Chombo cha “Chang’e” cha China chafunga safari tena kuchunguza sayari ya mwezi

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
75
123
VCG111494983489.png
Chombo cha anga za juu cha China, Chang'e No. 6 hivi karibuni kimefanikiwa kurushwa kutoka Kituo cha Anga ya Juu cha Wenchang nchini China kwa kutumia roketi ya Changzheng No. 5. Chombo hicho kitapelekwa katika sehemu ya nyuma ya sayari ya Mwezi, na kufanya utafiti mbalimbali, ikiwemo kuchora ramani, na kuchukua udongo, na kurudi duniani baada ya kumaliza majukumu yake.

Chang'e ni malaika mrembo katika hadithi ya kale ya Kichina, na aliishi pamoja na sungura wake katika Kasri ya Guanghan mwezini. Licha ya hadithi, mwezi pia umesimuliwa sana katika mashairi ya Kichina. Kwa mfano mshairi maarufu Li Bai wa Enzi ya Tang aliuita mwezi “sahani nyeupe”, na mshairi Su Shi wa Enzi ya Song kwenye shairi lake alieleza kwamba ingawa watu wanaopendana wako mbali, lakini wanaweza “kutazama mwezi mmoja angani”. Kuchunguza mwezi ni ndoto ya Wachina inayoendelea kwa maelfu ya miaka.

Chang'e No. 6 itachukua sampuli ya udongo kwenye sehemu ya nyuma ya mwezi. Kwa kuwa kasi ya mwezi kuizunguka dunia na kasi ya kujizunguka ni sawa, sehemu ya mwezi inayoonekana na binadamu ni ileile, na sehemu yake ya nyuma haiwezi kuangaliwa moja kwa moja na binadamu, hivyo hali ya sehemu hiyo haijulikani kabisa. Hadi sasa, binadamu wamechukua sampuli za udongo kutoka kwenye mwezi kwa mara 10, lakini sampuli hizo zote zinatoka kwenye upande wa mbele wa mwezi. Wanasayansi wanaamini kwamba udongo wa upande wa nyuma wa mwezi una historia ndefu zaidi, na una umuhimu mkubwa katika utafiti wa kisayansi. Hivyo, Chang'e No. 6 inapanga kufanya utafiti wa makini kwenye upande wa nyuma wa mwezi, ili kujua mambo mengi zaidi ya sayari hiyo. Imeripotiwa kuwa mchakato mzima wa Chang’e No. 6 kutoka kurushwa kutoka duniani hadi kurudi duniani utachukua takriban siku 53. Ikilinganishwa na Chang'e No. 5 ambayo ilichukua sampuli kutoka kwenye upande wa mbele wa mwezi na kurudi mwaka 2020, Chang'e No. 6 itatumia teknolojia mpya nyingi zaidi, ikiwemo kuchimba udongo kwa akili bandia, kuruka kutoka upande wa nyuma wa mwezi.

Mradi wa Chang'e No. 6 pia ni wa ushirikiano wa kimataifa, kwani licha ya China inayoongoza, nchi nyingine nne zikiwemo Ufaransa, Sweden, Italia na Pakistan pia zimeshiriki kwenye mradi huo. Nchi hizo nne zimeleta vyombo vyao vya kipekee vya kisayansi. Kwa mfano Ufaransa imetoa vifaa vya kitaalamu vya kugundua radoni ili kugundua usambazaji wa gesi ya radoni kwenye uso wa mwezi, Sweden imetoa vifaa vya kuchambua ion hasi, Italia imetoa vifaa vya kusaidia kuchora ramani ya mwezi, na Pakistan imetoa satilaiti ndogo ya ICUBE-Q.

Kuchunguza mwezi si kama tu ni ndoto ya watu wa China, bali pia ni ndoto ya binadamu wote. China itaendelea kuchangia nguvu zake katika matumizi ya amani ya anga ya juu.
 
Inamaana mwezi haujizungushi katika mhimili wake kiasi cha kuchota udongo mara 10 zote wakaishia kuchota upande wa mbele tu.
 
Back
Top Bottom