Chuki dhidi ya Bikira Maria inawapofusha Wasabato na kudai Mwanamke wa Ufunuo anasimama badala ya Kanisa lao

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,706
Wadau hamjamboni nyote?

Nimerudi kwenu Wakuu

Iko namna hii,

Inajua kwanini Wasabato wanadai y Mwanamke anayetajwa kwenye Ufunuo 12 anasimama badala ya Kanisa lao la Waadventista Wasabato (SDA)?

Ipo sababu kubwa ya msingi ya chuki hiyo dhidi ya Bikira Maria aliye Mama wa Bwana wetu Yesu Kristo

Ndiyo Msabato mueleze chochote atakuelewa ila usithubutu kumpa sifa yeyote Bikira Maria nakuthibitishia ndugu yangu mtagombana

Chuki hiyo inawapofusha wengi wao na kuamua kutafsiri kwa njia potofu fungu hilo ambalo liko wazi kabisa na wala halihitaji kufunga siku arobaini Ili kulielewa.

Kwao Bikira Maria hana thamani zaidi ya kumfananisha na Bahasha ambayo kawaida ikitumiwa hutupwa jalalani

Tukirudi kwenye mada hebu waulize kuwa kama kweli huyo mwanamke ni Kanisa je Mtoto aliyezaliwa ni nani?? Baadhi yao watakujibu kuwa huyo Mtoto ni Yesu Kristo!

Waulize tena pia kipi kilitangulia kati ya Kanisa na huyo Mtoto?

Yaani Mwanamke ni Kanisa lakini Mtoto aliyezaliwa ni Yesu Kristo!! Ajabu kubwa kabisa

Karibuni tujadili kwa heshima na staha

Jumapili njema

UFUNUO 12

12:1 Kisha ishara kubwa ikaonekana mbinguni. Palikuwa hapo mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!

2 Alikuwa mja mzito, na akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto.

3 Ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka kubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji.

4 Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimama mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa.

5 Kisha mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi

800px-Woman_Apocalypse_Hungary.jpg
 
Huu Mstari wanatamani ufutike kwenye Biblia lakini ndio ushakua hivyo tena:

Lk 1:46-50 SUV​

Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.

Tunasema Mariam Bint Yoakimu Mungu alimtakatifunza na kumfanya Mama wa Kristo kwa sababu: hebu soma na Mimi hapa maneno ya Elisabeti alipokua mjamzito wa Yohana Mbatizaji:
Luka 1:

Lk 1

SUV

https://www.bible.com/sw/bible/164/LUK.2.SUV

LK 1​

1Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, 2kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, 4upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
Kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji Kwatabiriwa
5 Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti. 6Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. 7Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana.
8Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, 9kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba. 10Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. 11Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. 12Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. 13Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. 14Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. 15Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. 16Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. 17Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa. 18Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi. 19Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. 20Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake.
21Na wale watu walikuwa wakimngojea Zakaria, wakastaajabia kukawia kwake mle hekaluni. 22Alipotoka hali hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu. 23Ikawa siku za huduma yake zilipokuwa zimetimia akaenda nyumbani kwake. 24Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, akisema, 25Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.
Kuzaliwa kwa Yesu Kwatabiriwa
26Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. 28Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. 29Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? 30Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. 32Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Nimerudi kwenu Wakuu

Iko namna hii,

Inajua kwanini Wasabato wanadai y Mwanamke anayetajwa kwenye Ufunuo 12 anasimama badala ya Kanisa lao la Waadventista Wasabato (SDA)?

Ipo sababu kubwa ya Msingi, Chuki dhidi ya Bikira Maria aliye Mama wa Bwana wetu Yesu Kristo

Ndiyo Msabato mueleze chochote atakuelewa ila usithubutu kumpa sifa yeyote Bikira Maria nakuthibitishia ndugu yangu mtagombana

Chuki hiyo inawapofusha wengi wao na kuamua kutafsiri fungu hilo ambalo liko wazi kabisa na wala halihitaji kufunga Ili kulielewa.

Kwao Bikira Maria hana thamani zaidi ya kumfananisha na Bahasha ambayo ikitumiwa hutupwa jalalani

Hata hivyo waulize kuwa kama huyo mwanamke ni Kanisa je huyo Mtoto aliyemzaa ni nani?? Baadhi Yao watakujibu kuwa huyo Mtoto ni Yesu Kristo!

Waulize tena pia kipi kilitangulia kati ya Kanisa na huyo Mtoto?

Karibuni tujadili kwa heshima na staha

Jumapili njema

UFUNUO 12

12:1 Kisha ishara kubwa ikaonekana mbinguni. Palikuwa hapo mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!

2 Alikuwa mja mzito, na akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto.

3 Ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka kubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji.

4 Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimama mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa.

5 Kisha mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi

View attachment 2530598
Maria yupi huyo tena?
Na kwa nini umpe sifa mwanamke mwingine za kumzidi mama yako?
Huyo Maria ndo nani?
Au yule ambaye ile riwaya ya Wazungu inasema mtoto wake alikuwa na nguvu kumzidi?
 
Huu Mstari wanatamani ufutike kwenye Biblia lakini ndio ushakua hivyo tena:

Lk 1:46-50 SUV​

Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.
Hakika amebarikiwa kuliko wanawake wote na mzao wa tumbo lake amebarikiwa.

Unawezaje ukamchukia mama yake mtu alafu ukasema unampenda huyo mtu, huo ni unafki wa kiwango cha SGR
 
Hivi kwani Maria pamoja na kumzaa Yesu, bado akalala na Yusuph wakazaa watoto wengine ambao ni wadogo zake Yesu. Bado mpaka leo anatambulika kama bikira?
Naomba kueleweshwa wadau
Kwa mujibu wa imani ya wakatoliki Maria hakuzaa tena na wala hakujamiiana na Yosefu! Kwa hiyo baada ya Maria kumzaa yesu hakuzaa tena na alibaki na bikra yake ! Maana kama Mimba iliingia kwa uwezo wa roho mtakatifu maana bikra haikuondolewa na pia wakati wa kuzaa ikuwa ni kwa uwezo wa roho mtakatifu hivyo maria ni Bikra daima! Haya mambo huwezi kuyajua kama huna imani !
 
Mimba ni nini? Imani ni nn? Utofauti wa utungaji wa mimba kiimani na hizi mimba tunazozijua ni upi?
 
Mimba iliingia kwa uwezo wa roho mtakatifu haikutungwa kwa mwanamke kuingiliwa na mwanaume! Malaika Gabriel alimtokea Maria na kumtia Moyo sasa ww unaiona hiyo mimba ilikuwa ni ya kawida?
Uwezo wa binadamu kutungisha mimba ni kujamiiana, manii na yai zinatungisha mimba. Uwezo wa roho mtakatifu kutungisha mimba ni kufanya nini? Ni nn na nn vinasababisha utungwaji wa hiyo mimba? Yai la maria lilihusika?
Tunaposema mimba ilitungwa kwa uwezo wa roho tunamaanisha nini?
Basi hapa utaogopa hata kufikiri majibu sababu utachomwa moto siku ya mwisho. Ni kama vile tumewekewa ukomo wa kufikiri na unapojaribu kuuvuka huo ukomo unaambiwa kuna adhabu ya moto wa milele.
 
Hivi kwani Maria pamoja na kumzaa Yesu, bado akalala na Yusuph wakazaa watoto wengine ambao ni wadogo zake Yesu. Bado mpaka leo anatambulika kama bikira?
Naomba kueleweshwa wadau
Kwa hili kunywa k vant itakueleweshaa tu boss
 
Back
Top Bottom