Choo cha Kisasa cha Kukalia na Karaha /Adha zake kwa Jamii ya Kitanzania.

Hivyo vyo niling'oa home, kwenye master nikaweka cha kuchutama japo wife alinuna. Havina raha yoyote ile. Yaani kujitawaza unatumia nususaa, gogo hali ishi unakuwa umejibana husipo kuwa makini una toka mikono ina nuka mavi mpaka unajishitukia. Natena ukienda kukata gogo unasaula kila kitu.
Hahaha hahah
 
Mimi nikiingia toilet nikakutanana aina hii haja huwa inakata kabisa, labda nikojoe tu!
Habari za msimu wa siku kuu.

Choo cha kisasa cha kukalia ni dizaini ya choo chenye sink ya kukalia na kwa asilimia kubwa kilichotengenezwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu au wenye matatizo ya miguu na kiafya kwa ujumla ikiwemo na wazee tofauti na kile cha kawaida cha kuchuchumaa.

Kwa hali isiyo ya kawaida,choo hiki kimekuwa kimekiwa kikipendelewa sana kuwekwa majumbani tena majumba ya kifahari, na nyumba za kawaida, kwenye mahoteli, na sehemu nyingi za public na private nyeti kwa matumizi ya wote.

Sehemu nyingine huwa kunakuwa na vyoo viwili yaani milango miwili ya choo. Kimoja cha kuchuchumaa kwa maana kwa watu wasio na ulemavu , wazee, ama wenye matatizo ya kiafya na chumba kingine cha choo chenye hiyo choo/sink ya kukalia kwa ajili ya watu wa category tajwa hapo mwanzo.

Kwa hali isiyo ya kawaida, kumekuwa na wimbi kubwa la watu kupendelea kutengeneza choo cha kulalia kuliko kile cha kuchuchumaa.

Hapa chini nimekuwekea Karaha zake kwa indinkibwa la watu hasa watanzania. Na kuichukulia kuwa si mazoea yetu na hatujazoea kujisaidia tukiwa tumekaa!

Kiukweli kuna taabu tena taabu sana kutumia choo cha dizaini hii. Yaani muundo huu wa Choo unatushinda wstu tulio wengi tena sana kutumia. Mara uingiapo chooni na kukuta huu muundo wa choo amani hukosekana.

Ni kweli kuna raha au starehe yake wakati wa kupush gogo kwa maana ya mkao mzuri wa starehe, ila taabu na Karaha huja wakati wa Kujichamba aka kujitawaza, Aiseee!! Nishidaaaa!!

Japo kuwa kuna huo mpira wa kujisafishia, watu hatujaweza kuutumia maana huishia kujilowanisha nguo hasa suruali au skirt kwa upande wa makalioni na mbele kwa mapaja.

Yaani ukijaribu Kujichamba kwa kuupitisha kwa nyuma au mbele taabu tubu. Lazima ujilowanishe nguo hata kama suruali ama nguo umeishusha na kupunguza presha ya maji ya mpira kadri niwezavyo.

Mara nyingi watu huepuka aibu ya mlowano wa nguo kwa kupendelea kutumia TISHU ambazo huwa pale , ILA SASA SI VYOO VYOTE UTAINGIA NA KUKUTA KUNA TISHU! Utakuta zimeisha au hakuna kabisa na mtu umebanwa!

Wadau, Mwenye utaalamu wa matumizi ya hii sampuli ya choo bila Karaha hizo tajwa hapo juu atujuze.

Merry Xmas and Happy New Year 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raha yake kiwe kisafi
Cha watumiaji wachache
Pawe na maji
Pawe na tissue
Pawe na seat sanitizer

kwa umma bora cha kuchuchumaa kwa kweli
Ni rahisi kusafisha pia

ukikikuta hiki public ni mtihani..mara chache sana ni kisafi
huwa najisaidia km ng'ombe siwezi kukaa
 
Choo cha kiboya sana hicho hasa kwa extended family Afrika ama public!

Hivyo vyo niling'oa home, kwenye master nikaweka cha kuchutama japo wife alinuna. Havina raha yoyote ile. Yaani kujitawaza unatumia nususaa, gogo hali ishi unakuwa umejibana husipo kuwa makini una toka mikono ina nuka mavi mpaka unajishitukia. Natena ukienda kukata gogo unasaula kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi huwa na wasiwasi kwamba makalio yaliyonitangulia yalikuwa na vidonda? Majipu? Halafu ukifyatua mzigo maji ya chooni yanaruka juu mpaka kwenye kifyatulio. Mi huwa nasimama juu kwenye round na kuchuchumaa ili kukwepa mauzauza.
Ukisimama ndo mruko wa maji unaingia mpaka kwenye div
 
Wewe hujui raha ya choo cha kukaa. Me nikiingiaga chooni natamani nisitoke hasa pale wakati wa kunawa yale maji yanayotoka kwa kile kibomba cha kujisafisha yanakuwa kama yanatekenya mpk raha unatamani usitoke 😂 mimi ndio maana nikiingia chooni sitoki haraka. Hata kama nikiwa Sina choo nakaa tu halafu nafungulia maji 😂
download.jpeg
 
Back
Top Bottom