China yatimiza ahadi yake huku Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ikifungwa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
274578581_4682105641900712_4871545712448409150_n.jpg
Mwenge wa Olimpiki umezimwa, na kufunga pazia kwenye Michezo ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, lakini shauku bado inaendelea kutoka kwenye tamasha la michezo ambalo limechangamsha na kuhamasisha dunia katika wakati huu wa janga la Corona.

Thomas Bach, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), alipongeza Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kama "ya kipekee kabisa" wakati akihutubia kwenye hafla ya ufungaji Jumapili usiku. Alisema moyo wa Olimpiki unaweza tu kung'aa sana, kwa sababu watu wa China waliweka jukwaa kwa njia bora na kwa njia salama.

China imetimiza ahadi yake ya kuiletea dunia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi "salama na ya kifahari", kwani pia ilifanya juhudi kubwa kuonyesha ulimwengu wa siku zijazo ambao una wapishi wa roboti wakipika chakula, magari ya kujiendesha na uongozaji unaoungwa mkono na na akili ya bandia (AI).
 
Back
Top Bottom