Chozi la Kabwe kwa Makonda limekoma


Hata kama Kabwe alikuwa na makosa ya kiutendaji, siyo taratibu kuripoti makosa ya mfanyakazi kwenye mikutano ya hadhara na kwa staili ya usabiki kama ilivyofanyika. Taratibu za utumishi zipo wazi na lazima zifuatwe ili kulinda haki za waajiri na waajiriwa
 
Asante sana mkuu na mimi ndio nisemacho lakini vijana wa Lumumba ni povu tu 24 hrs
 
Mwanahabari siku zote uwe unakumbuka threads zako zote unazozileta humu JF ili zisomwe na wanajukwaa. Ninakwambia hivyo kwa sababu moja tu, weka kumbukumbu ya kila unachoandika, na kwa faida ya heshima yako, hakikisha unakuwepo mtiririko wa mawazo yako, ili heshima yako iendelee kuwepo.

Mara tu baada ya Rais kumsimamisha kazi Marehemu Wilson Kabwe, Mwanahabari uliweka uzi wenye kumuunga mkono Makonda. Ukaandika kwa kirefu juu ya kitendo cha serikali kuokoa fedha nyingi. Baada ya wiki chache kupita, na baada ya Wilson Kabwe kufariki dunia wewe huyo huyo Mwanahabari unaleta uzi ambao una ujumbe tofauti kabisa na ule wa mwanzo.

Maishani mwako simamia kitu kimoja, usiwe kama kinyonga anayeweza kubadilika kutokana na mazingira yanayomzunguka. Kumbuka kwamba threads zako zinasomwa na watu wenye uwezo tofauti wa kuweka kumbukumbu. Simamia msimamo mmoja, kwa faida ya heshima ya uandishi wako.
 
Kula gwara mkuu..waandishi wetu kama huyu @muandishihuru ni watu wakufuata upepo hawana uwezo wa kusimika nanga kwenye hoja moja wao ni gusa hapa gusa pale ili kundi fulani lifurahi
 
Mkuu tabia ya Mwanahabari Huru ni undumi la kuwili
 
alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya ufisadi wa richmond...huo ni ushahidi tosha


Haya shime basi tumpeleke mahakamani maana miaka inaenda tu (minane sasa)n na Mungu si Athumani kuna siku ataamua kumchukua na mtakuja kummwagia sifa kibao na kusahau kuwa mlimtuhumu kwa ufisadi.
 
Mawazo ya hovyo sana haya siwezi fanya kazi kwa mawazo ya wandishi kama wewe
 
Mawazo ya hovyo sana haya siwezi fanya kazi kwa mawazo ya wandishi kama wewe
Lengo langu ujumbe ukufikie. Kukufikia wewe ujumbe naamini na waandishi wengine watajifunza kuheshimu maadili ya uandishi. Unapokuwa unatoa maoni ya aina mbili tofauti kwenye suala moja, inabidi ujenge hoja nzito sana ili yule anayesoma habari zako na kuwa influenced nazo aweze kukuelewa.
Mchezo huu hauhitaji hasira, jifunze kuwa tayari kujifunza kitu kipya kama mwandishi wa habari mwenye nia ya kufanya kazi bora zaidi katika siku zijazo.
 
Haya ni madhara ya zile division five za Dr. Kawambwa, matokeo yake Prof Ndalichako anafanya kazi nzito ya kurudisha heshima ya elimu.

Mimi siyo wale saizi yako ambao nimakanjanja naona hoja imekushinda umekua kioja
 
Mimi siyo wale saizi yako ambao nimakanjanja naona hoja imekushinda umekua kioja
Kuna mdau kakushauri uachane na undumila kuwili kwenye uandishi wako. Hilo ni jambo muhimu kwako. Huwezi wewe huyo huyo ukamsifia Makonda kwa uamuzi wake, halafu haipiti hata miezi miwili unarudi JF na kuandika kitu tofauti kabisa na thread yako ya awali. Ujumbe unakufikia wewe na wengine wenye uandishi wa kishabiki unaosahau hata misingi ya kazi yenyewe.
 
Hapa jukwaani kuna elimu nyingi sana hutolewa zihusuzo mambo ysiyoonekana lakini ambayo ni dhahiri. hata angekuwa na roho ngumu kiasi gani , makonda anajihisi vibaya, tena anahisi kama sio yeye kifo kisingetokea. Mbaya zaidi, alivyojipambanua na viongozi wa dini wakimwekea mikono ya baraka kumbe ni unafiki mtupu. Katika maisha yake hili halitoisha wala kusahaulika. N aiwapo kuna lingine kama hilo basi hawezi kuwa salama tena kiroho.
 
tatizo halikuwa uwaziri mkuu..tatizo lilikuwa ni richmond...lowasa alishiriki mkataba wa richmond 100%

100% kwa kupewa maagizo na mkulu wake. Kama ni mawazo yangu nitalaumu au kujiuliza tu kuwa, kwa nini Lowasa hakujiuzulu alipoona mashinikizo yanazidi? Yaani naona angekataa na hata na iende mbali zaidi kujiuzulu kwa shinikizo hilo
 
Wewe ndio mkurupukaji badala yakujibu hoja umeanza kunishambulia lakini pole wenzako walijaribu wakashindwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…