Nitasema kweli daima,fitina kwangu mwiko. Na nitajielimisha kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu hiyo kwa manufaa yangu na wenzangu.
Hizi ni tu ya ahadi za kila mwana ccm mwenye kufuata itikadi na misingi ya cChama Cha Mapinduzi ambacho kwa sasa ndugu Daniel Chongolo ndiye katibu wake mkuu.
Ndugu Chongolo hivi karibuni alitoa ushauri wake kwa vijana wasomi wa kitanzania ambao wanasubiri ajira serikalini. Chongolo akiwa kama sehemu ya watunga ilani na wasimamizi wa sera aliwaeleza wasomi ushauri wenye nia ya kuwakwamua walipokwama kwenye mtego huitwao ajira.
Badala ya kupokea na kuanza kufanyia kazi ushauri ule, Vijana wasomi wakitanzania wameubeza na kudhani kwamba Chongolo ameaonesha dharau dhidi yao, wengine wakafika mbali na kuhoji kulikuwa na haja ipi ya vyuo vikuu kuanzishwa na muda wote huo ccm ilikuwa wapi?
Vijana wenzangu kwenda Veta sio dharau, wala sio matusi, kusomea ufundi sio laana kama mlevi mmoja aliyechoka kulamba asali kimya kimya sasa akaamua kupayuka na kuwaita vijana wenzetu wa boda boda kuwa wana laana, Vijana wenzangu vichwa vyenu vijazeni maarifa badala ya ujinga na kucheua upumbavu.
Nchi yetu bado ni changa mno kiumri bado hajitoshelezi kuajiri mamia kwa mamia, kwenda shule lengo kuu ni kukuweza kuyamudu mazingira yanayokuzunguka.
Ukiona elimu uliyokuwa nayo haijakuletea tija basi jaribu nyingine ili ikufae kwa mazingira ya sasa na sio kushupaza shingo kama wale wapumbav.
Mwaka 2021 Chama Cha Mapinduzi kiliagiza Ofisi ya Waziri mkuu kuanzisha programu kabambe ya kutoa nafasi ya ufadhili ya mafunzo ya ufundi stadi(uanagenzi) kwa vijana wa kitanzania wenye umri wa miaka 15 mpaka 35 katika Vyuo vyake vya ufundi.
Mwaka 2023 tarehe 22 mwezi wa 2 ofisi hiyo imetoa tena nafasi hizo nchi nzima na mwisho wa maombi ni tarehe 10 mwezi wa 3 na kufanya program hii sasa kutimu miaka mitatu (3).
Nahitimisha kwa kusema kwamba ndugu Chongolo alizungumza huku akiwa amebeba maono na mapenzi makubwa kwa vijana wote wa kitanzania wenye ari na nia ya kuitumikia na kufaidi matunda ya nchi yao, maono ya kupambana na wale maadui watatu ambao baba wataifa Mwalimu Nyerere alituachia ambao ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.
MIMI KITILINGO RAMADHANI NAENDA VETA.
(0699826969) SARANGA, UBUNGO.