Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,662
- Thread starter
- #21
CHOMBEZO: Mzee wa Dodo
SEHEMU: 21
MTUNZI: DR AMBE
SIMU: 0713646500….
...Snura alipagawa alikuwa kama kidonda kilichowekewa chumvi jinsi raha zilizokuwa zikimchonyota. Si wajinga waliosema ukiwa na hamu hata utafune makalatasi utayaona matamu. Snura alizitengeneza hamu mwenyewe alipoonja utamu ukakolea.
Baada ya mshikemshike wa kukata na shoka Snura alichoka kama aliyekuwa akitwaga chuma na usingizi mzito ulimchukua. Tumu naye alijilaza pembeni ya mkewe alikuwa amechoka sana baada ya kupiga mbili kwa moja.
****
Teddy baada ya mshikemshike wa usiku alizinduka usingizini baada ya kuamshwa na alam aliyotega kwa ajili ya kumwamsha kufanya kazi ya kufanya usafi na kuwaandalia matajiri zake kifungua kinywa na chakula la Gift. Kila alipotaka kunyanyuka kitandani uchovu ulikuwa mkubwa sawa.
Alijikuta akichukia kuwa msichana wa kazi, aliamini kama angekuwa mke wa Tumu basi angeamka muda anaotaka. Alisema alale kidogo kabla ya kuamka lakini aliposhtuka alikuta ameamka saa mbili kasoro asubuhi. Alinyanyuka haraka na kujiuliza tajiri zake wameondoka bila kupata kufungua kinywa.
Alitoka hadi sebuleni na kushtuka kukuta mlango umefungwa kwa ndani hakuna dalili zozote za watu kutoka. Ili kupata uhakika alikwenda hadi kwenye mlango cha chumba cha tajiri wake na kuonekana umefungwa ndani.
Alikwenda kuoga na kuandaa kifungua kinywa na chakula cha mtoto.
Mpaka anamaliza kuandaa pia kumlisha mtoto, tajiri zake walikuwa hawajaamka. Alijikuta akijiuliza siku ile ni siku gani kwani aliamini si mwisho wa wiki pia haikuwa siku ya sikukuu.
Wazo la kwenda kuwaamsha alikuwa nalo kwa kuhofia tajiri zake kuchelewa kazini japokuwa muda ulikuwa umekwenda. Wakati akienda kugonga mlango Tumu alikuwa ameshtuka usingizini na kuangalia saa iliyomuonesha ni saa tatu za asubuhi. Alishtuka usingizini na kumuamsha mkewe.
“Mke wangu tumechelewa kazini.”
“Kwani saa ngapi?”
“Saa tatu.”
“Duh! Sasa nifanyeje?”
“Itakuwaje kazini leo?”
“Watajijua wenyewe.”
“Mke wangu oga uwahi kazini.”
“Nikafanye nini?”
“Leo huendi?”
“Siendi”
Snura alijibu huku akigeuka na kujilaza kifudifudi na kumuachia nundu mumewe ambayo kwa muda ule alikuwa amemkinahi. Japokuwa naye alikuwa amechoka alinyanyuka na kutoka kwanza nje ili kuangalia hali iliyo. Alipofungua mlango alikutana na Teddy na kushtuka.
“Vipi Teddy?”
“Leo hamuendi kazini?”
“Ndiyo.”
“Kwa nini?”
“Siyo juu yako.”
“Mmh! Sawa.”
Tumu aliamini muda ule anaweza kuzungumza mawili matatu na Teddy kabla mkewe hajaamka.
“Teddy vipi?”
“Safi, shikamoo shemeji.”
“Asante. hebu ngoja,” Tumu alisema huku akirudi ndani.
Tumu alirudi ndani kwenda kumuangalia mkewe na kumkuta ndiyo kwanza anajigeuza katikati ya usingizi na kuendelea kulala mlao wa mchoko.
Alirudi haraka kumfuata Teddy ambaye wakati huo alikuwa jikoni akifanya usafi wa vyombo, alipofika alimtekenya.
“Aiiih!” Teddy aliruka na kusababisha chombo alichokuwa ameshika mkononi kidondoke chini na kupasuka.
“Muongo! Bado hazijaisha?”
“Ziishe wapi ulikuwa unamkomaza mwanao ukanisahau mama yake.”
“Mmh! Mpenzi si umesema wewe imetosha.”
“Ulitaka sifa nilikula vikataka kurudi lakini hamu haaishi.”
“Jamani si ulitaka mtoto akamilike viungo.”
“Mmh! Mwenzio sijui hata nilikuwa dunia gani, yaani namuonea wivu mama Gift. Ingekuwa kila siku kama yeye ningenenepaje .”
“Mpenzi tuachane na hayo kuna kitu nataka kukuuliza.”
“Kipi mpenzi?”
“Eti mimba hii ya nani?” Tumu alimuuliza akiwa anamtazama usoni kwa jicho kavu.
“Sijakuelewa una maana gani?” swali lilimshtua Teddy.
“Hapana, lazima nijue nani mwenye ujauzito huu.”
“Simjui,” Teddy alijibu huku akimpa mgongo Tumu.
“Kwa hiyo baba wa mtoto humjui?”
“Ndiyo, unamjua wewe.”
“Sasa mimi nitamjueaje ukiwa mwenye tumbo ni wewe?”
“Mwenye tumbo ni mimi lakini muwekaji ni wewe, sasa sijui kama humjui muwekaji.”
“Teddy hebu kuwa mkweli ili tujue nani mwenye mzigo.”
“Simjui,” Teddy alijibu kwa mkato na kuinama kookota vipande vya sahani vilivyo pasuka.
“Sasa mbona unasema wangu.”
“Nikuulize wewe unayejitoa akili,” Teddy alikuwa mkali.
“Akili kivipi?”
“Hii mimba kanipa nani?” alimuuliza huku akinyanyuka na kumuangalia jicho kavu.
“Ndiyo maana nakuuliza.”
“Unaniuliza nini?”
“Ili nimjue.”
“Kanipa Gift.”
“Gift ndiyo nani?”
“Mwanao.”
“Mwanangu! Acha utani.”
“Si ndiye ninaye lala naye kila siku.”
“Unajua mimi nakuuliza jambo la maana wewe unaleta utani.”
“Nitamwambia mkeo akiamka, nina imani utamuelewa kwa vile mimi hutanielewa.”
“Ina maana mimba ni yangu?”
“Sijui.”
“Ina maana unataka kumwambia mke wangu ili iweje?”
“Utajua tu, mi kukaa kimya unanifanya mjinga, ulipokuwa ukiniteremsha kufuri uliona raha leo hii unalishangaa tumbo, sasa subiri nipasue jipu kwa mkeo.”
Nini kitaendelea?