Chuki dhidi ya Bikira Maria inawapofusha Wasabato na kudai Mwanamke wa Ufunuo anasimama badala ya Kanisa lao

Tatizo binadamu huwa mnasifia mpaka mnakufuru,ni kweli bikira maria ni kati ya wanawake wema kabisa na ni miongoni mwa wanawake watano bora kabisa duniani, lakini hakuwa Mtume, wala hakuwahi kufanya miujiza, na alipokufa alizikwa kama binadamu wengine
Unahakika alikufa na kuzikwa kama binadamu wengine?
 
Hii ndo maana Waislam wanakataa Yesu sio Mungu wala si Mwana wa Mungu sababu Wakristu wamekomalia Yesu ana Mama ambae ni Maria na Wanamwabudu sasa Mungu kazaliwa au Mungu ana Mke?
Yesu hakuwah kumwita Maria mama na Anakataa hana Mama wala ndugu. Kumbuka alipoambiwa Mama na ndugu zako wanakusubir huku nje skiwa ibadan aliwajibuje wajumbe?
Hana Mama sasa alizaliwa na nani hasa?
 
Kwenye haya man made churches ambayo na Mimi nipo huku, Huwa nahisi kupigwa utakaposomwa mstari wa bible na mchunhaji akasema
"Hawa wanaotajwa hapa ndiyo kanisa letu"
" Kanisa letu lilitabiriwa hapa"


Ngumu Sana kuamini maana kanisa lingine nao wanatafuta mistari wao wanasema nao walitabiriwa

Vurugu tupu
 
Bikra Maria alipalizwa mbinguni mwili na roho ! Yu hai na hakufa
Hii ni kwa mujibu wa imani ya wakatoliki na aliwatokea watoto wa Fatma Lusia, Fransisca na Yasintha mara saba kwa nyakati tofauti
Wapi walipoandika katika biblia
 
Jana nilikomenti nikafuta.
Leo naweka msingi

A. Ukitaka kujua hicho kitabu cha ufunuo ni lazima uchague
1. Uelewe kuwa kitabu kimetumia lugha za picha (symbols) ambazo si vitu uhalisia.
Au
2. Uchukue vitu vilivyotajwa katika uhalisia wake.
Mfano
(a) Mwanamke ni mwanamke kweli?
(b) Nyoka ni nyoka kweli?
(c) . Nyota , mwezi ni vitu halisi?

Jambo lingine.
B. Acha biblia ijitafasriye yenyewe.
Yaani ukisema Mwanamke ni Kanisa tutataka uthibitishe kwa kutumia biblia hiyo hiyo si akili au mawazo yako. Na ikiwa utasema Mwanamke ni Bikra Maria tibitisha kwa Maandiko..

C. Angalia sifa za huyo mwanamke kama anazo Bikra Maria au zipo kwa Kanisa.
Mfano f5 na f6. Yanasema
(f)5. Mtoto akanyakuliwa kwa Mungu
(f6) Mwanamke akakimbia nyikani na kutunzwa kwa siku 1260.
Swali je ni Bikra Maria ana sifa hizi au Kanisa?


Asanteni. Wana wa Mungu
 
Back
Top Bottom