Chini ya asilimia 50, tunaenda mzunguko wa pili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chini ya asilimia 50, tunaenda mzunguko wa pili?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 4, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Endapo hakutakuwa na mgombea wa Urais ambaye amepata kura zaidi ya asilimia hamsini basi wagombea wawili waliopata kura nyingi zaidi wataenda kwenye mzunguko wa pili ndani ya siku arobaini baada ya uchaguzi. Kwa minajili hiyo tunaweza kuona kuwa yawezekana Prof. Lipumba ndiye anashikilia ufunguo wa ushindi wa aidha Kikwete au Dr. Slaa. Je, tuko tayari kwa mzunguko wa pili ukitokea kama ilivyotokea Brazili jana Jumapili baada ya mgombea wao wa Urais kuongoza saana kwenye kura za maoni lakini siku ya kura ameshindwa kupata asilimia zaidi ya 50?

  Mwanzoni nilifikiria kuwa sheria yetu inaruhusu mshindi kushinda kwa kura za wingi tu hata kama ni chini ya asilimia 50 kumbe mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi ya 1985 mwaka 1995 yameweka utaratibu wa raundi ya pili ya kura za rais.
   
 2. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sorry, Sijakupata Kabisa.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Iweke hivi:
  Brazili jana Jumapili baada ya mgombea wao wa Urais kupitia
  CHAMA TAWALA kuongoza saana kwenye kura za maoni lakini siku ya kura ameshindwa kupata asilimia zaidi ya 50
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Simple majority?
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  [/COLOR]

  You are very wrong there MMKJJ. A Constituional Amendment that came before 2000 elections removed that proviso that was in use in the 1995 elections. So from 2000 elections the winner is obtained only by simple majority. No run-off.
   
 6. R

  Rugemeleza Verified User

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mzee Mwanakijiji,
  Samahani tafsiri yako ya sheria si sahhi. Mkapa alibadilisha suala hilo miaka ya mwisho ya tisini kuelekea uchaguzi wa mwaka 2000 na kwa mujibu wa katiba ya nchi mshindi ni yule anayepata kura nyingi hivyo hakuna mchuano wa pili.
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,
  Kama kumbukumbu zangu zinanituma vema, sheria uliyoichambua hapo juu ya mshindi kushinda kwa asilimia 50 na zaidi ilikuja kutenguliwa na kurekebishwa na bunge enzi za Mkapa, nadhani ni mwaka 1998 au 1999, ambapo bunge lilikubaliana kwamba mshindi awe ni kwa 'Simple Majority'. Kubadilishwa huku kwa sheria kulitokana na woga wa Mkapa kushindwa, baada ya baadhi ya vyama vya upinzani kuunganisha nguvu katika uchaguzi wa mwaka 2000, hivyo kitishia kuishinda sisiemu.
  I stand to be corrected!

  Idimi
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ok.. kumbe nanii yangu ya awali ilikuwa sahihi.. basi all in all nilidhani JK atakuwa na matumaini kwenye runoff; lakini sasa naamini Dr. Slaa atashinda by simple majority. Thanks for observation, I stand corrected.
   
 9. M

  MLEKWA Senior Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM CAN READ SIGN OF THE TIME ndio maana waliona liko njiani linakuja hichi ndio kingekua kifo cha CCM kwani mgombea wao akikosa 50% angepigwa na chini round ya pili hilo linajulikana.ndio mwalimu Nyerere alipoweka kipengele kile na kusema kuna hatari ya kuwa na Rais aliechaguliwa na minonority ikiwa mtu hakuchaguliwa na watu wasiofika 50%.
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ''simple majority', nakumbuka watu waliuliza hata kama atashinda kwa asilimia 20, wakajibiwa ndiyo. Woga wa CCM walikimbilia kubadili sheria, ndiyo hasa ilimwingiza Amani kwa ku-twist figure 49..., Hii pia ilitokana na Maalim Seif na komandoo,ikabidi komandoo aongezewe zifike 51, hapo CCM wakagundua uwezekano wa round ya pili ni possible siku za mbeleni. Ukweli ni kuwa hawa CCM wanajua kuangalia upepo, walijua ipo siku atatokea mkombozi ingawa hawakujua ni Dr Slaa, wakaweka simple majority. Wanajua sana ku-focus mambo ya kura na ''kuchakachua'' hata miaka 20 ijayo,wasichojua ni kuondoa umasikini na kukuza uchumi wa mtanzania.
   
 11. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  MMM sijakuelewa. Are you serious? au unatupima watu tunajua kiasi gani katiba? for waht I know sheria hiyo ilitenguliwa awamu ya tatu. ni majority wins.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mkuu soma post # 8 ya MMM. Amekubali kuwa alighafilikiwa.
   
 13. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mwanakijiji na wewe umekuwa synnoveta mbona umeyakilia matokeo ya kura ya maoni si ulituambia utatangaza tarehe 3? Au nawewe umetishiwa nini?
   
 14. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wakuu, hii maneno ya kumuandaa mtu afe ili uchaguzi usogezwe, plus Sheikh Yahya na mautabiri yake!!!

  Kuna fact yeyote behind, maana nawaogopa CCM kwa hila!!!
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Baaada ya masahihisho hayo let us go on and kick JK and his CCM pretenders out of the pot of power. Safari hii mianya ya kuiba kura imezibwa ila NEC ndiyo wanajaribu kuifungulia kwa kutukataza wapigakura kulinda kura zetu kwa kuwa mita mia mbili nje ya kituo cha kupiga kura kuwamulika mashushu ambao watatka kupitisha noti kwenye vituo vya kupigia kura.

  NEC tusipowakemea wizi unaweza kuwepo ingawaje si sana kumzuia Dr. Slaa kuingia Ikulu na kuanza kazi ya kurejesha heshima ya Taifa hili.
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,934
  Trophy Points: 280
  Basi sheria hii itakuwa ya kijinga sana. Tuna vyama vingi sana vyenye usajili wa kudumu. Jee vyama kumi vikisimamisha wagomea na anayeongoza kwa simple majority ni mwenye asilimia 12% basi ndiyo imetoka? utakuwa upuuzi kuwa na Rais aliyechaguliwa na 12% ya wananchi.
   
 17. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  you wish.

  According to the National Bureau of Statistics, 20% of Tanzanian are living in urban areas, and 80% in rural areas.

  Wapenzi na washabiki wengi wa Slaa wako mijini. Wengi wao hawajajiandikisha. Na hata waliojiandikisha wengi wao hawatapiga kura. Mwanakijiji mmojawapo wa hao.

  Hivyo basi, kuwa Slaa atashinda mwaka huu ni kulazimisha.

  I am not pro Kikwete, but I am living a factual truth kwamba Kikwete will win, hata kama kwa hiyo simple majority, na hata kama ataacha kufanya kampeni leo.
   
 18. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Hivi ilitenguliwa au ilibadilishwa?
   
 19. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280

  Umesomeka kaka
   
 20. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Ungesema source ni voter's register ndio limekupa majibu ya waliojiandikisha rural na urban ningekubali. Halafu kama umeangalia upigaji kura wa 1995, 2000, 2005 na kukuta wengi wa wapiga kura ni wa rural ningekubali. Otherwise wewe, Shekh Yahya, Tendwa hamna tofauti!!

  Na hiyo source ya NBS uliyotumia inajumuisha na watoto pia? Kwani kwa sasa according to CIA Facts Tanzania asilimia 50% ni under 18!

  Kwa jinsi ulivyoanza na 'according to NBS ...' ndivyo ungeendelea na 'according to voters' register ....' na pia 'according to national election results reports of 1995, 2000, 2005 the trend shows that ....' Fanya hivi halafu utuambie!!
   
Loading...