Ching Shih: Haramia hatari kuwahi kutokea

Ctech

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
754
816
Nadhani ushawahi kusikia neno "Pirates". kuna movie moja maarufu inaitwa "pirates of the Caribbean". Pirates ni Maharamia, hiyo movie kwa kiswahili tungeweza kusema "Maharamia wa Caribbean"

Maharamia ni kikundi cha kihalifu hatari sana, sema uhalifu wao wanaufanyia majini kama vile kuteka meli, boat n.k. kwa Kawaida maharamia hawana huruma hata kidogo ukiingia katika rada zao.

Tukiachana na kudondoka pale amazon ukutane na wale wanawake wenye njaa kali na wanaume sehemu nyingine usiombe udondokee ni kwa maharamia..utakuwa huna bahati(Kidding)😂 Sasa unaambiwa pamoja na Uharamia kuwepo kwa miaka Mingi basi Haramia Hatari kuliko wote kuwahi kutokea katika historia alikuwa ni mwanamke..ndio ni mwanamke kabisa sijakosea!

Ni mwanamke mmoja wa Kichina anaitwa "Ching Shih" Hilo si Jina lake Halisi, hilo neno lina maana ya "Mjane wa Ching".. Ching alikuwa mumewe wa kwanza. Huyu mwanamke alikuwa ni mzuri balaa. Kibongo bongo tungesema ni kama vile "Amedownloadiwa" halafu alikuwa ni kahaba (huduma zetu pendwa zilikuwa zinapatikana hapa😂). Alifikia hiyo nafasi baada ya Kamanda wa kikundi cha kiharamia cha "Red Flag Fleet" kumnunua na kumuoa. Wakati huo huyu binti alikuwa na umri wa miaka 16 tu!

Pamoja na kuwa mke Kamanda huyo alimpa haki sawa kabisa kama alivyotaka mwanamke huyo kwahiyo akawa kamanda pia wa kikundi hicho.

Mwanamke huyu alipata heshima zote kama kamanda wa kikundi hicho, Punde mumewe alifariki naye akawa Nahodha kamili wa kundi Hilo.

Unaambiwa chini ya huyo mwanake kikundi hicho kilimiliki manowari ya kivita zaidi ya 300 na meli za msaada kama 1200..Hatari ilioje!

Unaambiwa mwanamke huyu alimiliki kundi la watu mpaka 80,000 na walitawala maji yote ya upande wa China.
Kuna kipindi serikali ya Uchina ilimwomba na kumsihi Ching Shih aondoke katika bahari ya maeneo ya Uchina aende katikati ya bahari.
 
Chai kama hii huwa inaunguza sana lips maana imezid tangawizi
 
Back
Top Bottom