mbalaka
JF-Expert Member
- Oct 7, 2017
- 2,241
- 2,622
kuna watu humu wakisikia marekani anadaiwa na china, wanajua marekani walienda kukopa fungu kwa wachina.Wachina mpaka leo, kila siku wanaenda Ulaya na America kutafuta wawekezaji. China kwa sasa ndiyo nchi inayoongoza kwa kuvutia mitaji mikubwa toka nje. Makampuni ya Ulaya na America huwekeza wastani wa dola bilioni 80 kwa mwaka.
Ili makampuni yaliyoko China yapate mitaji ya kutosha yanalazimika kujiandikisha kwenye share markets za Europe, America na Australia.
Watu wanaikuza China kuliko uhalisia. Kuna mambo kadhaa ndio ukweli kuhusu China:
1) kwa kiasi kikubwa, China haifanyi ugunduzi wa kiteknolojia. Wao huwa wanakopi kwa njia rasmi za kibiashara au kwa kuiba
2) China bado ni nchi inayoendelea, na kundi kubwa la Wachina ni maskini
3) Katika maendeleo ya watu, China ni nchi ya 89 Duniani. Inazidiwa hata na baadhi ya nchi za Afrika kama Botswana
4) China ni nchi ya pili kwa ukubwa wa pato la Taifa Duniani lakini kiuhalisia ipo chini sana ikilinganishwa na US. Ukubwa wa pato unatokana na ukubwa wa nchi na uwingi wa watu, na siyo kutokana na mifumo bora ya uchumi kama ilivyo kwa mataifa ya Ulaya na America.
5) Asilimia kubwa ya makampuni makubwa yaliyopo China, siyo ya wachina bali ni ya nchi za Magharibi. Kampuni pekee kubwa ya China ni HUAEI
6) Ni uwongo kuwa China imeikopesha US. Pesa ambayo serikali ya Beijing huwa inaidai Washington ni ya mauzo ya government treasury bills. Serikali ya China ili kutaka kujiimarisha na kutengeneza faida huwa wanapenda kununua treasury bills za US
7) Makampuni yote ya nchi za Magharibi yaliyowekeza China yana bima maalum ambayo inayafanya yasipate hasara yoyote kama endapo yatalazimika kufunga na kuondoka. Na yakifanya hivyo, uchumi wa China utayumba kwa kiasi kikubwa kuliko itakavyotokea kwa nchi za Magharibi. China inalijua hilo, ndiyo maana inajiegemeza sana Afrika.
8) Kilichoibadilisha China kwa kiasi kikubwa ni uwekezaji mkubwa wa nchi za Magharibi nchini China baada ya China kuachana na mifumo ya uchumi wa kijamaa. Wachina kwa miaka mingi wameishi katika uchumi duni.