Christmas Uchagani: Wachaga wako overrated!

Suala la mtu kwenda kwao ni suala la kujivunia sasa mwandishi Kama kabila haliendi kwao wewe unawashwawashwa Nini na kabila la wenzako???eti ulienda kufanya uchunguzi umelipwa nini au Nani kakulipa.naona watz kwasasa hatuna kazi zd ya umbea
 
Suala la mtu kwenda kwao ni suala la kujivunia sasa mwandishi Kama kabila haliendi kwao wewe unawashwawashwa Nini na kabila la wenzako???eti ulienda kufanya uchunguzi umelipwa nini au Nani kakulipa.naona watz kwasasa hatuna kazi zd ya umbea
Mimi nimekuja kujifunza huku Kilimanjaro. Zaidi nimeshare ripoti ya kile nilichokiona.
 
Kote kapitishwa road ndugu yangu. Nimempa offer nimtembeze kwetu na mbuzi tutamchinjia kabisa kama kumkaribisha mgeni. Halafu niambie mtu utaenjoy vipi sikukuu ambayo si Imani yako? Huyu mpemba sijui mngazija atafurahia vipi sikukuu ambayo si yake maana naamini ni muislamu?

Pili... kule watu wote wanajuana ndo maana wanaijua na kuifuragia hiyo sikukuu... yeye anapita barabarani huko hakuna anayejuana nae atasemaje sikukuu ikonove rated?

And actually mwaka huu majority hatujaenda. Hawajui kama sisi ni kabila la 2 kwa ukubwa Tz? Hatuwezi enda wote. Hatujaenda kwa kukosa nauli bali mambo yamekua mengi. Nafasi kwa ufinyu wake
Ndugu nimesome upya.
Kipi nimesema uongo?
Kipi unakipinga?
 
Mkuu.. mleta hoja naomba nikusahihishe juu ya research yako..

Kwanza kumbe wewe ulikua unapita main road tuu unaambiwa hapa ni kibosho, hapa rombo, hapa mwika, hapa uru etc. Ndo research zinavyoenda? Nilidhani umepata mialiko kwa familia kadhaa za huko hivyo ukazungukia mitaa hiyo yote ndani. Kumbe unapita road tu?

Pili, naomba nikuambie, Christmas siyo bar kule uchahhani. Christmas ni majumbani. Siyo barabarani. Christmas watu wakitoka makanisani hienda kusherehekea majumbani ndugu yangu. Hujikusanya kwa mojawapo ya familia either ndo zamu ya kusherehekea ama ambaye pochi ni nene zaidi ya wengine. Hamuwezi kulingana kiuchumi.

Christmas kwetu ni excitement kwakua watu tunaenda kukutana na familia. Unagikiria Macha hatujaonana mudaaaa unakua excited kumwona na kumsikia anakuja na lipi. Ni mojawapo na nafasi ya kupata challenges. Kama kwetu endapo mtu ameanguka kiuchumi kidogo wengine humchangia.

Kuhusu kujengeka tuache masikhara. Vijijini kumejengeka. Kumejengeka mno. Nikuhakikishie kijiji chetu hakuna nyumba ya udongo. Na kumejengeka toka 80's huko ijapokua tumekuja kuboresha zaidi.

Kwa hayo machache, niombe nikukaribishe this coming Christmas endapo mola atatupa nafasi tena. Nitakualika hakika na nitakuzungusha jimbo langu na utakuja badili huu uzi. Nikuahidi hilo.
Nimekuja uchagani kujifunza, sikuja kufanya research. Nilichoandika ni kile nilichokiona (observation), na mwanaJF yoyote anaweza naye kuja huku uchagani akatupa observation yake.

Kote huko nilikokutaja nilifika kwa barabara kuu, nikaingia ndani ya vijiji kadhaa na kukutana na watu mbalimbali katika maboma yao. Sijafika kila mahali na sikuwa na mpango wa kufika kila mahali.
 
Nimekuja uchagani kujifunza, sikuja kufanya research. Nilichoandika ni kile nilichokiona (observation), na mwanaJF yoyote anaweza naye kuja huku uchagani akatupa observation yake.

Kote huko nilikokutaja nilifika kwa barabara kuu, nikaingia ndani ya vijiji kadhaa na kukutana na watu mbalimbali katika maboma yao. Sijafika kila mahali na sikuwa na mpango wa kufika kila mahali.
Mkuu unazidi kuongopa. Hukusema umepitia kwenye maboma. Ulikua wapita tu. Na kusema sijui unepitia vijijjni ndo uongo zaidi. Mwenyeji wako tu mitaa mingine alikua anachanganya sembuse vijijini kwa wengine? Na kama mwenyeji wako ni mmachame unategemea ndo akutembeze kibosho vyema, rombo ama uru etc?

Wewe bwana hapa umeamua tu kutuingopea. Na sikukuu kama si yako hiyo hype utaipataje? Ni kama mimi niiongelee idd halaf niende na mwenyeji huko Masama wakati sijui mtu na napita barabarani. Ama labda utuambie wewe ulitaka Sikukuu iweje? Ulitaka ile hype ya Idd ndo uisikie kwenye Christmas na si Imani yako na ulikoenda si kwako? Halaf unajua weakness za observation method?
 
Na siyo kweli kwamba tangu tarehe 18 magar ya kwenda uchagani yamejaa, usafiri upo kama kawaida
Upo dunia ya ngapi? Magari yapo full Hadi wametoa vibali vya dharura kwa mabasi mengine kwenda UCHAGANI
Hapana chezea mangis wewe
 
Na siyo kweli kwamba tangu tarehe 18 magar ya kwenda uchagani yamejaa, usafiri upo kama kawaida
Upo dunia ya ngapi? Magari yapo full Hadi wametoa vibali vya dharura kwa mabasi mengine kwenda UCHAGANI
Hapana chezea mangis wewe
 
Mwaka huu niliamua kufanya tour trip huko Kilimanjaro ili kujifunza na kujionea shamrashamra za Wachaga wakisheherekea sikukuu ya Christmas.

Mpaka sasa bado nipo Uchagani.

Nimefanikiwa kufika maeneo ya Rombo, Mwika, Marangu, Old Moshi, Kibosho na Machame. Sijafanikiwa kufika maeneo ya Kirua Vunjo na Uru. Kuna mambo mazuri sana na mabaya machache niliweza kuyaona, kwa mada hii leo hapa sitayazungumzia mabaya wala mazuri (nitakuja na mada yake baadaye nikikamilisha ziara yangu), bali nitazungumzia baadhi ya mambo yaliyokuzwa kuliko uhalisia wake.

1. Sio kweli kuwa karibu kila Mchaga hurejea kwao kipindi hiki cha Kristmas. Ukweli ni kwamba idadi ya Wachaga wanaorejea makwao kipindi hiki huenda haifiki hata robo katika Miji (namaanisha Boma la Ukoo lenye muunganiko wa familia kadhaa zenye kushare wazazi) niliyoweza kuipitia, zaidi ya 80% ya wauhusika hawakurudi kwao. Kuna maboma kadhaa yalikuwa yamefungwa kabisa, hakuna aliyerejea kabisa!

2. Sio kweli kuwa kila jamii ya Kichaga kipindi hiki huweza kusheherekea Christmass kwa shamrashamra. Nimeweza kukutana na familia za Wachaga Waislamu (hasa maeneo ya Machame na Kibosho), jamii zingine maskini sana na familia nyingi zisizoeleweka nk, hao hawana muda wowote na sherehe za Krismasi. Wako busy na maisha yao mengine.

3. Misafara mingi ya magari binafsi yaliyokuwa yakielekea uchagani yalikuwa ni magari ya familia chache zenye uwezo mkubwa kifedha au maisha ya mbwembwe. Kifupi sana, magari yale huenda yanaakisi 10% tu ya familia za Kichaga. Wengi wa wachaga wamekuja kula sikukuu kwa kutumia usafiri wa umma bila kujali kama wanamiliki magari mijini au hawana kabisa magari.

4. Sehemu kubwa ya miji (maboma) zimejengwa kwa nyumba za kawaida kabisa na nyingine ziko kizamani japokuwa zinaonekana kutunzwa vyema. Zaidi ya 90% sio nyumba za gharama kubwa au kisasa. Pia niliweza kukutana na nyumba duni au mapagala yanayoonekana kutelekezwa lakini nikakuta kuna watu wanakaa!
Pamoja na ukweli huo, huwezi fananisha standard ya makazi na ukanda wa kusini Lindi na mtwara.
 
Back
Top Bottom