Chombezo: Chachandu za Beka wa Tanga

Chombezo: Chachandu za Beka wa Tanga

VAN HEIST

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
1,434
Reaction score
617
SEHEMU YA 01

Akiwa amefikisha umri wa kubalehe, Beka anayetokea Tanga mjini hakuwa bize na masuala ya mabinti kama vijana wa umri wake ambao walikuwa wanakwenda puta kuvifukuzia vidosho.

Mbaya zaidi vijana hao watukutu walikuwa wakiwatokea mpaka dada zao, walichokihitaji ni kumaliza tamaa za miili yao. " Mama Beka , kuna jambo linanitatiza ni vizuri tulizungumze," baba Beka almaarufu kwa jina la Mzee Kibandiko alimwambia mkewe. " Na wewe umeanza , yaani kitendo cha siku mbili hizi kukwambia mgongo unanisumbua unaona shida!" mama Beka alimwambia mumewe . " Hahahaha!" baba Beka alicheka. " Sasa unacheka nini?" mama huyo alihoji.

Kufuatia mkewe kuuliza sababu ya kucheka, Mzee Kibandiko aliyepewa jina hilo kutokana na kupenda kuvaa kibalaghashia kwa staili ya kukiegesha kichwani alimwambia hakuwa na maana aliyoitafsiri. " Sasa unamaanisha nini kama siyo kugeuza maneno baada ya kuona nimekubana ?" mkewe alimwuliza . Mzee Kibandiko alicheka na kumweleza kwamba jambo alilotaka kumuuliza ni kuhusiana na kijana wao Beka . " Umeanza, mtoto kafanyaje ?" mama huyo alihoji . " Siyo kafanyaje , we unamuona yupo sawa na wenzake ?" Mzee Kibandiko alimwuliza mkewe. " Kwani ana tofauti gani, hajafanyiwa suna au hasomi shule nzuri ?" mama huyo alimkomalia mumewe kwa maswali.

Mumewe ambaye kicheko chake kilikuwa karibu , alicheka na kumwambia mkewe kwamba alichotaka kumwambia siyo suala la Beka kufanyiwa suna au kusoma shule nzuri isipokuwa ni zaidi ya hayo . " Eh ! Makubwa ! Madogo yana nafuu!" mama huyo alimwambia mumewe . " Tena tusipokuwa makini yatakuwa makubwa haswa !" Mzee Kibandiko alimwambia mkewe.

Mama huyo alipoona mumewe hafunguki kuhusu alichotaka kumweleza alimwambia hakuwa na lolote zaidi ya kulilia chakula cha usiku ambacho zilipita siku tatu bila kukitafuna. Mzee Kibandiko alicheka lakini kabla hajamwambia hisia alizokuwanazo juu ya kijana wao , mlango wa sebuleni ulifunguliwa Beka aliyetoka shuleni akaingia. " Shikamoo baba, shikamoo mama?" aliwaamkia wazazi wake . " Marhaba mwanangu za shule?" mama mtu alimwuliza mwanaye. " Nzuri mama, " Beka aliitikia. " Vipi we mswahili za huko shuleni kwenu ?" baba yake alimsabahi . " Nzuri tu , pole kwa kazi !" Beka aliyekuwa kidato cha kwanza alimpa pole baba yake kisha akaelekea chumbani kubadili nguo.

Beka aliyekuwa handsome boy alipobadili nguo alitoka na kwenda sebuleni na kunyoosha sehemu ya chakula . Kabla hajafanya chochote, mama yake alimwambia kwenye poti kulikuwa na wali isipokuwa mboga, akamwambia asuburi akaipashe moto . Mama huyo aliinuka akaenda jikoni akawasha jiko la Mchina akawa anapasha moto mboga, wakati huo Beka alikuwa akisoma kipande cha Gazeti la Ijumaa Wikienda ambacho mama yake alifungiwa bidhaa alipotoka sokoni.

Huyu Kulwa Mwaibale na hizi stori zake za mapenzi sijui huwa anazitoa wapi ? Mfano hii ya Chikoko wa Mtwara inafurahisha sana ! Beka alijisemea moyoni wakati akisoma kipande hicho cha gazeti kilichokuwa na chombezo la Chikoko wa Mtwara lilomuhusu kijana aliyekuwa akipenda sana masuala ya mademu badala ya masomo . Wakati akiendelea kusoma , mama yake alirejea akiwa na mboga aliyoipasha moto na kumuwekea kisha mama huyo alikwenda kuketi alipokuwa mumewe. " Sasa mama Beka mimi naona nilichotaka kukueleza tutakiongea baadaye muda huu ngoja niende kwa baba Tunu kuna jambo nataka kuongea naye, " mzee huyo alimwambia mkewe. Mimi nilijua huna lolote zaidi ya kutaka naiii , lakini ngoja nisubiri utakaporudi nisikie unachotaka kuniambia, " mama huyo alimwambia mumewe.

Mzee Kibandiko ambaye kucheka ilikuwa kawaida yake alicheka na kumwambia amsubiri kisha aliomba ampikie tambi. " Na wewe na hizo tambi , hazipiti siku tatu lazima ule tambi, hamia basi huko Unguja ukazile mpaka uchoke!" mkewe alimtania.

Mzee huyo alipoondoka mkewe huku nyuma akajaribu kuchekecha akili kujua mwanaye alikuwa na tatizo gani lakini hakugundua . " Sijui atakuwa kafanyaje lakini kama anamtuhumu kwa mambo mabaya nitamtetea Beka wangu, kwanza hana makundi yeye muda wote ni kujisomea na kunisaidia kazi za nyumbani , akitoka ni kwenda kucheza mpira tu !" mama huyo aliwaza... itaendelea


Source: Global Publishers
 
SEHEMU YA 02

MPENZI msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale
mama yake Beka alipokuwa akijiuliza jambo
ambalo mumewe alitaka kumwambia
kuhusiana na kijana wao Beka lakini hakupata
jibu kwa sababu kijana huyo alikuwa mtulivu
sana. Je , nini kiliendelea?
Songa Nayo …
Wakati Mzee Kibandiko akielekea nyumbani
kwa rafiki yake baba Tunu , akawa
anajisemea moyoni kwamba alihisi Beka
alikuwa na matatizo kwa sababu hakuwahi
kumuona akipiga stori na wasichana kama
walivyofanya wenzake .
“ Huyu mtoto ananishangaza sana mbona
tangu akiwa mdogo anaonekana hana tatizo,
asubuhi akiamka jogoo wake huchangamka
kama kawaida , inakuwaje hajishughulishi na
mabinti kama akina Hussein na Rajabu?”
Mzee huyo alijiuliza .
Mzee Kibandiko ambaye enzi za ujana wake
alikuwa moto wa kuotea mbali kwa mademu
kwani akiwa kidato cha pili tu tayari
aliwapiga mimba wasichana wawili, aliapa
kumchunguza kwa kina Beka ili kujua kama
alikuwa na tatizo amtafutie tiba .
“ Beka ndicho kidume changu pekee cha
mbegu , nikizembea hatutawaona watoto
wake , lazima nipigane , mtoto gani hana
habari kabisa na wasichana wazuri kama
akina Salma na Prisca ?” mzee huyo aliwaza .
Kufuatia kutumia muda mwingi kutafakari
tabia ya mwanaye , alishtukia amefika
nyumbani kwa baba Tunu rafiki yake wa siku
nyingi . Bahati nzuri alimkuta baba Tunu na
mkewe wakiwa wameketi chini ya mti wa
muarobaini wanapiga stori, wakamkaribisha
kwa bashasha.
“ Na nyie mnavyopenda kuwa pamoja utafikiri
mumeoana juzi ?” Mzee Kibandiko aliwatania
wenyeji wake baada ya kukaribishwa .
“ Kwa taarifa yako , jinsi tunavyozeeka penzi
letu ndivyo linavyonoga, mama Tunu
asiponiona anakosa raha nami nisipomuona
nammisi sana!” Baba Tunu alimwambia rafiki
yake huyo, wakacheka .
Baada ya baba Beka kukaa kwenye kiti ,
alimuuliza rafiki yake kuhusu maendeleo
yake kazini akamwambia kwamba hakukuwa
kuzuri.
“ Kuna tatizo gani?” Alimwuliza.
Rafiki yake huyo alimfahamisha kwamba bosi
wao alifumwa akifanya mapenzi na mke wa
mtu ofisini kwake na kwamba alikong’ otwa
hadi kuvunjwa mkono. “ Sasa hilo ni tatizo?
Hiyo ndiyo dawa ya mabosi wapenda
michepuko na wake za watu … mimi
nimeipenda sana hiyo !” Mzee Kibandiko
aliwaambia, wakacheka .
Baba Tunu alimwambia kwamba kitendo cha
bosi wao ambaye alikuwa akiendekeza sana
michepuko kufumaniwa kiliwafurahisha
wengi lakini tatizo ni kwamba tangu
alipobambwa hakufika ofisi hivyo
hawakupata mshahara .
“ Kwani yeye kufumaniwa inahusiana nini na
masuala ya mishahara yenu ?” Mzee
Kibandiko alihoji .
Baba Tunu alimwambia kutokana na mfumo
wa kampuni yao, hakuna mtu mwingine
anayesaini cheki ya mishahara zaidi ya bosi
wao .
“ Kama ni hivyo hilo ni tatizo , pole sana
ndugu yangu, ” mzee Kibandiko alimpa pole
rafiki yake kisha alifungua waleti
akachomoa wekundu watatu wa msimbazi na
kumpatia.
“ Kaka yaani ujio wako ni kama Mungu
kakuleta, hapa tulikuwa tunaumiza vichwa
leo hadi kesho tutaishije na watoto maana
sikuwa na kitu kabisa na ndani hatuna hata
punje ya mchele ,” baba Tunu alimwambia
rafiki yake .
“ Hakuna tatizo ndugu yangu, mambo yako
yakiwa safi utanirudishia shilingi ishirini
inayobaki ikaushie ,” Mzee Kibandiko
alimwambia baba Tunu .
Mke wa baba Tunu alimshukuru sana
shemeji yake , kwa vile alipata fedha
aliwaaga akaelekea sokoni kununua chakula .
“ Kaka siyo siri, umeokoa jahazi lisizame
nilikuwa nachekecha akili nikamkope nani,
yaani asante sana ndugu yangu, ” baba Tunu
alimwambia rafikiye .
Rafiki yake huyo alipomshukuru , Mzee
Kibandiko alimweleza alikuwa amemfuata ili
amsaidie jambo lililokuwa likimtatiza .
“ Eh ! Nini tena?” Baba Tunu alimwuliza .
“ Si mwanao Beka ?” alimwambia.
Baba Tunu aliyekuwa akimuona kijana wake
Said aliyekuwa katika kipindi cha balehe
alivyokuwa akihaha kuwafukuzia mademu
akajua Beka ambaye naye alikuwa katika
kipindi hicho kishamdungua mtu mimba .
“ Vipi kisha mtundika mtu mimba nini? Maana
Said naye anavyohaha kuwafukuzia mabinti
kama fisi aliyeona mzoga wa swala, ” mzee
huyo alimwambia rafiki yake , wakacheka .
“ Si afadhali Said anayehaha , kidume cha
mbegu kinatakiwa kuwa hivyo , ” Mzee
Kibandiko alimwambia rafikiye .
“ Sasa mtoto kafanyaje , kaanza udokozi nini?”
Baba Tunu aliyekuwa na shauku ya kujua
kilichomsibu rafiki yake akamuuliza . itaendelea hapa hapa....

miss nuru
 
SEHEMU YA 03

Mpenzi msomaji, sehemu iliyopita niliishia pale
Mzee Kibandiko baba wa Beka
alipomweleza rafiki yake baba Tunu
kuhusiana na tatizo la kijana wake ambalo
alikuwa bado hajaliweka wazi, rafiki yake
huyo alimwuliza alikuwa kaanza udokozi?
Je, baada ya kumwuliza hivyo alijibiwa nini?
Tuwe pamoja…
ufuatia kuulizwa hivyo, alimfahamisha
kwamba hakuwa mdokozi isipokuwa alihisi
alikuwa na tatizo kubwa mwilini mwake.
“Kaambukizwa virusi vya ukimwi nini?” Baba
Tunu alimwuliza.
Baada ya rafiki yake kumuuliza hivyo, Mzee
Kibandiko alimwambia hakuwa na virusi
isipokuwa alihisi hakuwa kidume cha
mbegu.“Unaposema siyo kidume cha
mbegu unamaanisha jogoo wake hawiki?”
Baba Tunu alimwuliza.
“Haswa, tatizo hilo linanikosesha raha
sana!” Mzee Kibandiko alimwambia rafiki
yake.
“Wewe umejuaje kama jogoo wake hawiki?”
Baba Tunu aliendelea kumwuliza.
Alipoulizwa hivyo, alimwambia alijaribu
kumchunguza kwa muda mrefu kama
alikuwa na rafiki wa kike lakini hakuambulia
kitu.
Kauli hiyo ilimfanya rafiki yake kuangua
kicheko na kumweleza katika jamii wapo
vijana ambao hawana matatizo kiafya ila
hawana habari na mambo ya wasichana.
“Napingana na kauli yako, kwa vijana wa
kizazi hiki cha doticom labda katika kumi
atakuwepo mmoja na akichunguzwa
atakuwa na tatizo flani lakini katika hali ya
kawaida haiwezekani,” Mzee Kibandiko
alimwambia rafiki yake ambaye alicheka.
Kutokana na kauli hiyo, baba Tunu
alimfahamisha rafiki yake huyo kwamba
asiwe na mashaka na afya ya kijana wake
kwani hakuwa na tatizo na vijana waliotulia
wapo.
“Kaka siku zote maji hufuata mkondo, sasa
inakuwaje kwa umri alionao Beka asiwe na
pilika za mabinti? Nashindwa kumuelewa
huyu kijana,” Mzee Kibandiko alimwambia
rafiki yake.
“Kwa hiyo ungekuwa na furaha kama
ungemuona anawashughulikia mabinti wa
wenzako si ndiyo?” Baba Tunu alimwuliza.
“Tena sana, mimi nilipokuwa kama yeye
nilikuwa balaa ndicho kipindi
nilichowadunga mimba mama wa
mwanangu Jamila na mama wa Renatha, si
unaona wanavyonisaidia hivi sasa?” Mzee
Kibandiko alimwambia rafiki yake,
wakacheka.
Rafiki yake huyo alisisitiza kwamba Beka
hakuwa na tatizo na amshukuru Mungu
kumpa kijana mpole, aliyetulia, aliyezingatia
masomo na kuwasaidia kazi za
nyumbani.“Kaka unachonieleza ni sawa
lakini pamoja na kuzingatia masomo na
kutusaidia kazi za nyumbani, inafurahisha
kama unamuona mwanao anapiga stori na
vijana wenzake wa kike tena inafurahisha
zaidi akiwa anazungumza nao hata
chumbani kwake,” Mzee Kibandiko
alimwambia rafiki yake.
“Kaka wewe shukuru kuwa na kijana
aliyetulia, mwenzako Said anatusumbua
sana na masuala ya wanawake…jana tu
kapigana na wenzake, kisa kugombea
msichana,” baba Tunu alimwambia.
“Huyo sasa ndiye mwanaume, kijana wa
kiume lazima awe na mpenzi lakini siyo
Beka yeye akishamaliza kazi zake ni ndani
tu kama mwari,” Mzee Kibandiko aliendelea
kulalamika.
Mwishoni alimuomba ushauri rafiki yake
huyo kama alikuwa akimfahamu mtaalam
yeyote wa tiba za jadi amwelekeze ili
ampeleke kijana wake aliyeamini alikuwa na
tatizo.
“Kaka naomba uelewe Beka hana tatizo,
ukitaka kubaini hilo kesho alfajiri mgongee
chumbani kwake, akifungua mlango tupia
macho eneo la jogoo wake ukiona amefura
ujue hana tatizo,” baba Tunu alimwambia
rafikiye, wakacheka.
“Hilo nalo neno kaka, nitafanya hivyo,”
Mzee Kibandiko alimwambia rafikiye,
wakacheka.
Wakati marafiki hao wakiendelea
kuzungumza, mke wa baba Tunu alirejea
kutoka sokoni, aliwasalimia na kupita mbele
yao akawa anaelekea ndani.
Kwa kuwa mzee Kibandiko na mke wa baba
Tunu kiasili ni watani, baba Beka alimuita
ambapo mama huyo aligeuka kumsikiliza.
“Shemeji, hongera na mshukuru mkubwa
wangu kwa kukulisha vizuri maana
umefungashia si kidogo, ukitembea ni
tentemente hadi mzee anajisikia raha!”Mzee
Kibandiko alimtania shemeji yake.
“Na wewe baba Beka hukui tu, yaani
mambo yako ni yaleyale ya mwaka arobaini
na saba,” mama Tunu alimwambia Mzee
Kibandiko, wote wakacheka.

Itaendelea hapa hapa...
 
Mmmmmhhh!?! Hizo chachandu zitakuwa zinahusu nini kuhusu mlengo wa kimapenzi wa beka!!??
Au ni mtoto si rizki!!?
Duuuuh! Ngoja ni subscribe kwa hii story!! 8)
 
SEHEMU YA 04

ILIPOISHIA :Mpenzi msomaji sehemu iliyopita
niliishia pale baba Tunu alipomeza funda la
mate baada ya kulitazama wowowo la mkewe
lililokuwa likitikisika kulia na kushoto wakati
mama huyo alipokuwa akienda ndani na
kujisemea moyoni kwamba , kufuatia kummisi
sana lazima usiku wangenaniliuu . Je , kilijiri
nini? Songa mbele …
Baada ya mama Tunu kuingia ndani , marafiki
hao waliendelea na maongezi kubwa baba
Tunu alimsisitiza rafiki yake huyo kufanya
kama alivyomshauri ili kubaini kama jogoo
wa Beka alikuwa anawika au la!“Kaka kazi
hiyo nitaifanya alfajiri ya kesho , lazima nijue
kama mwanangu yupo salama au mtoto si
riziki , wewe mtoto gani nyumba zote
zilizotuzunguka kuna mabinti wazuri wana
maziwa ya kuchoma , yeye hana habari nao, ”
Mzee Kibandiko alimwambia rafiki yake .
Kufuatia kauli hiyo , baba Tunu alicheka na
kumwambia rafiki yake huyo hakutulia kabisa
kwani badala ya kufurahi mwanaye alitulia
yeye alikuwa anataka awe kiwembe kwa
mademu. “ Kaka we cheka lakini ukweli ndiyo
huo, mtoto wa kiume lazima aoneshe urijali
wake mapema ndiyo furaha ya wazazi, ” baba
Beka alizidi kutetea hoja yake .
Baada ya kumaliza kuzungumza ishu ya
Beka iliyowachukuwa muda mrefu , mama
Tunu aliyemaliza kupika aliwakaribisha ndani
kwa ajili ya kupata mlo. Marafiki hao wakiwa
wamejumuika mezani kwa ajili ya mlo , baba
Beka alimwita mama Tunu aliyekuwa
anakula jikoni .
“ Ila wewe mwanamke unajua kupika , hivi
nani alikufundisha kukaangiza namna hii ?
maana chakula ni kitamu zaidi ya vitamu !”
Baba Beka alimwuliza . “ Yaani wewe baba
Beka wewe , kuniita kote huko nilifikiri
unataka kuniambia jambo la maana kumbe
utani tu , hivi wewe mwanaume utakua lini ?”
Mama huyo alimwuliza .
“ Sasa mama nimekosea nini? Kukufagilia
kwa kujua kukaangiza ndiyo tatizo ? Kweli
nimejua sababu ya kaka yangu kuwa na
kitambi , ” baba Beka alimwambia shemeji ,
wakacheka .
“ Kama umependa chakula changu
nashukuru , mlete mkeo nimfundishe namna
ya kukupikia , ” mama huyo alimweleza baba
Beka na kuelekea jikoni huku akicheka.
Walipomaliza kula , Baba Beka aliwaaga
wenyeji wake ambapo rafiki yake
alimsindikiza hadi nje wakaagana akarejea
kwake. Alipofika nyumbani kwake, mkewe
alimkaribisha chakula lakini alimwambia
alikuwa ameshiba alikotoka .
“ Yaani baba Beka hapo ndipo unaponikwaza
mwenzako, nimekupikia wali wa nazi
unaoupenda na samaki ili ufurahie kuwa
nyumbani unaniambia umeshiba , ” mkewe
alilalamika.
Hata hivyo , baada ya mumewe kumuomba
msamaha na kumfahamisha kwamba alikula
kwa rafiki yake baba Tunu , mkewe akawa
mpole .
Wakiwa wameketi sebuleni huku Beka akiwa
ametoka, mkewe aliyekuwa na hamu ya
kujua jambo ambalo mumewe alitaka
kumweleza alimuomba afunguke.
Kufuatia kuambiwa hivyo , alimuomba kama
hatajali amweleze usiku lakini mama huyo
alimsihi amwambie kwani moyo wake
ulikuwa juujuu.
“ Kwani mwanao katoka ?” Baba Beka
alimwuliza mkewe.
Mkewe alimwambia hakuwepo na kuhoji
kama angekuwepo angezuia nini, mumewe
alimwambia hakuhitaji asikie aliyotaka
kumweleza kuhusu yeye .
“ Kwani mtoto kafanyaje mbona hutaki
kuniambia?” Mama Beka alimwuliza
mumewe .
“ Hebu twende chumbani nafikiri tutakuwa
huru zaidi , ” Baba Beka alimwambia mkewe
kisha aliinuka na kuelekea chumbani.
Mkewe aliyeacha mlango wa jikoni wazi ,
aliinuka na kwenda kuufunga kuhofia paka
mmoja msumbufu angekula samaki
aliowaandaa. Baba Beka licha ya umri
kusogea alikuwa mtundu sana, alipoingia
chumbani alivua nguo zote na kubaki kama
alivyokuja duniani akalala chali.
Mkewe akiwa hana hili wala lile alipofungua
mlango na kumuona mumewe alivyokuwa,
akaanza kucheka na kumwambia:
Je , kilifuatia nini? Usikose sehemu ifuatayo

itaendelea hapahapa...

Lmntrix, miss nuru
 
Mmmmmhhh!?! Hizo chachandu zitakuwa zinahusu nini kuhusu mlengo wa kimapenzi wa beka!!??
Au ni mtoto si rizki!!?
Duuuuh! Ngoja ni subscribe kwa hii story!! 8)

endelea kufuatilia mkuu utapata ukweli hapahapa
 
SEHEMU YA 05

Mpenzi msomaji, sehemu iliyopita niliishia pale
Mzee Kibandiko ambaye alikuwa mtundu
sana alipoingia chumbani kwake na kuvua
nguo zote na kubaki kama alivyokuja duniani.
Mkewe alipoingia aliishia kucheka na
kumwuliza : “ Hivi wewe baba Beka utakua
lini ? Kwa mfano mwanao akiingia ghafla na
kukukuta hivyo utajisikiaje?”
Je, baba Beka alijibu nini? Songa
mdogomdogoufuatia swali aliloulizwa na
mkewe, mzee huyo alicheka na kumjibu:
“ Ndiyo atakoma kuingia chumbani kwa
wazazi wake bila kubisha hodi. ”
“ Ila siyo vizuri unavyofanya ipo siku
utaumbuka!” mkewe alimwambia mumewe
na kuketi kitandani .
Kutokana na mumewe ‘ mkuu wake wa kaya ’
kuchachamaa, mkewe alipokiona chombo
kilivyokuwa , akapata hisia za yale mambo
yetu .
Mama huyo alimwambia mumewe kwamba
alivyofanya haikuwa vizuri, ambapo mumewe
alimwuliza kosa lake lilikuwa nini?“Si hayo
mambo yako , wewe ukishinda nyumbani
huwezi kutulia na kusubiri usiku , ” mkewe
alimwambia.
“ Wewe ukishikwa na njaa na chakula kipo ,
utasubiri mpaka usiku ?” Baba Beka
alimwuliza mkewe.
Kutokana na swali hilo, mama Beka alicheka
na kumwambia alikuwa akijiendekeza na
kumwambia muda ule haukuwa muafaka kwa
chakula cha usiku kwa sababu kijana wao
angeweza kufika muda wowote.
“ Akifika na kugundua tupo huku chumbani
atajua tunacheza kombolela ya kikubwa, ”
mzee huyo alimjibu mkewe.
Mama huyo ambaye tayari akili yake
iliachana na mambo mengine kutokana na
hisia alizokuwanazo , aliinuka na kwenda
kufunga mlango kwa funguo.
Alipofanya hivyo , alijongea karibu na kitanda
chao akaanza kuvua nguo na alipobakiza ya
mwisho , mumewe akamwambia ‘ stop ’ .
“ Sasa nistop nini, umegahiri ?” mkewe
akamwuliza .
“ Simaanishi hivyo bwana, hebu sogea huku, ”
mzee huyo alimwambia mkewe.
Mkewe ambaye naye alikuwa kaumbika na
kujaaliwa kuwa na nido zilizosimama wima
utafikiri hakuwahi kunyonyesha , alijongea ile
anataka kulala mumewe alimdaka na
kumvutia kifuani kwake .
Licha ya mshua huyo umri kwenda flani hivi
mambo aliyaweza , baada ya kumtuliza
mkewe kifuani alimletea mautundu ya kufa
mtu, mama Beka akaishiwa nguvu . Mzee
huyo ambaye zilipita siku kadhaa bila kula
tunda la mti wa katikati , hakufanya ajizi
alimalizia kukitoa kile kiwalo cha mwisho na
kujilia tende kwa raha zake .
“ Ila wewe baba Beka wewe mh !” mkewe
ambaye alifikishwa Kigoma mwisho wa reli
alimwambia.
“ Nimefanyaje?” Baba Beka alimwuliza
mamsapu wake .
“ Yaani kadiri unavyozeeka ndiyo unakuwa
naniii” mkewe alishindwa kumalizia sentesi
yake akawa anacheka .
“ Umeona eh , sasa ungenibania ungefurahi
namna hiyo ?” mzee huyo alimwambia
mkewe.
Wanandoa hao waliendelea kupiga stori za
hapa na pale ndipo mama Beka akamwomba
mumewe amwambie jambo alilotaka
kumwambia.
“ Oke mke wangu uliyeumbwa ukaumbika ,
unayejua kunitoa uchovu ninapokuwa
nimechoka , unayenipikia chakula kitamu
ninapokuwa na njaa na unayenipa chakula
cha usiku hata mchana, ” mzee huyo
alimwambia mkewe, wakacheka . “ Umeanza
utani wako , ningejua ningekubania , ” mama
huyo alimwambia mkewe.
“ Hahahahaa, usingeweza kwani nakujua sana
unavyokuwa unapomuona mkuu wa kaya
akiwa amekasirika ,” Mzee Kibandiko
alimwambia mkewe wakacheka .
“ Haya niambie sasa hilo jambo la mtoto !”
mama Beka alimwambia mumewe .
Kufuatia kubanwa, mzee huyo alimwuliza
mkewe kama aliwahi kumuona Beka akiwa
bize na mabinti.
“ Kivipi?” mkewe alimwuliza .
“ Wewe nijibu kwanza swali langu!”
Kufuatia mama huyo kuulizwa hivyo ,
alimfahamisha mumewe kwamba mbona
alikuwa akizungumza nao na hata asubuhi
ya siku hiyo alimuona amesimama na Sofia
mtoto wa jirani yao.
“ Na wewe mama Beka , mimi nachotaka
kujua ni zaidi ya kuzungumza nao, ” mzee
huyo alimwambia mkewe.
“ Sasa hapo ndiyo sikuelewi , zaidi ya
kuzungumza nao ndiyo kufanyaje ?” mama
huyo alimwuliza . Kutokana na swali hilo,
mumewe alimwambia si alikuwa amekua , je
aliwahi kumuona na mkamwana wake !
Kutokana na kauli hiyo mkewe alimuelewa
akamjia juu kwamba hakutegemea kama
angemweleza upuuzi wa namna ile .
“ Mama Beka , mimi nakuambia jambo la
maana kuhusu kijana wetu unasema ni
upuuzi, mimi ningekuwa mzembemzembe
kama yeye unafikiri ningekuoa na kumzaa
yeye ?” Baba Beka alihoji kwa hasira .
ITAENDELEA HAPA HAPA

miss nuru Lmntrix
 
Nipo baba, yaan mpaka sasa bado sijajua chachandu za beka zimefanyaje
 
SEHEMU YA 06

Mpenzi msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale
baba Beka alipomjia juu mkewe aliyemuita
mpuuzi kufuatia mzee huyo kumuuliza kama
aliwahi kumuona kijana wao akiwa na
mkamwana wao yaani mpenzi . Je , kilifuatia
nini? Ungana nami
Mama Beka , nakuambia jambo la maana
kuhusu kijana wetu unasema ni upuuzi, mimi
ningekuwa mzembemzembe kama yeye
unafikiri ningekuoa na kumzaa yeye ?” Baba
Beka alihoji kwa hasira .
Licha ya mama huyo kugundua mumewe
alikuwa amekasirishwa na kauli yake ,
hakujishusha badala yake alisisitiza kwamba
alikosea kumuuliza kama aliwahi kumuona
Beka akiwa na mpenzi .
“ Mimi sijakosea , nipo sahihi mke wangu
kwani sitaki aje awe mtoto si riziki !” Baba
Beka alimwambia mkewe. “ Awe mtoto si
riziki kwa sababu gani ? Hivi mbona
unamchulia mtoto mambo mabaya ?” Mama
Beka alihoji .
Kufuatia mkewe kutoa kauli hiyo , mzee
Kibandiko alimweleza kuwa vijana wote
wanaojihusisha na vitendo vya kishoga dalili
zilionekana tangu mapema. “ Unajua sikuelewi
mume wangu, sasa Beka ana dalili gani za
mambo hayo?” mkewe alimwuliza .
“ Sasa kama mtoto hajishughulishi na
masuala ya wanawake kama wanavyofanya
wenzake hapo kuna nini kama siyo
majanga ?” Mzee Kibandiko alimwuliza
mkewe. Mama huyo alimwambia mumewe
amshukuru Mungu kumjaalia utulivu Beka
kwani kuna vijana wamekuwa wasumbufu
kwenye familia zao mpaka wazazi wao
wamewachoka.
“ Kama ni usumbufu wa kutoka na wenzao
wa kike huo hauna tatizo, napenda kumuona
kijana wangu anachangamka kama enzi
zangu si unakumbuka mapigo yangu mama
Beka ?” mzee huyo alimwambia mkewe.
Ingawa mkewe awali hakupendezwa na
maneno ya mumewe , kufuatia kuulizwa kama
alikumbuka mapigo ya mumewe enzi zao
alijikuta akicheka peke yake .
“ Ila baba Beka una maneno mengi sana,
hapa tunamzungumzia Beka siyo mambo
yetu ya zamani, ” mama huyo alimwambia
mumewe .
Wanandoa hao walizungumza mengi lakini
kubwa mama Beka alimsihi mumewe
aachane na mawazo mabaya kuhusu kijana
wao na amshukuru Mungu kuwajalia kijana
aliyetulia.
“ Huo ni mtazamo wako , mimi nitafuatilia
kujua kama ni mzima au ana tatizo kwani
Beka ndiyo jembe ninalolitegemea hivyo
lazima lijue kulima na kung ’oa visiki ,” mzee
huyo alimwambia mkewe, wakacheka .
Kwa kuwa mama huyo alikuwa na majukumu
mengine ya nyumbani , alimuacha mumewe
akiwa amelala akaelekea bafuni
kuoga. “ Hawa wanawake hawajui tu , mtoto
wa kiume aliyepevuka lazima
awachangamkie wenzake wa kike , ” baba
Beka alijisemea moyoni baada ya mkewe
kuondoka.
Baada ya saa moja mbele , mkewe aliingia
chumbani na kumwambia mumewe kwamba
maji ya kuoga yalikuwa tayari pamoja na
chai ya tangawizi aliyokuwa akipenda
kunywa jioni . Mzee huyo ambaye hadi muda
ule alikuwa bado hana nguo mwilini aliinuka ,
mkewe alipotupia macho sehemu ‘muhimu’
na kumuona mkuu wa kaya alivyokuwa
amelala doro akaanza kucheka.
“ Sasa unacheka nini? Huo ndiyo uchokozi!”
mzee huyo alimwambia mkewe aliyekuwa
anaendelea kucheka. Alimpofikia
alimkumbatia kwa kuzungusha mikono katika
kiuno chake na kumbusu shavuni mmwaaa ,
hakuishia hapo akawa anaziminya hipsi zake
zilizokwenda shule.
Mpenzi msomaji, miongoni mwa wanawake
ambao hukosa ustahimilivu wanapobusiwa
na kushikwa sehemu za mapaja ni mama
Beka , alipofanyiwa hivyo alipagawa
kabisa . Mumewe aliyemfanyia vile kwa
makusudi hakuishia kumshika tu maeneo
hayo, aliingiza mkono wake kwenye blauzi
aliyovaa na kushika nido zake zenye ukubwa
wa wastani , sijui akawa anayafanyaje, mama
wa watu akawa anahema.
Wakati akimfanyia vimbwanga hivyo vya
mahabati, naye damu ilimchemka si kidogo
akajisemea moyoni kwamba : “ Mama Beka
huna ujanja lazima tulicheze segere tena. ”
Alichokifanya, alimvutia mkewe kwenye
uwanja wa fundi seremala na kumketisha
akaenda kufunga mlango na kurejea tena
kwa ‘ wife’ wake .
Wawili hao wakiwa tayari kwa kipute cha pili
walikatishwa na Beka aliyeingia ndani na
kuanza kumwita mama yake , kabla mama
yake hajaitika mumewe alimuwahi. “ Beka
unasemaje ?” baba yake alimwuliza . Beka
alimwuliza baba yake ni wapi alikokuwa
mama yake ndipo mzee huyo ambaye
alifahamu kama angemwambia walikuwa
wote chumbani angewaharibia dili lao la
kupeana tende tamu za Uarabuni,
akamdanganya kwamba alitoka.
Kumuondoa kabisa pale nyumbani , alimtuma
aende kwa shangazi yake Pili akamwambie
kesho akirudi kutoka kazini alihitaji
kuzungumza naye hivyo afike pale nyumbani .
Kwa kuwa Beka alikuwa akipenda sana
kuendesha baiskeli, alimwuliza baba yake
kama atumie usafiri huo au angempa nauli ili
apande gari .
ìNenda na baiskeli yako ila uwe muangarifu
barabarani kwani magari ni mengi , î mzee
huyo alimwambia kijana wake .
Mzee huyo alimruhusu atumie usafiri huo
kwa vile alijua angechelewa kurudi kwani
watoto wa dada yake walikuwa wakipenda
sana kuendesha baiskeli hivyo baada ya
Beka kufika kule wangeanza kuendesha.
Beka alipoondoka , mzee huyo alimkabili
mkewe kwa kumpagawisha mpaka mama wa
watu akawa hoi , hakumchelewesha akampa
mkomboti wa haja utafikiri muda mfupi
uliopita hawakuwa pamoja .
ITAENDELEA HAP HAPA...

WABALLA inc miss nuru Lmntrix
 
SEHEMU YA 07

Kwa kuwa Beka alikuwa akipenda sana
kuendesha baiskeli, alimwuliza baba yake
kama atumie usafiri huo au angempa nauli
ili apande gari.“Nenda na baiskeli yako ila
uwe muangarifu barabarani kwani magari ni
mengi,” mzee huyo alimwambia kijana
wake.
Mzee huyo alimruhusu atumie usafiri huo
kwa vile alijua angechelewa kurudi kwani
watoto wa dada yake walikuwa wakipenda
sana kuendesha baiskeli hivyo baada ya
Beka kufika kule wangeanza kuendesha.
Beka alipoondoka, mzee huyo alimkabili
mkewe kwa kumpagawisha mpaka mama
wa watu akawa hoi, hakumchelewesha
akampa mkomboti wa haja utafikiri muda
mfupi uliopita hawakuwa pamoja.
Kutokana na kipute alichopewa na
mumewe, mama wa watu akawa hoi,
mumewe alipomwambia waende wakaoge
akamsihi atangulie.
“Twende bwana tukaoge!” baba Beka
alimwambia mkewe.
“Kwa nilivyochoka wewe nenda ngoja
nipumzike kidogo, maana umeniweza kweli,”
mama huyo alimwambia mumewe.Baba
Beka aliyekuwa anamuelewa vizuri mkewe
anavyokuwa mara baada ya kumchezesha
kwata ipasavyo, kabla ya kuelekea bafuni
aliishia kucheka.
“Kwahiyo hapo roho yako nyeupeee!”
mkewe alimwuliza.
“Tena nyeupe kama theruji, kwa ujumla
nimelifurahia penzi lako mke wangu, wewe
ni mwanamke wa ukweli! “ baba Beka
alimfagilia mkewe.
Baada ya mzee huyo kumsifia mkewe,
akajishika kiunoni na kuanza kufanya
mazoezi ya kurukaruka huku akiwa kama
alivyotia timu duniani, mkewe akaishia
kucheka kwa vituko vyake.
“Hivi baba Beka utakua lini, sasa kufanya
hivyo ndiyo nini?” mkewe alimwuliza.
“Si nafanya mazoezi mama?” alimjibu
mkewe.
Kituko kilichomuacha hoi mkewe ni pale
alipolala chali sakafuni akawa anainua
miguu juu na kuishusha chini huku
akihesabu moja mpaka kumi.Baada ya
mzee huyo kufanya mazoezi yaliyokuwa na
lengo la kumfurahisha mkewe, aliingia
bafuni ambapo alioga akarejea chumbani,
akavaa bukta.
Alipomaliza, alitoka na kuelekea sehemu ya
kulia chakula akafungua chupa na kumimina
chai ya tangawizi kwenye kikombe.
Hakuishia hapo, alifungua chupa iliyokuwa
na asali akachota kijiko kimoja kikubwa na
kuchanganya kwenye tangawizi,
akakoroga.Kabla hajaelekea chumbani
alikomuacha mkewe, alipiga mafunda
mawili ya tangawizi, akajilamba na
kujisemea moyoni ‘safi sana.’
Mzee huyo alikuwa akipenda sana kupata
kinywaji hicho kwa sababu
kilimchangamsha na kilimuongezea nguvu
za simba alipohitaji kumkabili
mkewe.Alipoingia chumbani alimkuta
mkewe kapitiwa na usingizi, akajisemea
moyoni; “chezea mzee Kibandiko wewe?”
Kwa kuwa alibaki peke yake, alikwenda
kukaa sebuleni na kuendelea kunywa
tangawizi huku akitafakari jinsi
walivyopeana raha na mkewe.Kufuatia
kupenda sana vichekesho vya Mzee King
Majuto, aliweka DVD ya vichekesho vya
Majuto akawa anaangalia huku akicheka
peke yake.
Wakati anaendelea kutazama vichekesho
hivyo, mkewe akiwa kajifunga kanga
nyepesi maungoni mwake alitoka chumbani
na kwenda sebuleni.Alipomuona mkewe
akiangalia vituko vya Kingí Majuto,
akacheka na kumtania kwamba kumbe
ndiye alikuwa akimuiga mambo yake.
“Mambo gani?” alimwuliza.
“Si unayofanyaga, wewe si muda mfupi
baada ya kunanii ulianza kurukaruka huku
ukiwa huna nguo?” mkewe akamwuliza.
ITAENDELEA HAPA HAPA..

WABALLA inc miss nuru Lmntrix
 
SEHEMU YA 08

ILIPOISHIA :
Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale
mke wa mzee Kibandiko alipomfuata
mumewe sebuleni na kumkuta akiangalia
DVD ya vichekesho vya Mzee Majuto
akacheka na kumtania kwamba kumbe ndiye
alikuwa akimuiga mambo yake . Je , baada ya
mkewe kutoa kauli hiyo mumewe alisemaje?
Songa mbele . . . ufuatia mkewe kumweleza
hivyo , mzee Kibandiko licha ya kujua mambo
aliyokuwa akiyafanya, alimwuliza ni mambo
gani aliyomuiga Mzee Majuto ?
“ Si unayofanyaga, wewe si muda mfupi
baada ya kunanii ulianza kurukaruka ukiwa
huna nguo mwilini ?” mkewe akamwuliza .
“ Sasa kurukaruka ndiyo nimemuiga Mzee
Majuto?” alimwuliza mkewe.
“ Kuna tofauti gani?” mkewe alimwambia ,
wakacheka .
Mama huyo ambaye siyo siri siku hiyo
alifurahi sana kupewa raha na mumewe ,
alikwenda kuoga kisha akaingia jikoni kupika .
Akiwa anaendelea na zoezi hilo huku
mumewe akiwa sebuleni , alisikia kengele ya
baiskeli ya mwanaye Beka aliyerejea kutoka
kwa shangazi yake .
Beka alipoingia ndani alimsalimia mzazi
wake na kumfahamisha kwamba alimkuta
shangazi na kwamba angefika siku iliyofuata .
Beka alipompa taarifa hiyo mama yake ,
mama huyo alimweleza aende
akamfahamishe baba yake kilichojiri kwa anti
yake .
Kijana huyo aliyemkosesha raha baba yake
kufuatia tabia ya kutokuwa bize na mademu
kama rafiki zake , aliingia na kumwambia
mshua wake kwamba anti yake angefika
kesho yake kama alivyomtuma.
Beka alipompa taarifa hiyo baba yake ,
aliinuka kwenye kochi alilokalia akataka
kuondoka lakini mzazi wake huyo akaomba
asubiri kidogo.
Alichokifanya alimwambia aangalie juu ya
kabati la tv palikuwa na shilingi elfu moja
achukue kwa ajili ya matumizi ya shuleni
siku iliyofuata. Beka alimshukuru baba yake ,
akaenda kabatini akachukua fedha hiyo na
kuelekea chumbani kwake .
“ Kijana handsome boy lakini sijui kwa nini
hana habari na wenzake wa kike , huyu
atakuwa na tatizo lakini kesho alfajiri ndiyo
nitajua kama yupo fiti au la!” mzee Kibandiko
aliwaza.
Baada ya kula chakula cha usiku , kama
kawaida yake , Beka alichukua madaftari
yake na kuwaambia wazazi wake kwamba
anakwenda kujisomea chumbani huku baba
na mama yake wakiwa wanaangalia
tamthiliya.
“ Haya mwanetu sisi tunaburudika na
tamthiliya, uwe na usiku mwema , ” mama
Beka alimwambia kijana wake . Wakati
wanandoa hao wakiendelea kuangalia
tamthiliya, mama Beka aliyekuwa
akimuwazia mambo mazuri mwanaye
alimwambia mumewe :
“ Baba Beka , huyu mtoto kama ataendelea na
juhudi ya kujisomea, atakuja kututoa
kimasomaso hapo baadaye . ”
“
Ni sawa , hata aje awe msomi na kuwa na
fedha nyingi lakini haitakuwa na maana
kama atashindwa kuoa, ” baba Beka
aliyekuwa na wasiwasi sana na mwanaye
kwamba jogoo wake hawiki alimwambia
mkewe.
“ Sasa mtoto asioe kwa nini? Tena kwa
taarifa yako ataoa msomi mwenzake na
familia yao itaishi maisha mazuri , yaani
sipati picha hao wajukuu zetu watakavyoishi
kwa raha, ” mama huyo alimwambia
mumewe .
“ Hivi una uhakika kama mwanao yupo
salama, wewe unafikiri wajukuu wanaokotwa
huko mabondeni ee?” mzee Kibandiko
alimwambia mkewe. “ Hivi kwa nini unasema
hivyo baba Beka ?” mkewe alimwuliza .
Kufuatia swali hilo, mzee Kibandiko
alimwambia mkewe kwamba tatizo kila
anapomweleza kuhusu Beka kutokuwa
mjanja kama wenzake hamuelewi . “ Sikuelewi
kivipi, mbona mtoto hana tatizo lolote ,
anapenda kujisomea, kutusaidia kazi na hana
mambo ya ajabu kama wenzake , akitoka
shule muda mwingi hupenda kuwa
nyumbani !” mama huyo alimfagilia kijana
wake .
“
Sasa wewe unaona kukaa nyumbani au kuwa
goigoi ndiyo tabia nzuri? Mtoto angekuwa na
msichana wake hapo ingekuwa sawa , ” mzee
Kibandiko alimweleza mkewe.
Kufuatia kauli hiyo , mkewe alichukia na
kumjia juu mumewe kwa mambo yake ya
kijinga akainuka na kwenda chumbani.
Mumewe hakuwa na habari naye akabaki
akijisemea moyoni kwamba majibu kama
mwanaye alikuwa kidume cha mbegu au la
angeyapata alfajiri, akazima runinga na
kwenda kulala .
Alipofika chumbani alimkuta mkewe kalala
na kaangalia ukutani huku wowowo lake
pana likiwa limemwagika pande zote za
dunia. ìBahati yako nimechoka vinginevyo
ningekubilingisha mpaka asubuhi , î mzee huyo
alijisemea moyoni .
Alichokifanya alipanda kitandani akalala bila
kumbughudhi mkewe, kutokana na uchovu
wa sebene la nguvu walilolicheza siku hiyo ,
hakuchukuwa muda mrefu akapitiwa na
usingizi.
ITAENDELEA HAPA HAPA

WABALLA Inc miss nuru Lmntrix
 
SEHEMU YA 09

Mpenzi msomaji sehemu iliyopita niliishia
pale mzee Kibandiko aliyebaki sebuleni
alipozima runinga kisha kwenda chumbani
na kumkuta mkewe akiwa amelala. Je,
kilifuatia nini? Songa mbele...
Alipofika chumbani alimkuta mkewe kalala
na kaangalia ukutani huku wowowo lake
pana likiwa limemwagika pande zote za
dunia.
“Bahati yako nimechoka vinginevyo
ningekubilingisha mpaka asubuhi,” mzee
huyo alijisemea moyoni.
Alichokifanya alipanda kitandani akalala bila
kumbughudhi mkewe. Kutokana na uchovu
wa sebene la nguvu walilolicheza siku hiyo,
hakuchukuwa muda mrefu akapitiwa na
usingizi.
Kwa kuwa alipanga kumchunguza kijana
wake Beka kujua kama jogoo wake alikuwa
na hitilafu au la, alfajiri na mapema aliamka
na kwenda chumbani kwake.
Akiwa ndani alimuamsha Beka ambaye
aliamka fasta na kutaka kujua mzazi wake
alitaka kumweleza nini alfajiri ile.Beka
alimuamkia baba yake huku mbele ya bukta
yake pakiwa pamefura, mzazi wake aliitikia
salamu huku akitabasamu na kumuuliza kwa
nini hakujifunika shuka!
Beka bila kujua kama mzazi wake alikuwa
akimchunguza alimjibu kwamba alihisi joto
ndiyo maana hakujifunika shuka.
Wakati kijana huyo akimweleza hivyo mzazi
wake, bado jogoo wake alikuwa
kachangamka jambo lililomfurahisha sana
baba yake.“Oke, Beka endelea kulala ngoja
nijiandae ili niende kazini,” mzee huyo
alimwambia kijana wake ambaye alibaki
kujiuliza sababu ya baba yake kuingia
chumbani kwake asubuhi ile wakati hakuwa
na mazoea hayo.
“Huyu kijana hana tatizo kwani damu
inamchemka kama kawaida, nafikiri
kinachomtatiza ni aibu,” mzee Kibandiko
alijisemea moyoni huku akiangalia marudio
ya taarifa ya habari kupitia runinga ya TBC.
Mkewe alipoamka alimkuta mumewe
akiangalia runinga, walisalimiana kisha
mzee huyo alimwita na kumwambia aketi ili
amwambie jambo flani.
“Hapana baba Beka, wewe huoni kama
kumekucha halafu mwanao akitukuta hapo
unafikiri itakuwaje?” mama Beka aliyejua
mumewe alitaka mambo flani pale sofani
alifunguka.
Baba Beka aliyekuwa akipenda kumpa
mkewe vionjo sehemu yoyote hata sebuleni
Beka alipopitiwa na usingizi, alimwambia
asihofu alitaka kumwambia jambo zuri
kuhusu kijana wao.
Mama Beka ambaye wakati huo alikuwa
kajitanda kanga pekee aliketi ndipo
mumewe alimwambia kwamba asubuhi ile
alikuwa na furaha mno.
“Furaha ya nini?” mkewe alimwuliza.
“Mwanao kanifurahisha sana tena sana!”
mzee huyo alimwambia mkewe.
“Kwani kafanyaje?”
Kufuatia kuulizwa hivyo, alimweleza kuhusu
wasiwasi aliokuwanao kwa mwanaye na
kwamba alifanya uchunguzi na kugundua
hakuwa na tatizo, isipokuwa uwoga ndiyo
ulimtatiza.
“Huo uchunguzi umeufanyaje?” mkewe
alimwuliza.Baba Beka alimweleza kila kitu
mkewe ambaye aliishia kucheka na
kumuuliza atakua lini maana mambo
aliyoyafanya hayakupaswa kufanywa na mtu
mzima kama yeye.
“Mimi kama mzazi napaswa kujua afya ya
mwanangu kiundani, kujua kama anaweza
kuoa na kupata watoto siyo kukaa tu kumbe
mtoto ana Joka la Kibisa,” mzee Kibandiko
alimwambia mkewe, wakacheka.
Wakati wanandoa hao wakipiga stori
walisikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa
wakajua Beka, wakasitisha maongezi
yao.Beka alipofungua mlango aliwasalimia
kisha alikwenda kuoga, huku nyuma baba
yake alimwambia mkewe kwamba walikuwa
na kijana wa ukweli, mama akacheka.
Baada ya mzee huyo kuangalia taarifa ya
habari na Kipindi cha Jambo, alikwenda
kuoga na kunywa chai kisha akaelekea
kazini.
Jioni aliporejea kutoka kazini, kwa mara ya
kwanza alimkuta Beka akipiga stori na binti
mmoja aliitwaye Rhoda wakiwa
wamesimama kibarazani.Kitendo hicho
kilimfurahisha sana na kumshukuru Mungu
wake kusikia kilio chake kwani awali alijua
kijana wake hakuwa kidume cha mbegu.
“Hayo ndiyo mambo ninayoyataka, mtoto
wa kiume unatakiwa uwe shapu siyo
unawaogopa mademu ambao wameletwa
duniani kwa ajili ya wanaume,” baba Beka
alijisemea moyoni wakati akikaribia kuingia
geti la nyumba yake.
“Shikamoo baba na pole kwa kazi,” Beka
alimwamkia baba yake.
Baada ya Beka kumpa heshima yake mzazi
wake, Rhoda naye alimwamkia ambapo
mzee huyo aliitikia salamu yake kwa
uchangamfu wa hali ya juu.
ITAENDELEA HAPAHAPA

WABALLA Inc miss nuru Lmntrix
 
SEHEMU YA 10

Mzee Kibandiko alipoingia ndani, Rhoda
alimwambia Beka alikuwa akimuogopa tu
baba yake kumbe alikuwa mchangamfu
vile . Beka alimfahamisha msichana huyo
kwamba baba yake hakuwa na noma ni mtu
aliyependa utani wa hapa na pale.
“ Basi mimi nilivyokuwa naumuona nilifikiri ni
mkali, hata nilipomuona anakuja moyo ulipiga
pa nikajua angetufurumsha, ” Rhoda
alimwambia Beka , wakacheka .
“ Sasa atufurumshe kwa kosa gani ?” Beka
alimwuliza . Kufuatia swali hilo, msichana
huyo alisema si baada ya kuwakuta
wanazungumza angefikiria walikuwa
wakiongea mambo ya mapenzi !
Kutokana na kauli hiyo , Beka alicheka na
kumweleza baba yake asingeweza kufikiria
hivyo kwa sababu yeye Beka hakuwa na
tabia mbaya zaidi ya kupenda
kujisomea. Rhoda ambaye alikuwa akivutiwa
sana na ‘ uhandsome’ na utulivu wa Beka ,
alimfagilia kwa tabia hiyo na kumwambia
jambo hilo lilimfanya ampende ila basi tu !
“ Basi nini?” Beka alimwuliza .
“ Si wewe upo bize na masomo na kukaa
hapa nyumbani kwenu utafikiria mwari ?”
Rhoda aliyekuwa na lake la moyoni
alimwambia Beka .
“ Mimi siwezi kutembea huku na huko utafikiri
daladala, mimi nataka hapo baadaye niwe
rubani au daktari bingwa wa magonjwa ya
akina mama, ” Beka alimwambia demu huyo,
wakacheka . Wakati wakicheka , mama Beka
aliyekuwa ndani alimwita kijana wake ndipo
baba yake aliyekuwa sebuleni akifuatilia
maongezi ya kijana wake na Rhoda kupitia
dirishani alimuuliza mkewe alikuwa akimuitia
nini.
Mama huyo alisema alitaka amletee jagi la
umeme ili achemshe maji ya kunywa , ili
mwanaye azidi kuzungumza na Rhoda, mzee
huyo aliinuka akachukuwa jagi na
kumpelekea mkewe.
“ Ee ! Makubwa !” Mama huyo aliguna .
“ Makubwa nini?” Mzee Kibandiko alimwuliza
mkewe.
“ Kwani wewe ndiye Beka ?” Mkewe
alimwuliza .
“ Wewe unamtaka Beka au ulikuwa unataka
jagi?” Naye alimwuliza .
“ Haya bwana yameisha, asante kwa kuwa
baba mwema , ” mama Beka alimtania
mumewe , wakacheka .
Baada ya mama huyo kutoa kauli hiyo ,
aliendelea na shughuli zake za jikoni na
mzee huyo alikwenda sebuleni akatega
masikio yake kusikia maongezi ya Beka na
Rhoda.
“
Huyu binti kampenda sana Beka lakini
mwanangu sijui karogwa , anaacha
kuchomekea mambo ya kueleweka yeye
anasema anataka kuwa sijui rubani sijui
dokta bingwa, ” mzee huyo aliwaza .
Hakuishia hapo , alijisemea moyoni kwamba
enzi zake binti kama Rhoda angetafunwa
fasta kwani alikuwa kajileta tunduni
mwenyewe .
Beka ambaye hakusikia alipokuwa akiitwa na
mama yake , aliendelea kupiga stori za
kawaida na Rhoda ambazo silimfanya mzazi
wake aliyekuwa sebuleni kutakamani
kumwambia achomekee ishu ya yale mambo
yetu lakini alishindwa .
Baada ya vijana hao kuzungumza kwa muda
mrefu , Rhoda alimuomba Beka amsindikize
lakini kijana huyo alikataa na kumweleza
muda ule alitaka kumsaidia mama yake
kuchota maji.
“ Hayo maji utachota, nisindikize mpaka pale
kwenye mchungwa halafu unarudi, ” Rhoda
binti ambaye pale mtaani kwao alikuwa
tishio kwa uzuri alimwambia Beka lakini
kijana huyo alikataa .
Kitendo hicho kilimkera sana baba yake
Beka ambaye kuna wakati alikuwa
akisimama dirishani na kuwachungulia.
“ Hili toto ni majanga tupu, binti mzuri kama
huyu kamfuata nyumbani mtoto kajirahisi
hadi mwisho lakini halielewi eti linataka
kumsaidia kuchota maji mama yake , kweli
hili ni ----- la mabwege !” Baba Beka
alipandwa na hasira .
Je , kilifuatia nini? Usikose sehemu ijayo
 
Back
Top Bottom