Choo cha Kisasa cha Kukalia na Karaha /Adha zake kwa Jamii ya Kitanzania.

hivi vyoo hapana kwakweli ukizingatia asili yetu sisi hua tunaishi watu wengi kwa pamoja nyumbani ni ngumu sana kutunza na kuhakikisha usafi.
 
Kuna nyumba ya jirani mafuriko mafuriko yaliingia kwenye lile shimo la mavitaka nje, wenye nyumba wakashangaa nyumba nzima inanuka mavi, kuja kuangalia kumbe Shimo nje lilijaa likawa linarudisha mavi ndani. Watu waliikimbia nyumba asee.
Choo bovu sana hili linatia kinyaa mno!

Ni bora kuchuchumaa porini kuliko kukalia hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raha yake kiwe kisafi
Cha watumiaji wachache
Pawe na maji
Pawe na tissue
Pawe na seat sanitizer

kwa umma bora cha kuchuchumaa kwa kweli
Ni rahisi kusafisha pia

ukikikuta hiki public ni mtihani..mara chache sana ni kisafi
huwa najisaidia km ng'ombe siwezi kukaa


Sent using mazonge yamezidi
 
Kuna mtu milimvunjikia kwa kupanda na kuchuchumaa, nyama yote ya kwenye paja ilichimbwa na kutoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli bhana lile dubwasha likivunjika halafu likukate huwa linakata kweli si masikhara.

Mimi siku hizi hata nikitaka chumba gesti sharti langu kubwa sitaki choo cha kukaa basi wahudumu nikiwapigia simu tu wanacheka kwanza wanasema aaaah kumbe wewe?

Sent using mazonge yamezidi
 
Mi huwa na wasiwasi kwamba makalio yaliyonitangulia yalikuwa na vidonda? Majipu? Halafu ukifyatua mzigo maji ya chooni yanaruka juu mpaka kwenye kifyatulio. Mi huwa nasimama juu kwenye round na kuchuchumaa ili kukwepa mauzauza.
Mkuu ma-ceramic yale siyo imara sana kuyabebesha uzito mkuwa kwa style ya kulipandia juu mazima. Kuna siku litakupasukia. Ila hizo changamoto ulizoelezea ni za kweli na zinatupata wengi.
 
Habari za msimu wa siku kuu.

Choo cha kisasa cha kukalia ni dizaini ya choo chenye sink ya kukalia na kwa asilimia kubwa kilichotengenezwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu au wenye matatizo ya miguu na kiafya kwa ujumla ikiwemo na wazee tofauti na kile cha kawaida cha kuchuchumaa.

Kwa hali isiyo ya kawaida,choo hiki kimekuwa kimekiwa kikipendelewa sana kuwekwa majumbani tena majumba ya kifahari, na nyumba za kawaida, kwenye mahoteli, na sehemu nyingi za public na private nyeti kwa matumizi ya wote.

Sehemu nyingine huwa kunakuwa na vyoo viwili yaani milango miwili ya choo. Kimoja cha kuchuchumaa kwa maana kwa watu wasio na ulemavu , wazee, ama wenye matatizo ya kiafya na chumba kingine cha choo chenye hiyo choo/sink ya kukalia kwa ajili ya watu wa category tajwa hapo mwanzo.

Kwa hali isiyo ya kawaida, kumekuwa na wimbi kubwa la watu kupendelea kutengeneza choo cha kulalia kuliko kile cha kuchuchumaa.

Hapa chini nimekuwekea Karaha zake kwa indinkibwa la watu hasa watanzania. Na kuichukulia kuwa si mazoea yetu na hatujazoea kujisaidia tukiwa tumekaa!

Kiukweli kuna taabu tena taabu sana kutumia choo cha dizaini hii. Yaani muundo huu wa Choo unatushinda wstu tulio wengi tena sana kutumia. Mara uingiapo chooni na kukuta huu muundo wa choo amani hukosekana.

Ni kweli kuna raha au starehe yake wakati wa kupush gogo kwa maana ya mkao mzuri wa starehe, ila taabu na Karaha huja wakati wa Kujichamba aka kujitawaza, Aiseee!! Nishidaaaa!!

Japo kuwa kuna huo mpira wa kujisafishia, watu hatujaweza kuutumia maana huishia kujilowanisha nguo hasa suruali au skirt kwa upande wa makalioni na mbele kwa mapaja.

Yaani ukijaribu Kujichamba kwa kuupitisha kwa nyuma au mbele taabu tubu. Lazima ujilowanishe nguo hata kama suruali ama nguo umeishusha na kupunguza presha ya maji ya mpira kadri niwezavyo.

Mara nyingi watu huepuka aibu ya mlowano wa nguo kwa kupendelea kutumia TISHU ambazo huwa pale , ILA SASA SI VYOO VYOTE UTAINGIA NA KUKUTA KUNA TISHU! Utakuta zimeisha au hakuna kabisa na mtu umebanwa!

Wadau, Mwenye utaalamu wa matumizi ya hii sampuli ya choo bila Karaha hizo tajwa hapo juu atujuze.

Merry Xmas and Happy New Year 2020
Niwe mkweli choo cha namna hii ni hatari mno kwa matumizi ya public. Nakumbuka nilienda wilaya ya kwimba kikazi,aisee kuna lodge moja pale sitaitaja niliambiwa nzuri mno,kweli ndani kuko flesh,kitanda safi,kasheshe ikaja usiku ule nataka kushusha mambo ebhanaee kuingia toilet choo cha kukaa afu kichafu balaa.Niliishiwa pozi,kiukweli nilichokifanya nilitoka nje kuuliza kama kuna toilet za nje nikaambiwa hakuna,nikarudi room nikapiga hesabu nilichoamua Nikupanda pale juu nikakanyaga nikafanya yangu.KWA HILI NIWAPONGEZE Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro pamoja na kuwa na toilets za kukaa lakini usafi wa pale huwa sijuti kwenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm kwa uelewa wangu mdogo naona kama kuna vitu tunaiga hata visivyoo faa kuigwa,jamii ya watu weupe (wazungu) vyakula vyao wanavyokula ni laini laini,hivyo hata wanapokwenda chooni hutoa choo laini,,sasa kwa jamii yetu afrika vyakula ni ugali mtama,ugali dona,ugali muhogo na wali kidigo,magimbi, mihogo,hapo ukienda kutoa mzigo ni kama tofari lililorushwa kwenye dimbwi la maji,utasikia pwaaaaa na mpaka liyayuke mpaka lichokonolewe na ndio hupelekea kuziba vyoo hivi vya kisasa,,jamani yetu mashimo mzigo ukifika chini unasikia sauti tiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom