe kulitetea. Hata huko Kenya, India au Nigeria wana Diaspora hawakujikusanya na kwenda kuloby bungeni au serikalini. Kama tunajiona bado hatuko tayari ni sawa .............. tuache mpaka tutakapokuwa tayari. Maana TZ tusha zoea kuwa wa mwisho katika kila kitu!!
 
Mkuu OLESAIDIMU, salaam! Hebu tujadiliane kidogo. Assume NasDaz nipo German for 10 years na kwa sheria za German, mtu aliyeishi pale for 10 years or more anaweza ku-claim citizenship. Likewise, assume nataka ku-invest in tourism industry, lakini kwa sheria za German, anyone investing in the sector MUST be German Citizen. Kutokana na hilo, naamua ku-claim German citizenship si kwa sababu naipenda sana Ujerumani bali nafahamu nikishapata Uraia, nitarahisisha mambo yangu...ikiwa ni pamoja na hilo la ku-invest in tourism industry! Now tell me, what kind of serious crime niliyoifanya hapo hata ninyang'anywe uraia wangu wa Tanzania? Kumbuka, mtu ameenda ughaibuni kutafuta maisha..kule anagundua ukishapata uraia, basi mambo ndo yanakuwa rahisi zaidi kuliko otherwise...kinyume chake, huku nyumbani tunasema that's serious crime ambayo hukumu yake ni kukunyang'anya uraia...that's not right at all.

Lazima tufahamu kwamba, wengi wa wale wanao-opt kupata uraia wa kule kwingine, wanafanya hivyo kwa ajili ya maslahi na wala si kwamba mahaba yao yanahamia huko!
 
Mkuu Mr. Zero, I berg to differ with you to some extent. Diaspora is one of Interest Group kwa suala zima hili la Katiba Mpya...is like jamii ya wafugaji, wenye ulemavu n.k. Pamoja na kwamba suala la Diaspora limekuwa engineered kutokea serikalini, Diaspora nao wana wajibu wa kushawishi wajumbe...si lazima waende pale bungeni; we've social networks now. Pamoja na kwamba serikali ndio wameleta suala hili, nao wanaweza kusaidia kuelimisha jamii coz' ndio wanaofahamu vizuri nini umuhimu wa hii kitu! It's very unfortunately kwamba kuna watu wengi sana hawafahamu dhana mzima ya Diaspora na dual citizenship. Linapokuja suala la duala citizenship, wengi wanadhani kwamba hata yule mshikaji aliye pale (say) Kinondoni au Sinza, anaweza kuchukua Uraia wa US...wanachodhani ni kwamba yule mfanyabiashara mjanja mjanja wa Kariakoo, anaweza kwenda kuchukua uraia wa China, kisha akishafanya mabo yake hapa, anasepa China! Watu wanadhani kwamba yule Mkurugenzi fulani pale mitaa ya Samora, anaweza kuchukua uraia wa Malaysia kisha anaiibia serikali na kukimbilia Malaysia! Wengi hawafahamu kwamba tunaposema dual citizenship inamuhusu Mtanzania aliye nje ya nchi...kwamba anachukua uraia wake kule ili arahisishe mambo yake bila kupoteza uraia wake wa Tanzania! Si sahihi kusema kwamba kv ni suala lililoibukia wizarani basi ni wenyewe ndio walipigie debe. Ikiwa Diaspora watetewe na serikali yenyewe, what about wafugaji, walemavu, wanaharakati n.k?
 
Last edited by a moderator:
Wewe unajuaje kama maisha yako unayaendesha pasipo sisi, Unajua ni Watanzania Diaspora wangapi wamewekeza miradi yao nchini na imetoa ajira kwa Watanzania?. Ama unatazama vitu kwa rangi zake maana Wazungu, Wachina na Wahindi unawaona na kuwatofautisha nasi kutokana na rangi zao (race) lakini sisi Watanzania wazawa wenye rangi ya makalio hata kama tukiwekeza unachokiona na kudhania kila mwekezaji mweusi ni Mtanzania wa ndani pasipo kujua ukweli. Unaona jinsi akili yako inavyokudanganya wewe mwenyewe!


Mkuu binafsi nimewekeza nyumbani na nimewaajiri Watanzania ambao wanapokea mshahara mzuri tu na wanalipa kodi, biashara yangu kiduchu lakini inalipa kodi, hivyo sio swala la mimi kuwepo ama kuishi Tanzania isipokuwa uraia pacha uutrawawezesha hata watoto wao wewe kufikiria nje ya box. Ikiwa hakuna ajira nyumbani wataenda nje, hakuna Elimu bora nyumbani wataitafuta nje na kadhalika pasipo kupoteza Uraia wao.

Taabu tunazopitia sisi tunaporudi nyumbani hazina maelezo. na kwangu binafsi ni upumbavu mkubwa kunipa visa ya miezi mitatu mkitegemea within miezi hiyo nitaweza kumaliza yaliyonileta nyumbani, matokeo yake tunaishi Kidanganyika. Mfumo huu unasababisha rushwa kila kona maana wakijua wewe sii raia vijana wa TRA watakupa njia za kuepa kodi, Immigration officer watataka kukuongezea muda kupitia mlango wa nyuma yaani kifupi uraia wa nchi moja hauendani kabisa na dunia tunayokwenda.
- Nimemaliza.
 

Nimeoma point yako mkuu. Ni Watanzania ndio wanapata hasara wasipo ruhusu dual citizenship. Kwa hiyo ni naona kama tz wanakataa mzawa kuwa na urai pacha basi wazuie mgeni yeyote ambae kwao kuna uraia pacha asipate uraia tz which is not possible.
 

Mimi nawatetea walo nje japo sina tatizo hilo. Wabongo tulio nyumbani hatuna sababu ya kuzuia uraia pacha kwa walio nje zaidi ya wivu tu. swala ni haki ya kuendelea kuwa watanzania baada ya kuchukua uraia wa nje. Uraia pacha utawa-protect kisheria kama wana kijisha au kibanda chake wasije wakatapeliwa na mnao jifanya mnatengeneza pesa ndefu kumbe mnafanya ufisadi. Watu bongo malizao wakati ni raia halali . Je itakuwaje kama mafisadi wakijua wewe sio rai kisheria. Watu wameondoka bongo kwenda kutafua elimu nje baada ya kukosa nafasi bongo mnataka wapoteze haki ya kuwa rai wa bongo. Wakati kilasiku munawauzia passport waindi, wakenya na wanaigeria. Pumba** zenu
 
Kaeni huko huko.Kama mnataka kutuchangia fanyeni harambee kusanyeni hela mtuletee tujenge mambweni na visima huku huku.Hivi mchina akiomba uraia,mhndi naye,mmexico halafu wakigombea uongozi hapa mchina akawa rais,mmexico PM NA KANJIBAH SPIKA ITAKUAJE

Waindi na wachina passport ya bongo wanainunua kama karanga mataani. Na wakisha maliza kuiibia bongo kurudi kwa hawana shinda maana nchi zao zinaruhusu uraia pacha. Tatizo ni kwa wabongo masikini walio kosa nafasi za shule au kazi bongo wakaamua kwenda nje kutafuta elimu na kazi. Alafu munawaazibu kwa kutowa haki ya kuendelea kuwa wabongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…