Christmas Uchagani: Wachaga wako overrated!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,106
35,042
Mwaka huu niliamua kufanya tour trip huko Kilimanjaro ili kujifunza na kujionea shamrashamra za Wachaga wakisheherekea sikukuu ya Christmas.

Mpaka sasa bado nipo Uchagani.

Nimefanikiwa kufika maeneo ya Rombo, Mwika, Marangu, Old Moshi, Kibosho na Machame. Sijafanikiwa kufika maeneo ya Kirua Vunjo na Uru. Kuna mambo mazuri sana na mabaya machache niliweza kuyaona, kwa mada hii leo hapa sitayazungumzia mabaya wala mazuri (nitakuja na mada yake baadaye nikikamilisha ziara yangu), bali nitazungumzia baadhi ya mambo yaliyokuzwa kuliko uhalisia wake.

1. Sio kweli kuwa karibu kila Mchaga hurejea kwao kipindi hiki cha Kristmas. Ukweli ni kwamba idadi ya Wachaga wanaorejea makwao kipindi hiki huenda haifiki hata robo katika Miji (namaanisha Boma la Ukoo lenye muunganiko wa familia kadhaa zenye kushare wazazi) niliyoweza kuipitia, zaidi ya 80% ya wauhusika hawakurudi kwao. Kuna maboma kadhaa yalikuwa yamefungwa kabisa, hakuna aliyerejea kabisa!

2. Sio kweli kuwa kila jamii ya Kichaga kipindi hiki huweza kusheherekea Christmass kwa shamrashamra. Nimeweza kukutana na familia za Wachaga Waislamu (hasa maeneo ya Machame na Kibosho), jamii zingine maskini sana na familia nyingi zisizoeleweka nk, hao hawana muda wowote na sherehe za Krismasi. Wako busy na maisha yao mengine.

3. Misafara mingi ya magari binafsi yaliyokuwa yakielekea uchagani yalikuwa ni magari ya familia chache zenye uwezo mkubwa kifedha au maisha ya mbwembwe. Kifupi sana, magari yale huenda yanaakisi 10% tu ya familia za Kichaga. Wengi wa wachaga wamekuja kula sikukuu kwa kutumia usafiri wa umma bila kujali kama wanamiliki magari mijini au hawana kabisa magari.

4. Sehemu kubwa ya miji (maboma) zimejengwa kwa nyumba za kawaida kabisa na nyingine ziko kizamani japokuwa zinaonekana kutunzwa vyema. Zaidi ya 90% sio nyumba za gharama kubwa au kisasa. Pia niliweza kukutana na nyumba duni au mapagala yanayoonekana kutelekezwa lakini nikakuta kuna watu wanakaa!
 
Umeeleze very general things. Nyumba za zamani zipo. Wachaga si malaika kwamba kila mahali wana nyumba nzuri.

Kuja public transport ni kitu kimekuwa kikifanyika miaka na miaka. Kuja Private cars zimeanza miaka si mingi.
Kama ilivyo sehem nyingine. Si wote wanaweza kuja.. itategemea hao wengine wana majukumu gani.

Either wanaweza wasije hii sikuu.. wakaja siku zingine.

So sioni point ya kuwa overrated hapo. Ni issues za kawaida mabazo wenyeji wanazijua.
 
Kweli vyasaka mmeamua kutuandama mwaka huu. Huu ni uzi wa 5 juu ya utamaduni wa kwenda nyumbani mwisho wa mwaka.

Nadhani badala ya kutuponda muige mambo mazuri kutoka kwa wachaga, kusalimia Ndg jamaa na marafiki angalao Mara moja kwa mwaka ni jambo jema.
 
Back
Top Bottom