saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,173
- 6,157
Shida siyo soko huru abiria hana option huu ni uonevu uliopitiliza na uwizi wa nguvu. Wasimame maeneo ya mjini kupata chakula.lakini pia ukumbuke kwenye soko huru, demand inaamua bei kwenye bidhaa zisizodhibitiwa. hata kama ungekuwa wewe una kamgahawa pale nata nzega, mabasi kama kumi yakakwama kwa sababu yoyote ile, nakwambia kikombe cha chai ya siturungi utauza buku. miaka fulani ya nyuma barabara bado zile za wahenga, tulikwama pale kateshi kwenye kamlima kale kalikuwa na utelezi sana,ilikuwa usiku kimvua kinanyesha ni kijijini, tuluziwa chai yenye chumvi sio sukari, chapati nadhani zilikuwa za unga wa mhogo bei siikumbuki ila ilikuwa maradufu. waache tuwapige pesa wasomali hao na wewe hapo ujifunze kitu. halafu investment yao naona ni too risky ukikosana na madereva tu imekula kwake, au latra wakatoa utaratibu mwingine, wamewake. kwa hiyo wanakimbizana kurudisha pesa zao