Haya ni mambo ya kijitakia, wakati mwingine naona no bora tuendelee kupigwa tu kwani tunastahili. Zamani magari yote yalikuwa yanasimama stendi, sehemu yenye hoteli na migahawa mingi, na bei za kila aina, wasafiri wanachjagua wale wapi. Ushindani kwenye hizo hoteli ulikuwa unafanya wenye hoteli kupika vyakula vizuri na kuuza bei rafiki. Mara ''wajanja'' wachache wakaanza kujenga hoteli katikakati ya mapori na kufanya deal na wenye mabasi ili yasimame pale. Ukienda pale hakuna ushindani, msosi ni kidogo na wanapanga bei wanayotaka. Na mbaya zaidi mnapewa dakika kumi tu ili muwe na haraka ya kununua na vichwa vyenu visiweze ku-mind bei ya vyakula. Tukiunga wote na kudai magari yarudie kupaki stendi za umma kama zamani mambo yatabadilika.