Mwaka 2015 Chadema iliazima mgombea kutoka chama tawala ikitarajia kushinda kwa kishindo, matokeo yake wote tunayafahamu waliangukia pua. Baadaye mgombea huyo aliwatelekeza na kurudi nyumbani kwake, wakashindwa kumchafua kama wanavyofanya kwa watu wengine wanaokihama chama hicho kwa sababu walikuwa wameshatumia nguvu kubwa kuutangazia umma kuwa jamaa alikuwa clean; in short waligeuka mabubu kwake.
2020 hiyo, CDM wanaonekana kuuanza mchakato wa kutafuta wagombea mapema kabisa. Script iliyochezwa na CDM mwaka ule wa 2015, inaonekana kutumiwa na ACT-Wazalendo wakitarajia matokeo tofauti.
Niwakumbushe ACT-Wazalendo kuwa mwaka 2015, Watanzania wengi walitaka mabadiliko, lakini hawakutaka ahadi za baadhi ya watia nia kwa wakati huo kuwa wangeweza kuleta mabadiliko hayo. Yalitokea makundi makubwa manne ambayo ni Neutrals, Team Lowassa, Team Membe, na Upinzani. Team Membe ilionekana kukosa mvuto kwa kiasi kikubwa kwani BM hakuwa na mvuto kabisa kwa wapiga kura. Ili kuepuka mpasuko ndani ya chama, CCM walimweka Mgombea anayeweza kuleta mabadiliko hayo na ambaye hakuwa na makundi yoyote ndani ya chama, huyo ni JPM.
Matumaini mapya yaliibuka, kwani JPM alijipatia wafuasi wengi kutoka katika team hizo kwa sababu alikuwa na record nzuri ya utendaji kwenye Wizara alizoziongoza. Na mia misimamo yake katika utendaji ilifahamika wazi, na ni moja kati ya sifa ambazo tulikuwa tukitaka Rais ajaye awe nazo.
Edo aliporejea CCM, ndipo CDM ilipoanza kuzikwa rasmi. Hata wanachama kindakindaki wa CDM walionekana kuvunjwa mioyo na kitendo hicho wakidai kuwa hawakufurahishwa na kitendo cha viongozi wa CDM kuwaletea mgombea aliyeazimwa kutoka nyumba ya pili. Edo hakuhama CDM peke yake, bali wimbi kubwa la viongozi wa CDM kama Wabunge na madiwani lilimfuata.
Kuna kila dalili kuwa ACT-Wazalendo nao wanataka kucheza mchezo kama huo. Lakini wakumbuke kuwa Edo alikuja huko baada ya mfumo wa chama chake kuona kuwa hafai kupeperusha bendera yake. Hivyo iwapo ACT-Wazalendo nao watamchukua mtu ambaye mfumo wa CCM unamuona kuwa hafai, basi watarajie kupotea kama ambavyo CDM inapoteza mvuto kwa wapiga kura.
Ni vema vyama vikawaamini wanachama wao walioshiriki kuvijenga vyama hivyo katika nyakati za taabu na raha, kwa ndio wenye uchungu halisi na vyama hivyo. Tamaa za muda mfupi na ubinafsi ndio unao vipoteza vyama vingi vya siasa.
Chonde chonde Upinzani, acheni kuazima wagombea kutoka kwa washindani wenu. Siku wakiamua kurudi nyumbani kwao mtapotea mazima, kwani huko kimsingi ndiko ambako rekodi zao za utendaji ndani ya chama zipo. Msitarajie kuwa watadumu kwenu milele.