Chombezo: Tipwatipwa tetema, Oooh tetema

Chombezo: Tipwatipwa tetema, Oooh tetema

SEHEMU YA 29

ILIPOISHIA:
Nilivuta picha na kujiona nikiwa nimekonda sana, mwili mzima ukiwa na vidonda na nikikohoa sana kutokana na maambukizi ya Ukimwi, mapichapicha ya majeneza, watu wakiwa msibani na misalaba makaburini yakawa yanapitapita kwenye kichwa changu na kuzidi kunipagawisha.
“Hebu ngoja kwanza, dereva hebu simama!” nilisema kwa sauti ya juu, Jack akanigeukia kwa mshangao.
SASA ENDELEA...
“Vipi tena?”
“Nimepigiwa simu kuna dharura nyumbani! Wewe nenda mimi nitakuja siku nyingine,” nilimwambia huku nikiwa tayari nimeshasimama na kwa kuwa nilikuwa nimepanda upande wa mlangoni, Bajaj iliposimama tu, niliruka na kuzunguka upande wa nyuma, nikavuka barabara mbiombio huku nikikoswakoswa na magari na bodaboda.
“Chandeee! Una nini wewe?” aliita Jack kwa sauti ya juu lakini tayari alishachelewa, daladala iliyokuwa inatokea upande wa Shekilango ikielekea Makumbusho ilikuwa imenikaribia, nikaipungia mkono, ikasimama! Nikajichoma ndani na safari ikaanza huku nikigeuka kumtazama Jack na yule dereva wa bodaboda ambao walikuwa wamepigwa na butwaa.
Niliwaona wakigeuza Bajaj na wakawa wanaifuata ile daladala yetu kwa nyuma, Jack akawa ananipigia simu yangu, nikapokea.
“Mbona sikuelewi Chande!”
“Nimepigiwa simu Jack! Nyumbani kuna matatizo.”
“Muongo! Muda wote upo na mimi mbona sijaona simu yako ikiita?”
“Imeita Jack, kweli tena.”
“Unakimbia kwenda kupima si ndiyo?”
“Ha...pa...na! Sijakimbia.”
“Kwa hiyo kumbe wewe unajijua una ngoma ulikuwa unataka kuniambukiza si ndiyo?”
“Mimi sina ngoma Jack! Kweli tena, huwa natumia kinga,” nilidanganya huku nikitetemeka. Hofu ya kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ilinifanya niwe mithili ya kifaranga cha kuku kilicholowanishwa na mvua.
“Sasa sikia! Najua hujapigiwa simu wala nini ila umekwepa kupima ngoma! Nakupa nafasi ya mwisho, shuka kwenye daladala sisi tupo nyuma yako, mguu wangu mguu wako mpaka hospitali tukapime. Ukikataa kwenda kupima leo basi naomba usinitafute tena.”
“Nitakuja Jack lakini siyo sasa hivi! Nakuomba unielewe! Nitakuja, kweli tena, siyo kwamba naogopa kupima,” nilisema lakini Jack akakata simu akionesha kupandwa na jazba. Mbele kidogo niliishuhudia ile Bajaj ikigeuza na kurudi kule ilikotoka, nikashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye siti yangu.
Kumbe wakati naongea na Jack, nilikuwa naongea kwa sauti ya juu kiasi cha kufanya abiria wengine wote wawe wananitolea macho huku wengine wakibonyezana. Nikasikia wengine wakianza kucheka chinichini huku wakinitazama kwa macho ya kuibia.
“Vipi kijana, unaogopa kupima ngoma? Inaonesha una mambo mengi wewe.”
“Aah! Hamna mzee, huyu dada anataka kunichanganya.”
“Sasa unaogopa nini? Si bora ukapime ili ujue moja! Siku hizi kuna dawa na ukifuata masharti unaweza kuishi miaka mingi tu, nakushauri nenda kapime,” yule mzee niliyekuwa nimekaa naye siti moja alianza kunihubiria kwa sauti kubwa, nikaona kama anazidi kuniletea ‘uchawi’.
“We mzee vipi wewe? Nakuheshimu ujue,” nilisema kwa sauti ya juu huku nikisimama pale nilipokuwa nimekaa, abiria wengine wakaanza kuchangia hoja, eti kila mtu akinishauri nikapime.
“Nyie mmepima? Mbona mnanishikia bango mimi? Kwanza sijawahi kufanya mapenzi, mimi bado mdogo,” nilisema kwa sauti ya kupaniki na kusababisha abiria wote ndani ya daladala waangue vicheko kwa nguvu.
“Hata macho yako yanaonesha kwamba wewe ni mjanjamjanja sana wa wanawake! Naona umepatikana leo, kapime kijana,” walizidi kunishambulia nikaona njia nyepesi ya kuepukana na zogo hilo ni kuteremka kwenye daladala.
“Konda shusha hapo!”
“Unashuka umefika kweli? Au ndiyo umevurugwa?” yule mzee akizidi kuniandamana, abiria wote wakawa wanacheka hawana mbavu. Daladala ilipopunguza mwendo kwa sababu ya foleni, nilienda kushuka kwa nguvu, konda wala hakunidai nauli, naye akawa anacheka sana.
“Mnapenda kuuza mechi mkiambiwa kupima mnakuwa wakali! Kapime mdogo wangu, ngoma kitu gani kwani,” alisema kondakta nikiwa nimeshateremka, nikasikia gumzo kubwa likiibuka mle ndani ya daladala, kila mtu akisema lake.
Hata sikuwa najua pale niliposhukia ni wapi, niliiona siku hiyo kuwa ya mkosi mkubwa kwangu!
Nyumbani baba mdogo anatishia kwamba akimgundua anayemlia mali zake atamuoa kisha kumchinja, Jack ananing’ang’aniza nikapime virusi vya Ukimwi, abiria ambao hata hawanifahamu nao wananishikia bango nikapime! Ama kwa hakika ilikuwa siku mbaya sana kwangu.
“Broo eti hapa ni wapi?”
“Bamaga!”
“Hapa nikitaka kwenda Kinondoni napanda magari ya wapi?”
“Panda yanayoenda Makumbusho, ukifika pale kituoni ndiyo kuna magari! Vipi mbona jasho linakutoka sana?”
“Aah! Kawaida tu,” nilimjibu kijana mmoja aliyekuwa anauza maji pale kituoni, nikawa naelekea kwenye sehemu ya kuvuka barabara ili nikapande magari ya Makumbusho kama alivyoniambia! Kichwa kilikuwa kimechanganyiki
wa kabisa.
Ni hapo ndipo nilipomkumbuka yule mama niliyekutana naye kwenye daladala wakati nikimfuata Jack, nikaona anaweza kuwa msaada mzuri kwangu kwa muda huo kwani nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa.
“Haloo mama!”
“Haloo mwanangu! Umefika Mori?”
“Nimefika mama na sasa narudi! Nilikuwa nataka kuonana na wewe, ulisema nitakupataje?”
“Hapo ulipo kuna dereva yeyote wa bodaboda?”
“Ndiyo!”
“Hebu mpe simu niongee naye!” aliniambia, nikamsogelea dereva mmoja wa bodaboda ambaye baada ya salamu, nilimpa simu, akawa anaongea na yule mama.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 30

ILIPOISHIA:
“Hapo ulipo kuna dereva yeyote wa bodaboda?”
“Ndiyo!”
“Hebu mpe simu niongee naye!” aliniambia, nikamsogelea dereva mmoja wa bodaboda ambaye baada ya salamu, nilimpa simu, akawa anaongea na yule mama.
SASA ENDELEA...
Baada ya muda, alinirudishia simu yake na kuniambia kwamba wameshaelewana. Akanipa ishara kwamba nipande na safari ikaanza nikiwa sielewi ni wapi tunapoelekea. Tulienda mpaka Mikocheni, dereva akawa anakata mitaa tu na muda mfupi baadaye, alipunguza mwendo na kusimama.
“Mpigie mwambie tumeshafika,” alisema, nikatoa simu huku nikishangaa huku na kule, mandhari ya eneo hilo yalinifanya nishikwe na ushamba. Nyumba zote zilikuwa za maana kwelikweli, zikiwa na mageti makubwa! Mtaa wote ulikuwa kimya kabisa.
“Nimefika mama!”
“Haya ngoja nakuja, usimlipe huyo bodaboda tumeshaelewana,” alisema kisha nikakata simu. Muda mfupi baadaye, geti moja lilifunguliwa, nikamuona yule mama akitoka, safari hii akiwa amebadilisha nguo na kuvaa kinyumbaninyumb
ani, mkononi akiwa ameshika noti ya shilingi elfu kumi.
Alikuja mpaka pale tuliposimama, tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, akampa dereva bodaboda ile hela kisha akanipa ishara kwamba nipokee chenji kutoka kwa yule bodaboda.
“Haya ahsante kijana, hebu mpe namba yako ya simu ili baadaye akupigie,” alisema, basi yule dereva wa bodaboda akanitajia namba yake, nikawa nahangaika kusevu kwenye kisimu changu huku nikiwa nakifichaficha. Baada ya kumalizana naye, tuliongozana na yule mama mpaka ndani.
Lilikuwa jumba la maana kwelikweli, mle ndani kulikuwa na bustani nzuri za maua zilizotunzwa vizuri. Kumbe wakati nampigia simu, alikuwa amekaa bustanini akiwa anasoma ‘novel’ huku mezani kukiwa na laptop ya kisasa! Ilionesha yule mama alikuwa anaishi maisha ya ‘kishua’ kwelikweli tofauti kabisa na nilivyomdhania nilipomuona kwa mara ya kwanza. Nilijiuliza kama hayo ndiyo maisha yake, kwa nini ahangaike kupanda daladala? Sikupata majibu.
“Vipi Chande, kwema?”
“Kwema mama, shikamoo!”
“Si tulishasalimiana jamani? Haya marahaba, umefurahi sasa,” alisema huku akitabasamu, nikajikuta na mimi nimetabasamu.
“Unaendeleaje?”
“Aah! Bado mama, natembea kigumu tu lakini hata siko poa,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu na kusogeza kiti chake karibu yangu, akawa anaongea na mimi kwa upole akitaka nimueleze ni nini kilichokuwa kinanisibu. Kwa hali ilivyokuwa, sikuwa na ujanja zaidi ya kumueleza.
Nilianza kwa kumueleza historia yangu tangu nilipofika jijini Dar es Salaam baada ya kuchukuliwa kijijini na baba mdogo. Nilimuleza jinsi nilivyoanza kufanya biashara ya samaki na jinsi pepo mchafu alivyonikumba kiasi cha kunifanya niwe nabadilisha wanawake hovyo, tena bila tahadhari.
Sikumficha kitu, nilimueleza yote mpaka nilivyojikuta nikiangukia dhambini na ma’mdogo na yote yaliyokuwa yanaendelea mpaka kilichotokea asubuhi hiyo nilipoenda kuonana na Jack na kunishinikiza nikapime ‘ngoma’.
Nilipofika hapo, alishindwa kujizuia, akacheka sana mpaka machozi yakawa yanamtoka.
“Kwa nini unajihusisha na mambo yote hayo wakati nikikuangalia umri wako bado mdogo? Kwa nini unacheza kwenye miiba tena ukiwa huna viatu? Hujui dunia imeharibika sana siku hizi?” aliniambia huku akikaa vizuri. Akaanza kunipa darasa la nguvu, alinieleza madhara ninayoweza kuyapata kutokana na tabia yangu ya kubadilisha wanawake hovyo na mwisho akaja kwenye ‘point’ ya kupima.
Alinipa ushauri nasaha wa nguvu, akanitaka niondoe hofu ndani ya moyo wangu na kukubali kupima kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee inayoweza kunifanya nikajua kuhusu hali yangu ya kiafya na kujua nini cha kufanya.
“Siku hizi kuna dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi lakini pia wapo watu ambao hata mimi nawajua wameishi miaka mingi tu wakiwa na virusi, cha msingi ni kufuata masharti, nikazidi kuchanganyikiwa.
Kutokana na ushawishi mkubwa alioutumia, hatimaye nilijikuta nikifanya maamuzi magumu kwamba liwalo na liwe. Akaniambia ndani kwake ana vipimo vya Ukimwi ambavyo hutoa majibu kwa usahihi zaidi ndani yamuda mfupi na akanihakikishia kwamba kama nitakuwa nimeathirika, atanisaidia kwa kila kitu.
Aliinuka na kwenda ndani, muda mfupi baadaye alitoka na kipimo, sikuwa najua kwamba siku hizi kumbe unaweza hata kupima Ukimwi nyumbani. Akanitoboa kidogo kwenye kidole na kuchukua damu, nikawa natetemeka kuliko kawaida.
“Ukikutwa una virusi vya Ukimwi utachukua uamuzi gani?” aliniuliza, nikawa nababaika nikiwa hata sijui nini cha kumjibu, akabadilisha swali.
“Ukijikuta huna virusi vya Ukimwi utafanyaje?”
“Nitashukuru sana, nitamshukuru Mungu na kamwe sitarudia tena makosa. Nitatulia na kusubiri mpaka muda wa kuoa ufike, na ukifika nitahakikisha naenda kumpima huyo mchumba wangu, nimekoma,” nilisema huku bado nikiwa natetemeka, akachukua kile kipimo alichokuwa amekiweka mezani kikiendelea kusoma majibu.
“Habari njema ni kwamba huna maambukizi ya virusi vya Ukimwi ila kwa uhakika inabidi tuje turudie tena baada ya miezi mitatu,” alisema, furaha niliyokuwa nayo nilijikuta nikimrukia mwilini na kumkumbatia kwa nguvu, na yeye akanikumbatia.
“Unaonaje kama ukihamia na kuja kukaa hapa? Nina hakika nitakudhibiti na utakuwa umeondokana na hatari kubwa ya kuja kufumaniwa na mama’ako mdogo.”
“Nashukuru mama! Nipo tayari hata kuwa nakutunzia bustani zako na kufanya usafi, kwani hapa unaishi na nani?”
“Naishi mwenyewe na dada wa kazi! Wanangu wanasoma nje ya nchi.”
“Na mzee je?”
“Mzee gani tena! Mume wangu alifariki miaka mingi tu iliyopita! Naishi mwenyewe na nimeshazoea,” aliniambia, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama. Kiukweli nilimshukuru sana na sikutaka kupoteza muda, tulikubaliana kwamba nirudi nyumbani na kwenda kuaga, nitumie njia yoyote ilimradi niondoke kwa usalama.
Kweli nilifanya hivyo, nilirudi nyumbani ambako nilimdanganya baba mdogo kwamba nataka kwenda kusalimia kijijini mara moja kisha nitarejea. Mama mdogo alikuwa mgumu sana kukubaliana na suala hilo lakini niliposhikilia msimamo, alikubali.
Nikaenda kuyaanza maisha mapya ya Mikocheni, huku nikibadilisha namba ya simu, nikapewa simu mpya nzuri ambayo ndiyo niliyoweka laini yangu mpya na nikaanza ukurasa mpya wa maisha yangu.
Baada ya miezi kama mitatu hivi kupita, nilikuja kumtafuta tena Jack na kumweleza kwamba nipo tayari kwenda kupima lakini aliniambia kwamba tayari alishapata mwanaume mwingine ambaye walienda kupima na sasa hivi wapo kwenye mipango ya ndoa, japo niliumia moyoni lakini niliamua kuyaacha mambo yasonge mbele.
Nikamtakia kila la heri kwenye maisha yake na tukaendelea kuwa marafiki wa kawaida. Mwishoni mwa mwaka, watoto wa yule mama walirejea kutoka nchini Uingereza walikokuwa wanasoma, nao wakafurahi sana kunikuta pale kwao, nikiwa namsaidia mama yao majukumu ya hapa na pale.
Siku zilizidi kusonga mbele, baadaye nikajikuta katika penzi na mtoto wa yule mama aliyekuwa anaitwa Trixie, tukapendana sana na mama yake akaona hakuna tatizo kwa sisi kuwa wapenzi lakini hakutaka tugusane kabisa mpaka tutakapofunga ndoa na kuwa mume na mke.
Kwa kuwa Trixie hakuwa amemaliza masomo, shule zilipofunguliwa, alisafiri na wenzake kwenda kumalizia masomo, tukawa tunaendelea kuwasiliana kwa karibu, huku nyuma yule mama sasa akawa ananichukulia kama mkwewe ambapo aliniambia natakiwa kurudi shule ili angalau na mimi niwe na msingi imara kwenye maisha yangu.
Nilipelekwa VETA ambako nilianza masomo ya ujenzi wa minara ya simu, nikaelekeza nguvu zangu zote huko na taratibu maisha yangu yakaanza kubadilika. Mwaka mmoja baadaye, mimi na Trixie tulifunga ndoa baada ya kuwa tumepima afya zetu na hatimaye tukawa mke na mume.
Namshukuru Mungu kwamba mpaka sasa maisha yanaendelea vizuri, mimi ni fundi wa minara ya simu, Trixie anafanya kazi benki na tayari tuna mtoto mmoja, makazi yetu yakiwa ni Mbezi Beach.

*MWISHO.*
 
Safi sana... Bonge la story...

Chapter Closed...

Cc: mahondaw
 
Naona the bold kabadilisha Tasnia kutoka shushushu mbobevu mpaka kuwa mchuuzi wa Samaki mwenye uchu wa papuchi
 
aaaahh mi nkajua maza nae utambandua,umezingua aisee
 
HUBA LA MISS TANZANIA-PART 23

"Ooh my God.....looh salaleee...! picha yangu kabisaaa au mtu anayefanana na mimi?" aliuliza kwa mshtuko Shebby baada ya kusimuliwa na Sada juu ya ujio wa mtu wanayemhisi ni afisa usalama, ambaye alikuwa hana asili wala fasili mtu huyo machoni mwao. Mtu huyo alikuwa si mwingine bali ni Kachero Manu alikuwa amefika kazini kwao RAJA SAFARI TOURS kufanya taftishi na baadhi ya watumishi wa hapo. Kilichomleta hapo kwenye kampuni hiyo ni kujaribu kufanya taftishi kama muuaji wa Profesa Kaganda ndio huyo huyo muuaji wa Bwana Pateli! Taftishi ambayo ilizaa matunda asiyoyategemea kwa Kachero Manu. "Ni sura yako wewe nakufahamu vizuri sibahatishi na sijaja hapa kuleta maneno ya mkahawani au kwenye vijiwe vya kahawa" Sada alikazia maneno kwa ukali akionyesha kutopendezewa na ubishi wa Shebby. "Nisamehe bestito sijakusudia kukubishia, haya tuyaache kwanza, ehee...! Akasemaje sasa huyo jamaa kuwa nimefanya tukio gani? " aliomba msamaha Shebby huku akiendelea kumdodosa Sada. "Kapita kuhoji kila mtu pale kazini huku anamuonyesha picha yako, sasa Mzee Sheni yule mpishi wako uliyekuwa unaenda nae mbugani karopoka maneno ya sumu hata yasiyohusu, sijui oooh...! Ulikufukuzwa kazi kwa sababu mkichangia bibi na Bosi wetu marehemu Pateli, hapo ndio huyo mgeni akavutika na udaku wa Mzee Sheni kaondoka nae ofisini katokomea kusipojulikana... kila mtu anasikitika juu yake yule Mzee sijui ataacha lini taarifa za lolololo, zitakuja kumponza siku za usoni" alizidi kupasua maneno Sada bila mficho kwa Shebby bila kuelewa kuwa amemfaa vilivyo. "Naanza kuogopa sasa mie nimefanya kosa gani mpaka nasakwa kwa udi na uvumba! " alijisemesha kwa huzuni Shebby hali ya kuwa anajua kila kitu kinachoendelea. "Dalili zinaonyesha ni usalama wa taifa huyo mtu, maana kaja na gari zao nyeusi zile" alizidi kuweka tashididi ya mazungumzo yake. Shebby sasa taharuki ilimkamata vilivyo, alitambua sasa polisi wameshafika mbali kwenye uchunguzi wao wa mauaji ya mfululizo kuanzia kwa Bosi Pateli na Profesa Kaganda. Hivyo akizubaa kidogo tu itakula kwake atashindwa kutekeleza kisasi chake kwa Dr.Sonko. "Inabidi bestito Sada unipe hifadhi nyumbani kwako la sivyo nitaumbuka! " alivunja ukimya Shebby kwa Sada akiomba auni ya ulinzi. Sada alivuta pumzi ndefu baada ya kusikia maneno yake ya Shebby. "Unanipa mtihani mzito sana Shebby, maana hujaniambia umefanya nini mpaka unatafuta, lakini pia hata mie unanipa mashaka unaonekana mambo yako kiuchumi sasa yapo bambam unasukuma ndinga la gharama huenda kuna tukio zito umefanya unatafutwa!" Sada alitikisa kiberiti kwa Shebby huku akionyesha kama hatokubali kirahisi. Lakini uhalisia wa mambo Sada alikuwa anampenda kwa dhati Shebby alikuwa hawezi kupindua kwa chochote atakachomwambia. Kwa zaidi ya miaka 6 tokea wamefahamiana, Sada alikuwa moyoni anaungua kwa joto la mapenzi kwa Shebby, na ndio maana alipoona kuna mtu anamsaka Shebby alishindwa kujizuia kutokumpa taarifa. Miaka yote alikuwa anajipa moyo ipo siku tu, huenda Shebby atamtakia kuwa anampenda. Aliposikia Shebby amenasa kwenye huba la Miss Tanzania na kishatangaza ndoa, aliugua karibia mwezi mzima, yu mahamumu hoi bin taabani hajiwezi kitandani. Alipopata nafuu na kurudi kazini alianza kuzoea kuwa Shebby ndio kapuruchuka sio wake tena, lakini walipoonana siku Shebby amekuja kuchukua barua yake toka kuzimu pale ofisini, ugonjwa wake wa huba kwa Shebby ukaibuka upya. Meseji cha chombezo zile za umeamkaje, umeshindaje na za usiku mwema zilikuwa hazikauki katika simu ya Shebby toka kwa Sada. "Hata wewe Sada, mwandani wangu huniamini unaniona kama mimi ni mjuba nishakua mtu wa ovyo sasa nani ataniamini tena?" alijifaragua kujilalamisha mbele ya Sada huku akijivika usoni mwake huzuni kubwa na kujitia kuinama chini. "Baby.....usinidhanie vibaya, sikuwa na nia mbaya nikihofia tu nikataka unitoe wasiwasi mimi nakuaminia zaidi ya asilimia 100% huwezi kuniingiza matatizoni" alijibu Sada huku moyoni akiwa na mlipuko wa furaha wa kuitwa mwandani na Shebby kwa mara ya kwanza kwa muda wa miaka 6. Shebby akawa anachekea tumboni kwa namna alivyomnasa kiulaini Sada kwenye mtego wake wa kumpa hifadhi mpaka anaitwa 'baby'. Maana alifahamu fika sasa msako dhidi yake wakimkosa nyumbani kwake, utahamia kwenye mahoteli na nyumba za kulala wageni hivyo hatokuwa salama kabisa. Kimbilio pekee ambapo ni salama palibaki nyumbani kwa Sada na ingekuwa ngumu kwa vyombo vya usalama kuleta hisia kuwa Shebby yupo nyumbani kwa Sada." Nilikuwa nataka kushangaa sana kama na wewe Sada ni rafiki mnafiki yule mkia wa fisi, ambaye wakati wa shida anakuepa kama mkoma vile" alizungumza Shebby kwa kujiamini huku anamalizia 'Ice-cream' yake kushushia mlo wake kabambe. Wakaendelea kusogoa hadithi moja mbili tatu huku wakijiandaa kuondoka kuelekea nyumbani kwa Sada huku furaha ya Sada ikiwa ni sheshe kama kumsukuma mlevi akijua fika Shebby akifika kwake vibwanga na vitimbi atakavyomfanyia hawezi kupindua kwake.

Ulikuwa ni usiku mbichi wa saa 2:30 usiku katika maeneo ya 'Mbezi Juu-Kwa Pembe' siku hiyo ya Jumamosi,Kachero Manu alikuwa ndio kwanza anaegesha kwenye eneo la maegesho la 'LIBRA SOCIAL HALL' gari yake aina ya 'Toyota Crown Royal Saloon' rangi ya maziwa. Aliegesha eneo ambalo hatapata usumbufu pindi atakapohitaji kuliondoa gari lake kwa haraka hasa ukichukulia siku hiyo ni ya mwishoni mwa juma, kadamnasi ya watu walikuwa wamefurika kuja kustarehe mpaka che. Ilikuwa dalili zinaonyesha ndani ya ukumbi ule kulikuwa kuna tafrija ya harusi inafanyika. Wahudhuriaji walikuwa wanazidi kumiminika huku wakiwa wamevalia mavazi yao nadhifu huku wakionekana wana furaha kubwa. Ghafla wakati Kachero Manu anajiandaa kuvuka upande aingie kwenye moja ya mashine za kutolea fedha zilizopo hapo hapo 'LIBRA SOCIAL HALL' usafiri wa Bwana na Bibi harusi ulikuwa unaingia. Fahari ya macho ikabidi Kachero Manu akodoe macho kuwaangalia wapendanao hao waliokuwa ndio wanashuka kwenye gari yao ya kifahari huku Bibi harusi akionekana kupendeza mpendezo wa Shamsi Matlai. Wakawa wanatembea masi masi kwa mwendo wa pole kuingia ukumbini mule,huku nyimbo mbalimbali za muziki zkipigwa kuchagiza uingiaji wao ndani ya ukumbi. Kachero Manu akapuuzia kuendelea kufuatilia yasiyomhusu akavuka ng'ambo ya pili na kuingia kwenye moja ya mashine ya kutolea fedha ya katikati inayomilikiwa na benki ya NBC, huku yasari kwake kulikuwa na mashine ya benki ya NMB na yamini kwake kuna mashine ya benki ya CRDB, na zote zilikuwa na watu wanachukua fulusi zao wakafanye mapochozi ya usiku huo kwenye starehe zao za mwishoni mwa juma. Akachukua kiasi cha pesa anachohitaji kisha akatoka na kuifuata barabara ya giza ya upande wa kulia kama alivyoelekezwa nyumbani kwa Shebby. Alitembelea kwa mwendo wa mashi mashi kwa takribani robo saa, mpaka akakutana na kibanda umiza kimejaza watu kibao wanashuhudia mchuano wa mechi za ligi kuu ya uingereza kabumbu uwanjani wachezaji wanamenyana katika runinga. Akapita na hamsini zake na hamna hata mmoja hata aliyegeuka kumtazama yeye. Alivyoenda mbele zaidi akaanza kuteremka bonde kushuka chini kwa mbali akawa ameziona nyumba nga'mbo ya pili zimejitenga. Akaenda mubashara kwenye baiti mojawapo ya kati kati ambayo ni duka la kuuza bidhaa ndogondogo. Alipofika dukani, alikuta wateja wanahudumia bidhaa mbalimbali za mahitaji yao ya siku, akazuga nae pia ni kama mhitaji wa bidhaa huku macho yake yote yanakodoa nyumba ya pili yake ambayo ndio nyumba haswa anayoishi Shebby. Alimuona mama mmoja yupo nje ya kibaraza anachoma maandazi. Akafanya maamuzi ya kumvaa yule kumuulizia kama Shebby yupo kwenye baiti. "Mama shikamoo...mimi ni mgeni wa mpangaji mwenzenu Shabani Zomboko sijui nimemkuta? " aliuliza Kachero Manu kwa yule mama. "Marhaba mwanangu, wala sifahamu maana huyo Shebby kutoka kwake na kurejea kwake anajuaga mwenyewe, labda umpigie simu au pita moja kwa moja na veranda hiyo chumba chake kimejitenga peke yake utakiona tu! " alijibu yule bila kumtazama usoni Kachero Manu huku akiweka maandazi mapya ya kuchoma kwenye karai linalochemka mafuta ikiwa ni ishara hana haja ya maswali zaidi yupo kikazi zaidi. Kachero Manu akajiongeza akaanza kutembea na veranda huku akigusa kiunoni kuhakikisha mguu wa kuku wake upo salama tayari kwa kutumika kama ikibidi. Kwa bahati baiti yote ilikuwa kimya kasoro chumba kimojawapo kulikuwa na muziki unapigwa kwa sauti ya chini. Akafika kwenye kile chumba kilichoungana na sebule alichopanga Shebby akakuta taa zimezimwa ishara ya kwamba hamna mtu ndani. Akaanza kubisha hodi kujiridhisha kama kweli hamna mtu. Aligonga kama mara tatu ukimya ukawa umetamalaki. Akaangalia muda kwenye saa yake ya mkononi, saa ikasoma ni saa 3:15 usiku juu ya alama. Himahima akachomoa mkungu wa funguo zake malaya mfukoni akaanza kukorokochoa kwa funguo hizo kwenye kitasa hicho cha mlango. Funguo wa tatu kujaribisha ukakubali kukifungua kitasa kile sasa mlango ukawa umefunguka. Haraka haraka akaingia ndani na kuurudishia mlango ule bila kufunga tena na ufunguo, alijua hatopoteza wakati mrefu. Akawasha kurunzi yake ndogo ya kumuwezesha kupata nuru ya kutosha kumuongoza chumbani mule huku mkono mwingine ukiwa umebeba bastola tayari kwa kushughulika ikibidi. Alipotupa macho kwenye sebule ile kwa haraka haraka hakuona chochote kitakachokuwa msaada kwake akaamua aelekee chumbani kwa Shebby. Kwa bahati alipokanyaga tu zulia la kujifutia miguu akahisi kama kuna kitu kigumu chini yake. Akanyanyua zulia lile akaona funguo mbili moja kubwa na nyingine zimeunganishwa kwa silsila nyembamba. Akatabasamu kwa jinsi mambo yanavyokwenda bambam. Akafungua mlango wa chumba kile akaingia bila hata kuubugaza mlango kwa pupa yake aliyokuwa nayo. Alipomulika kurunzi kitandani akakuta picha zimezagaa pale kitandani akasogelea na kuokota picha mojawapo. Ilikuwa ni picha ya Profesa Kaganda ikiwa imewekwa alama ya vema kuonyesha tayari ameshashughulikiwa. "Shabaaashi...! Huyu ndio muuaji asiyejulikana maluhuni mkubwa Shebby utanitambua mimi ni nani! " alijikuta anaropoka kwa sauti ya taratibu. "Tupa silaha yako chini na nyoosha mikono juu" ilikuwa ni sauti ya kama muungurumo wa radi katika masikio ya Kachero Manu huku mtutu baridi wa bastola ukiwa umegusa sikio lake la kushoto. Alishtukizwa kwa namna asiyoitarajia hata kidogo mpaka akajilaumu kwa kutochukua tahadhari ya kutosha. Bila ubishi wowote akatupa chini bastola yake na kunyoosha mikono yake, likawa ni kosa la kujutia la pili kwa Kachero Manu. Mtu yule aliyemuweka chini ya ulinzi akamnukiza puani kwa kitambaa, hanchifu kilicholowa kemikali. Pale pale Kachero Manu akajikuta anaishiwa nguvu na kuanguka chini puuuh kwa kupigiza kichwa kwenye tendegu la mguu wa kitanda kama papai lililoiva sana. Akapoteza fahamu chumbani mule mwa Shebby.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom