Chonde chonde Rais Samia mkumbuke Mwijaku katika uteuzi

Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Naomba umteue mtangazaji wa Clouds FM katika cheo cha ukuu wa wilaya kwani kijana huyu ni mzalendo wa hali ya juu.

Kuchukua fomu ya kugombea cheo cha Spika hivi leo kumeonesha jinsi gani Mwijaku ana nia ya kuwatumikia Watanzania.

Mara zote kijana huyu amekuwa mstari wa mbele kuonesha uchawa wa hali ya juu kwako.

Ni mtangazaji wa Kwanza kutangaza kwamba yeye ni chawa wako, na yeyote anayekupinga atapambana naye. Mh.Rais huoni kwamba huyu kijana amejitolea maisha yake kwa ajili yako bila kujali hatari ya Sukuma Gang ya kumzulu?

Isitoshe huyu kijana ni msomi ana degree mbili kutoka vyuo viwili tofauti,UDSM na MZUMBE.

Naomba sana mtukufu Rais kwenye teuzi zako usimsahau,
natabili Mwijaku atagombania hata Ubunge kupitia CCM 2025, akipata mteua awe hata naibu waziri.

Ni hayo tu.
JamiiForums1251708252.jpg
 
Badala ya kumshauri kuwa aache kuwa fisadi na aache kuhamasisha ufisadi kwenye serikali yake tena kupitia TV ya Taifa unamshauri utopolo?Una kichaa?
 
Back
Top Bottom