Chondechonde Maalim Seif Sharif Hamad

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Tunasikia CCM wanakutongoza ili uingie katika maridhiano na CCM , jambo hilo usjije ukalikubali hata sekunde ya sekunde, achana nalo mara moja, wamechukua serikali kwa nguvu, wameteka uchaguzi, wamepanga matokeo, wameyatangaza waliyoyapanga, leo maridhiano ya nini, kubwa lipi lililowafanya watake maridhiano, ndugu wasomaji CCM wamsehinda uchaguzi wa Zanzibar kwa kishindo , sasa haya anayoyadai CCM yanatokea wapi sababu yake nini ?

Maalim Seif kaa chonjo na mtego huu hawa wanataka kukugombanisha na umma uonekane wewe ulitakalo ni madaraka na ccm wanataka wakupe pipi ya umakamo kaambali na pipi hio hizo ni zile pipi za wataliana zilizozikigaiwa Nungwi, madhara yake sio leo leo.

Yaliyotokea Zanzibar hakuna asie yajua kuhusu yaliyofanywa hata CCM kuibuka na ushindi mnono Maalim kaa mbali na ushindi wao ukitia mguu sijui maridhiano maridhiano ulikuwa ufanyike uchaguzi huru, wameuharibu ili watafute maridhiano ya kuhalalisha haramu atakaewakubalia yupamoja nao.

Kuna clip zinaenezwa zikimsafisha mshindi wa uchaguzi haramu huo kama tuuonavyo sisi na eti yale yaliofanywa kuupata ushindi yeye hahusiki na hakupendezewa nayo na atawawajibisha waliohusika na mauaji na utesaji, tunkwambia Maalim hilo ni lake akilifanya tutaliona na tutampongeza na asipolifanya bado litabakia kuwa ni lake.

Watu kwa mamia wameuliwa Zanzibar (Unguja na Pemba) leo hii eti maalim njoo tuzungumze yaishe.
 
Hata ikibidi wazungumze basi sio lazima maalim awe VP.

Act wazalendo watafute yule wanae muona kuwa anafaa kuwa mrithi wake.

Maalim yupo 77 sasa abaki kuwa mwenyekiti wa Act kukijenga chama zaidi.

VP waitoe hio nafasi kwa Dkt Faki aliekua mgombea mweza wa Membe au Othman Masoud aliekua Mwanasheria mkuu Zanzibar.

Maalim Atumie muda huu kukijenga Act na kuwajenga kisaikolojia wazanzibari wenye imani naye miongo ya 4 kuwa Struggle bila ya yeye inawezekana zaidi
 
Maalim Seif akiingia makubaliano yoyote na CCM baada ya uharamia wote huu basi atakuwa msaliti wa Wazanzibari.

Ni sawa na mbakaji ambake mwanamke kisha baada ya hapo ajifanye anamhurumia, anamjali, kwamba eti toka zamani alikuwa akimpenda na blah blah kibao

Maalim Seif jihadhari na Masheikh na viongozi wastaafu watakaotumwa kwako kuja kukulainisha.

Hii issue is not about you Maalim, It is about the people of Zanzibar and their destiny!.

Usihalalishe haramu kuwa halali, waache CCM watawale watakavyo mpaka pale Nusra ya Allah itakapokuja!.

Yaani eti Maalim apate kura below 20% huu si uporaji ni ubakaji wa wazi wa maamuzi ya Wazanzibari!
 
Unamshauri mtu ambae hana zaidi ya miaka mitano inatakiwa awe amakufa kupisha wengine wazaliwe?

Yaani akikataa hii mitano hana kitu kingine anaweza kuifanyia Zanzibar kwa umri wake.

Mdanganye afe bila sifa yoyote.
 
Agenda tuliokuwa nayo kwa sasa ni kufuta Umoja wa kitaifa

Tukiingia Baraza la wawakilishi tuna zaidi ya theluthi mbili

Inaekwa mezani kura za Ndio nyingi tumeifuta

Hatutaki tuchanganye mchele na Pumba
Umeelewaaaa
 
Seif jana kaenda kuzitembelea nyumba za walioathirika na vile vipigo vya wanajeshi kule Pemba, na kwa aliyoyaona kule, sidhani kama ana chembe ya hilo wazo la kutafuta maridhiano na CCM kwenye akili yake, itakuwa ngumu sana.
 
Seif jana kaenda kuzitembelea nyumba za walioathirika na vile vipigo vya wanajeshi kule Pemba, na kwa aliyoyaona kule, sidhani kama ana chembe ya hilo wazo la kutafuta maridhiano na CCM kwenye akili yake, itakuwa ngumu sana.
Hii ilibidi ianzishiwe uzi mkuu, huna taarifa kamili?
 
Mtoa mada sijui kama unatambua msimamo wa Maalim Seif kuhusu CCM. Kwake yeye ni heri akae "meza moja" na CCM (kushirikiana) kuliko na msaliti Lipumba.

Maalim amekuwa akionesha msimamo huu si kwa maneno, kwa vitendo pale alipoihama CUF kwa kumkwepa msaliti na pia kufanya maridhiano na CCM yaliyopelekea kuanzisha SUK Zanzibar na CUF kubatzwa jina la CCM B na CHADEMA.
 
Viana wa vyombo vya dola kutoka Tanganyika waliokwenda huko kushiriki uharamia dhidi ya watu wa zanzibar wanasema wazi jinsi walivyokuwa wakidumbukiza kura mara nyingi nyingi kwa maslahi ya CCM, nao nafsi zinawasuta, hawana amani kabisa. Wana msongo wa mawazo, Halafu eti leo Maalim akae na maharamia!. Hiyo siyo busara.

Huku bara, mapolisi na vibegi vyao vidogodogo mgongoni walionekana wakiingia vituoni.

Huu uchaguzi siyo uchaguzi ni kama mapinduzi ya kijeshi dhidi ya wananchi!
 
Viana wa JKT kutoka Tanganyika waliokwenda huko kushiriki uharamia dhidi ya watu wa azabzibar wanasema wazi jinsi walivyokuwa wakidumbukiza kura mara nyingi nyingi kwa maslahi ya CCM, nao nafsi zinawasuta, hawana amani kabisa. Wana msongo wa mawazo, Halafu eti leo Maalim akae na maharamia!. Hiyo siyo busara
Wadogo zake Hussein Mwinyi nao wamepata ubunge. Raha ilioje kaka rais wadogo mawaziri. Maajabu ya chama cha wanyonge.
 
Mkuu nakuelewa. Wote tumeumia kwa yaliyotokea na naamini Maalim kaumia zaidi.

Tatizo la hii kadhia huoneshi road map na hatma take.

Kuna mada niliandika juzi. "Bila kurudiwa uchaguzi umuhimu wa Maalim Seif kuingia GNU in mkubwa na militia sababu zangu"

Bado naamini madhara ya Maalim Seif na ACT kuwa nje ya Serikali japo hio ya kinafiki in makubwa kuliko kuwa ndani.

Hasa ikiwa hakuna sindikizo lolote la kimataifa. Hili jambo halitaki jazba.

Somo la 2015 na kilichotokea in kubwa.

Afrika hatujawa tayari na demokrasia. Msimamo wa Maalim unajulikana kuhusu Zanzibar.

Tulipofika in kuangalia namna ya kupunguza madhara na kuweka utulivu was mapambano.

Wazanzibari wameuliwa, wamejeruhiwa wamenyanyaswa na kupotezwa who cares? Mara ngapi yamefanyika mini kimepatikana?

Mara ngapi Maalim amegoma? Miafaka mingapi imefanyika who cares?

Dalili zinaonesha Zanzibar inakwenda kumalizwa soon. Vyama Vingi vimemalizwa na natabiri vyama makini kufutwa.

Mapambano ya kuidai Zanzibar na kupatiwa haki zake ukiuwa vyama kwa sasa ni kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana.

Hapa hapataki jazba bila focus. Mini hatma ya uamuzi was kugoma kwa sasa unless kuwe na uhakika was kurejewa uchaguzi ambao sio rahisi.

Mapambano yaendelee ndani ya Serikali na nje. Hii ndio nusra ya Zanzibar kwa sasa. Huku bara hio fursa haipo.

ACT waingize watu ndani, wasindikize madai ya haki kwa waliodhulumiwa, waimarishe harakati nje na kupigania demokrasia kimataifa ili huko mbele mambo yasijirudie.

Kufanya hivyo ukiwa ndani na huku nje ukiwa na umma in bora kuliko kukosa kujua kinachopangwa huko serikalini.

Zipo taarifa kwamba wahafidhina wanaomba ACT wasiingie serikalini. In kama wanaona nuksi ACT kuingia na has a Maalim Seif.

Tulipofika watu watulize akili na kuacha mihemko.

Wazanzibari wanahitaji kuponywa na wakati huo huo safari ya ukombozi I we salama.

Ni hayo tu.
 
Exactly , Maalim Seif asikubali kabisa kushiriki serikali ya wamwaga damu .Yaani mimi sikujua kabisa kama CCM na viongozi wake wanashida na uongozi wa nchi sana kiasi cha kumwaga damu za maelfu ya watu ili tu wabaki madarakani .
 
Back
Top Bottom