SEHEMU YA 22
ILIPOISHIA:
“Kesho siendi kazini, nitapumzika nyumbani nifanyefanye usafi.”
“Nielekeze basi nikufuate unakoishi?”
“Akuu! Kwangu huwa hawaingii wanaume, unataka kuja kunifanya nini?” ilisomeka meseji yake, nikaona kama ananizingua, nikaamua kumpigia kabisa huku ‘mkuu wa kaya’ akiwa ameshaanza kusisimka kutokana na majibu yake ya kichokozi.
SASA ENDELEA...
“Nambie!” alisema kwa pozi alipopokea.
“Poa da Jack, mambo yanaendaje?”
“Fresh! Umenikumbuka mpaka jina, una kumbukumbu wewe! Nambie muuza samaki!”
“Mi siitwi muuza samaki bwana, naitwa Chande.”
“Haya nambie muuza samaki Chande, leo kuna nini mpaka umenikumbuka?”
“Nimekumiss mshkaji wangu, nataka kukuona kibonge wangu wa ukweli.”
“Mh! Siyo bure, kunimiss huko vipi?” alisema huku akichekacheka, ikabidi niwe ‘siriasi’ kidogo, nikaanza kumchombeza. Kwenye sekta hiyo nilifanikiwa kumteka kwani kila nilichokuwa naongea, yeye kazi yake ilikuwa ni kucheka tu, mwisho akanielekeza alipokuwa anaishi.
“Nakaa Sinza Mori, hapa nyuma ya Lachaaz,” aliniambia, nikashusha pumzi ndefu na kumshukuru, nikamwambia asubuhi nitakuwa mgeni wake.
“Tena ndiyo vizuri uje unisaidie kufua,” alisema huku akicheka, moyoni nikawa najua kwamba ‘imeisha hiyo’, nikakata simu huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wangu. Sikuwahi kutoka na mwanachuo kama Jack, ingawa nilikuwa na uzoefu sasa na wanawake wenye mwili kama wa kwake, huku mtaani tunawaita vibonge au matipwatipwa.
Baada ya kumaliza kuweka mambo sawa, nilirudi kitandani na kujilaza, angalau mawazo ndani ya kichwa changu yakawa yamepungua. Haukupita muda mrefu, nikapitiwa na usingizi. Nilikuja kuzinduka baada ya kusikia mlango wangu ukigongwa kwa nguvu.
Nikaamka harakaharaka na kwenda kufungua, hamadi! Nikakutana uso kwa uso na baba mdogo ambaye alikuwa akinitazama, akiwa amenikazia macho, nikajua nimekwisha.
“Shika..moo baba!” nilimsalimia kwa kubabaika, hakuitikia salamu yangu na badala yake, alinionesha ishara kwamba nirudi ndani, naye akanifuata, akaja na kukaa kwenye uchago wa kitanda changu, huku akiwa bado amenikazia macho.
“Chande! Najua kuna mambo unayoyajua kuhusu mama yako mdogo lakini hutaki kuniambia. Mimi nakuchukulia kama mwanafamilia lakini inawezekanaje uone mambo yanayonihusu hayaendi sawa halafu ukanyamaza? Huoni kama huo ni usaliti?” aliniuliza baba mdogo, nikawa natetemeka kwelikweli kwa sababu sikuwa najua kilichokuwa ndani ya kichwa chake.
“Nimekuchagua wewe kuwa msimamizi wa hii biashara ya samaki ambayo siyo siri inanisaidia sana kuitunza familia lakini inakusaidia na wewe mwenyewe. Kwa nini unakuwa sehemu ya kunihujumu?” alisema, nikashusha pumzi ndefu na sasa nikawa naamini kwamba kumbe alichokisema mama mdogo kwamba hakuwa anajua chochote kuhusu masuala ya uhusiano wetu, yalikuwa ni ya kweli.
“Baba kiukweli mimi unanilaumu bure tu, hakuna ninachokijua. Ma’mdogo ndiye aliyeniambia kwamba nisiende kuuza samaki kwa sababu kuna mteja wa jumla, jana aliniambia hivyohivyo na leo ameniambia hivyohivyo, nikajua una taarifa,” nilisema huku nikijitahidi sana kukwepesha macho yangu yasikutane na yake maana nilijua anaweza kuujua ukweli kwa kunitazama machoni.
“Hawa wanawake siyo ndugu zetu kabisa, hata wewe ukija kufikia hatua ya kuoa unatakiwa kuwa makini sana, mwanamke anakuwa rafiki yako mambo yako yanapokwenda vizuri tu, mambo yakianza kwenda mrama anakuwa wa kwanza kukukimbia.
“Huyu mamaako mdogo si unaona anavyoanza kunihujumu hapa, mambo yakianza kwenda vibaya nikakosa fedha za kumpa anunue anachokitaka, utasikia anatembea hata na muuza genge, hawana maana kabisa hawa,” alisema baba mdogo, safari hii akionesha kuwa mpole kwangu.
Zile hasira zake zote zilimalizwa na maelezo ya uongo niliyompa, akaendelea kuzungumza na mimi kwa kirefu na kunitaka nisimamie vizuri biashara na mtu wa mwisho ambaye natakiwa kupokea maagizo kutoka kwake, ni yeye na si mtu mwingine yeyote.
“Ikitokea anakwambia chochote, unatakiwa kuniuliza mimi kwanza. Akikwambia sijui kuna mteja wa jumla sijui nini, unatakiwa unipigie mimi simu kwanza usikie nitasema nini,” alisema, nikawa natingisha kichwa kuonesha kwamba namuelewa.
Baada ya mazungumzo marefu, aliinuka na kutoka, akaniacha angalau nikiwa na amani ya moyo. Nilichokuwa nimekiamua kuanzia mwanzo ndicho nilichoendelea kukishikilia ndani ya moyo wangu, ilikuwa ni lazima nianze kumkwepa ma’mdogo kwa sababu tukiendelea tu, siku si nyingi baba mdogo angekuja kuujua ukweli na sijui nini ambacho kingekuja kutokea.
Basi niliendelea kujilaza chumbani kwangu, chakula cha usiku kilipokuwa tayari, ma’mdogo ambaye sasa alikuwa na mumewe kule ndani, alimuagiza mwanaye mmoja aje kuniletea chakula kama ilivyokuwa utaratibu wa siku zote.
Msosi huu haukuwa na u-spesho wowote, kilikuwa ni chakula nilichozoea kula siku zote, nikajua lazima ameogopa kufanya kama alivyofanya ndani ya siku mbili hizi kwa sababu mumewe alikuwepo. Nilikula na baada ya kumaliza, nilitoa vyombo na kwenda kuviweka kwenye karo pale nje.
Wakati nanawa mikono, nilisikia mlango wa chumba cha yule mpangaji ukifunguliwa, akachomoza kichwa na kunitazama huku akigeuka huku na kule kuangalia kama hakukuwa na mtu aliyekuwa akitutazama. Akanionesha ishara kwa mkono kwamba niende, nikatabasamu.
Nilitazama huku na kule na nilipojiridhisha kwamba hakukuwa na mtu anayetutazama, harakaharaka nilielekea kwenye chumba chake, nikachoma ndani mzimamzima.
“Vipi! Umeshakula?”
“Ndiyo!”
“Nilikuwa nimekuandalia msosi wa nguvu nilipotaka kuja kukwambia nikamsikia baba’ako mdogo anaongea na wewe. Vipi kuna nini kwani maana nasikia muda mrefu ni kama wanavutana na mkewe. Amekushtukia nini?”
“Aah! Hamna, ni ishu za kifamilia.”
“Mi nakushauri Chande achana na mama’ako mdogo, siku mwenyewe akijua itakuwa kizaazaa hapa. Kwani mimi sikutoshi?” alisema kwa sauti ya kunong’ona, huku akijigeuzageuza kwa pozi za kikekike, mtandio mwepesi aliokuwa amejifunga ukalifanya umbo lake zuri lijichore, nikameza mate kama fisi aliyeona mfupa.
Je, nini kitafuatia?
Sent using
Jamii Forums mobile app