TANZIA Zimbabwe: Wicknell Chivayo, mke wake wafariki kwenye ajali ya Helikopta

TANZIA Zimbabwe: Wicknell Chivayo, mke wake wafariki kwenye ajali ya Helikopta

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,714
Reaction score
7,813
Serikali ya Zimbabwe (kupitia msemaji mkuu Nick Mangwana) imethibitisha kuwa leo jioni, Septemba 30, 2026, helikopta iliyokuwa na watu 6 (mfanyabiashara mashuhuri, abiria wengine, na marubani wawili) imeanguka katika eneo la Marondera na hakuna aliyepona.

Mamlaka na vyombo vya habari nchini Zimbabwe na kimataifa vimethibitisha kuwa mfanyabiashara huyo ni Wicknell Chivayo, na alikuwa ameambatana na mke wake (Lucy "Lulu" Muteke) pamoja na watu wengine waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Chivayo alikuwa mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa nchini Zimbabwe na alifahamika pia kwa ukaribu wake na viongozi na watu mashuhuri barani Afrika, pamoja na shughuli zake za kutoa misaada na michango mbalimbali. Ripoti za hivi karibuni zimeeleza kuhusu uhusiano wake wa karibu na viongozi wa kisiasa na kidini nchini Zimbabwe.

IMG_20261001_195228_738.jpg

Soma Pia:
ddddddddd.jpg
omaklsdm.jpg
 
Hofu Yatawala Zimbabwe baada ya Helikopta Inayodhaniwa Kumbeba Mfanyabiashara Wicknell Chivayo kuanguka Marondera
HARARE, Zimbabwe

Hali ya sintofahamu na taharuki imetanda nchini Zimbabwe kufuatia ripoti za kuanguka kwa helikopta inayodhaniwa kumbeba mfanyabiashara maarufu na tajiri nchini humo, Wicknell Chivayo.
Tukio hilo limetokea jioni ya leo karibu na mji wa Marondera, ambapo vyombo vya habari vya ndani kupitia mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) viliripoti kushuhudiwa kwa msafara wa zaidi ya magari ya wagonjwa (ambulensi) sita yakikimbia kwa kasi kutoka mji mkuu wa Harare kuelekea eneo la tukio.

Hadi kufikia sasa, mamlaka za usalama na vyombo vya dola bado havijatoa taarifa rasmi kuhusu waliokuwemo ndani ya chombo hicho wala hali halisi ya usalama au afya ya mfanyabiashara huyo. Hali hii imeacha umma ukiwa kwenye hofu kuu huku wananchi wakisubiri taarifa za kina kutoka vyombo husika kufahamu hatima ya safari hiyo na iwapo kuna manusura.

Habari zaidi kuhusiana na tukio hili zitaendelea kuripotiwa kadiri mamlaka zitakavyotoa ufafanuzi rasmi.

View attachment 3681298
View attachment 3681299
View attachment 3681300
 
Be extra ordinary rich or poor!...kwa akili za kibinadamu tunaona tumeyaweza maisha,but tunakula na kunywa na kutamba kwa bure kabisa,chini ya jua,walikuwapo akina mansa mussa,leo hata kaburi lake halijulikani lilipo.(Wealth is useless),
Nchi za ulaya nyingi zimetambua hili,mwanadamu apate nyumba,gari,apate chakula safi na uhakika wa kuweza kuyamudu mahitaji yake ya nafsi,ndiyo furaha halisi ya mwanadamu,amerika leo hii gari umapata kwa dola 500,huna utakopeshwa mara moja,yote hii ni kutengeneza furaha kwa umma wote.
-Usisogelee wala kutamani kuwa sawa na wale wenye mali zinazopindukia,ni wajinga kabisa kwa tamaa zao!....
 
Back
Top Bottom