Chit Chat Praise and Worship Team

Chit Chat Praise and Worship Team

Leo tumeanza rasmi leo.
Bado naendelea kufunga na kuliombea jambo hili kulifanya lipate kibali machoni mwa BWANA na likawe chachu ya mabadiliko ya mioyo ya wana CHIT CHAT.
Leo tunaanza na wimbo huu
"TUFANI INAPOVUMA SANA"
Maisha yetu yamejaa tufani na msongo wa mawazo. Majumbani na makazini kwetu hamna amani ya kweli na wala hamna upendo wa kweli, ni TUFANI.
Bila YESU hatuwezi kushinda.

Tufani Inapovuma




  1. Tufani inapovuma,
    Sana moyoni mwangu,
    Huona pa kujificha,
    Mkononi mwa Mungu,

    Chorus,
    Hunificha, hunificha,
    Adui hatanipata,
    Hunificha, hunificha,
    Mkononi mwake.
  2. Pengine kuna taabu,
    Yanisongeza kwake,
    Najua si hasira,
    Ni ya mapenzi yake.
  3. Adui wakiniudhi,
    Nami nikisumbuka,
    Mungu atavigeuza,
    Vyote viwe baraka.
  4. Niishipo duniani,
    Ni tufani daima,
    Anilindapo rohoni,
    Nitakaa salama.

CC: Madame B, Zion Daughter, ndyoko, Jacaranda, green city


 
Last edited by a moderator:
Afadhali umeirudisha tena hapo sasa tumeelewana best ila mm nitakuwa Mwalimu wa hilo kundi kwani nafaa sana kuwa teacher wao kuwaongoza sauti ya arto, ternal, saprano na sauti nyingine na kuwaweka katika note viilivyo
 
Back
Top Bottom