Usione Mchungaji Msigwa na Mr.Sugu wamechakazwa mno na wakina mama kule Iringa na Mbeya ambako wanachukuliwa kama wafalme ukaona ni tukio la kawaida.
Jesca Msambatavangu ambaye ni mbunge wa Iringa na Tulia Ackson ambaye ni mbunge wa Mbeya ni wanawake kwa muonekano tu lakini ni mashupavu kama wanaume.
Madam Jesca kama alivyozoeleka kuitwa na wakazi wa Iringa anabebwa na yafuatayo;
Kwanza ni mzungumzaji mzuri sana na katika eneo hili kamuacha Msigwa kwa mbali sana. Kipindi nipo Iringa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020 wakazi wengi wa Kihesa walitamani sana Jesca agombee na lingekuwa Jambo la kushangaza asingefanya hivyo.
Pili, Madam Jesca anazijua siasa za Iringa sana. Mwanamke kupita kwenye nafasi ya uenyekiti wa CCM Mkoa sio Jambo la kitoto. Jesca anazijua mno siasa za Iringa.
Tatu , madam Jesca ni Jasiri mno. Licha ya kusimamishwa uanachama kwa kile kinachodaiwa hujuma aliyofanya kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 hakukata tamaa. Alijirudi na kuomba radhi na hapa ndipo ninasema ni Jasiri kwa sababu wengine huwa wanasusa kabisa.
Kwa upande wa Sugu kule Mbeya ana kazi sana na kushindana na Tulia. Nimebahatika pia kwenda Mbeya ya Sugu na Mbeya ya Tulia nikiri kusema ni Mbeya mbili tofauti. Mbeya ya Tulia maendeleo yanaonekana. Kwa Mbeya, Tulia yawezekana akawa mbunge wa kudumu kwa sababu:
Kwanza, ni msomi. Tulia anatumia usomi wake Kuwapatia wana Mbeya kile wanachokitaka nacho ni maendeleo. Leo hii wanyakyusa hawawezi kuongea sentesi bila kumtaja Tulia.
Pili, Tulia ni mwanasiasa na siasa safi ndio zinazotupatia uongozi bora. Tofauti na mwenzake Sugu ambaye ni mwanaharakati ,zama za siasa za kiharakati zimepitwaa na wakati na zimewachosha sana wana Mbeya.
Tatu, Chini ya Tulia ,Mbeya ipo salama zaidi. Tulia anawajibika kwa wapiga kura wake sana na anawajibika kwa makundi yote bila kujali itikadi zao.
Madam Jesca na Tulia Ackson wana sifa za ziada zinazowatofautisha na Mch. Msigwa na Mr. Sugu hivyo sitoshangazwa na kujitutumua kwa Sugu na Msigwa kutozaa matunda. Kiongozi ni sharti na ni budi awe na sifa na uwezo wa ziada.